Nirvana ya Andrew Nyerere

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Yule lama aliyekuwa mwalimu wetu mpya aliisukuma kando ile lectern na akakaa chini mbele yetu katika nafasi ya lotus,akakaa katika jukwaa lililoinuka kidogo ambalo lilikuwepo katika lecture room zote za Tibet. Katika milo yetu katika mabwalo ya kula tulikuwa na lectern ambapo msomaji alikaa au alisimama,kwa sababu wakati wote tulipokuwa tunakula tulisomewa ili akili zetu zijazwe mawazo ya kiroho wakati miili yetu inajazwa tsampa. Haikudhaniwa kuwa ni jambo zuri kula na kufikria chakula. Ilikuwa ni kawaida kwa lecture rasmi kutolewa na mhadhiri amesimama katika lectern,na tulikuwa wepesi kuelewa, kwa vile Mwalimu wetu mpya alikuwa amekaa mbele yetu ilionyesha kwamba alikuwa ni mtu wa aina tofauti. Akasema,''Sasa hivi mlikuwa mnajadili kuhusu Akili Sahihi,na natumaini mko kati hali sahihi ya akili kwa sababu akili ndio chanzo cha matatizo ya Binadamu karibu yote. Hamu za mwili zinaweza kuleta matatizo sana hasa katika jumuia ya monasteri ambapo wakazi wote ni waseja. Kwa hiyo ni lazima kuimiliki akili-kuwa na akili sahihi,kwa sababu tukiwa na akili sahihi tunaweza kuepukana na ukosefu wa furaha ambao unaotokea tunapotamani vitu ambavyo tunajua vizuri sana kwamba hatuwezi kuwa navyo.
''Unajua Buddha alifundisha kwamba wanaume mara nyingi wanapotoshwa na ambacho tunaweza kuita athari ya kutazama[visual impact]. Wanaume,mwanaume wa kawaida ana tabia ya kuwatukuza wanawake''. Alimtazama mvulana mkubwa kidogo,akatabasamu na kusema,''Najua kijana mdogo kama wewe,ambaye wakati mwingine unaambatana na mtawa wa makamu kwenda sokoni,wakati mwingine unaweza kustahili kuitwa'Mperepesa macho',lakini Buddha alifundisha kwamba mambo kama hayo hayafai kwa mtawa kwa sababu hamu ndio baba wa matendo.'' Wazo linakufanya utende jambo ambalo unafahamu kwamba ni kosa.'' Lazima tuchukue Njia ya katikati,hata hivyo,na tusiwe wazuri sana au wabaya sana. Kuna hadithi ya msafiri moja aliyekuwa anasafiri barabarani;muda mfupi uliopita msichana mzuri alipita,na alikuwa na hamu sana ya kufahamiana naye. Kwa bahati mbaya ilibidi aende machakani mara moja kwa shughuli ambayo siyo lazima tuijadili,na alikuwa na hofu kwamba alipoondoka labda yule msichana alikuwa amempita. Alimuona mtawa mzee wa Kibuddha anakuja,na akamsimamisha na kusema,''Unaweza kunieleza,Mheshimiwa Mwalimu, kama mwanamke mzuri sana amepita njia hii katika safari zako?'' Yule mtawa mzee alimtazama na sura isiyo kuwa na hisia zozote na kujibu,''Mwanamke mzuri?Hiyo siwezi kukuambia.Mimi nimefundishwa katika kuwa na akili sahihi,kwa hiyo naweza tu kukuambia kwamba fungu la mifupa lilinipita muda mchache uliopita,kama lilikuwa la mwanaume au la mwanamke si wezi kusema,kwa sababu ilikuwa hainihusu mimi kitu chochote.''
Yule lama alicheka bila kutoa sauti[chuckle] huku akisema,''Hiyo ni Akili Sahihi ambayo imevuka mipaka,ambayo imekuwa kama kichekesho.[By the way,Buddha anabisha kabisa kwamba mtu ana lazima ya kucheka kwa sauti,yaani kucheka kwa zaidi ya 'chuckle' Buddha anacheka kwa 'chuckle',ha ha ha only three times.]Hata vivyo,tuendelee na hili somo ambalo halieleweki kabisa hata kidogo.'' Aliendelea kutueleza kwamba Njia ya Nane Takatifu ina madhumuni,madhumuni ambayo wale wanaoifuata watafikia lengo wanalolitaka,watafikia nirvana. Nirvana maana yake hasa ni kuisha kwa matamanio,mwisho wa kuwa na kutoridhishwa na tamaa. Ni mwisho wa tamaa na aina nyingine za ashiki za mwili ndio utamwezesha mwanaume au mwanamke kuwa katika hali ya raha.
Nirvana ni ukombozi kutokana na mwili,kutokana na ashiki na ulafi wa kila aina wa mwili. Haina maana hata kidogo kwamba ni mwisho wa kupata uzoefu wa aina yoyote,au mwisho wa elimu au mwisho wa maisha. Siyo sahihi kusema kwamba nirvana ni kudumu katika hali ambayo hakuna kitu chochote;hilo ni kosa ambalo limeendelezwa na watu wasiokuwa na ufahamu wanaongea kuhusu mambo ambayo hawayafahamu hata kidogo. Nirvana siyo tu kutafakuri kwa raha kubwa,ila,badale yake,ni uhitimisho wa elimu ya kiroho na uhuru kutokana na hamu za mwili. Hali ya nirvana ni hali ya kuwa katika utakaso,utakaso kwa maana ya kuwa bila ashiki kwa vitu vya mwili. Lakini hata kama ukifikia nirvana,yaani uhuru kutokana na hamu za mwili,bado unaendelea kujifunza mambo ya kiroho na kuendelea katika ngazi nyingine,ghorofa nyingine za kuishi. Wabuddha wanaamini katika Mzunguko wa Kuzaliwa tena,wanaamini kwamba binadamu anazaliwa tena Duniani,anaishi Duniani,halafu anakufa,halafu anarudi tena Duniani katika mwili mwingine,yaani anazaliwa upya Duniani ili masomo aliyojifunza katika maisha yaliyopita yaeleweke vizuri zaidi.

Nirvana siyo pahali,siyo pahali ambapo unaweza kupaonyesha kwenye ramani. Ni hali ya akili,ni hali ya mtu kuwa na mawazo;kufikiri ni moja ya thawabu kubwa za Mbuddha mzuri,na kukosa mawazo ni jambo ambalo ni la kulaaniwa kabisa.
Nirvana siyo kupoteza ufahamu wa nafsi yako binafsi unapofikia mwisho wa maisha yako Duniani,ni kinyume chake kabisa. Kuna Nirvana nyingine ambayo kwa lugha ya Kihindi inaitwa Parinirvana.

''Mbuddha mzuri'',alisema yule Mwalimu wetu lama,''ni mtu mwenye furaha sana,mtu ambaye anajishughulisha na kuwasaidia wengine,mtu ambaye anawafikiria wengine. Mbuddha mzuri ni mtu ambaye haheshimu au kutambua mgawanyiko au matabaka ambayo yapo katika nchi kama India,kwa sababu mtu haifikii hali ya furaha kwa kutegemea mashamba ya wazazi wake. Mwana wa mfalme anaweza kuwa hana furaha,wakati maskini ombaomba anaweza kuwa na furaha. Jinsi alivyozaliwa hakumwezeshi kugundua jinsi ya kuyashinda mateso,hali ya mkoba wa wazazi wake haina uhusiano wowote na hilo. Njia pekee ya kuwa huru kutokana na hamu ambazo siyo kamilifu ni kuifuata njia iliyohakikiwa ya ,Njia Nane ambayo inampa mtu elimu ya kujielewa,na mtu akijielewa anaweza kuwa na furaha ya kudumu.''

Yule lama alitutazama na kusema,'' Nadhani mnafikiria kwamba sisi Wabuddha ndio tuna idadi ya wafuasi wengi kuliko dini yoyote duniani,mnadhani sisi ni wa maana kuliko wote. Hiyo siyo sahihi,kwa sababu sasa hivi moja ya tano tu ya watu wa dunia hii ni Wabuddha. Tunao Wabuddha Thailand,Ceylon,Burma,China,Japan,Korea,Tibet,na idadi fulani India. Kuna aina nyingi za Ubuddha,na zote zinatoka katika chanzo kile kile,kwa hiyo ni wazi kwamba haipaswi uwepo msuguano kati yetu,kwa vile tunatoka kwa mzazi yule yule. Tunaweza wote kufikiri kwa njia yetu wenyewe. Baadaye katika mhadhara wetu tutajadili kuhusu matumizi ya dini,lakini kwa sasa nataka mziseme 'Kinga' tatu.''
Kinga Tatu
Nitajikinga kwa kumtumia Buddha
Nitajikinga kwa Kuyatumia Mafundisho
Nitajikinga kwa kulitumia Kanisa.[la Buddha] Sangha.

Yule lama akasema,''Nyinyi watoto lazima muiseme hiyo asubuhi na kabla ya kulala usiku. Lazima iingie katika akili yenu ya chini[subconcious mind]. Unaweza kuiita mfano wa Kukana Maisha[Great Renunciation] kulikofanywa na Mwanzilishi wa Ubuddha alipoondoka kwenye kasri ya familia na kuvaa joho la mtawa.''

'Nyinyi watoto,'' aliendelea,'' mtaachana na vishawishi vya mwili. Mtajifunza kuwa vijana wa mwenendo mzuri,tabia nzuri,vijana wenye mawazo yaliyotakasika,kwa sababu katika siku zijazo ambazo zitazoifika nchi yetu,siku ambazo uovu utatanda,kwa sababu mambo mabaya yataitokea nchi yetu tunayoipenda,itakuwa lazima kwa vijana wenye tabia nzuri kwenda nje,ambako,kwetu sisi,ni mahali ambako hakujulikani kabisa na kuudumisha utamaduni wetu uwe hai. Kwa hiyo,ni nyinyi wa kizazi kipya ambao ni lazima msome na kujitakasa,kwa sababu sisi wa kizazi cha zamani hatuwezi kuwafuata.''

Alituambia,''Katika safari zenu mtakutana na Wabudha wa aina ya Zen. Mtajiuliza kama maisha yao ya kujitesa ni lazima,kwa sababu kwa Wazen Buddhist wanaamini kwamba wote wanaofundisha na kila kitu kinachofundisha- kama vile vitabu au misahafu-ni kama tu vidole vilivyonyooshwa,vinaonyesha njia ambayo unatakiwa kuchukua. Fikiria watu ambao umewaona,fikiria unapowatazama wahujaji wanatembea hapa Katika Barabara ya Mduara,angalia jinsi ambavyo kama kiongozi fulani au gypsy akionyesha kitu,kama mmoja wetu kwenye madirisha yetu,jinsi macho ya wahujaji wakati wote yanafuata na kukitazama kidole kinachoonyesha badala ya kitu kilichoonyeshwa. Hili ni jambo ambalo limeeleweka na dhehebu ambalo likaja kuitwa Zen Buddhist. Ni imani yao unaweza kuufahamu ukweli kwa uzoefu wako binafsi tu. Ukweli hauwezi kujulikana kwa kusikiliza tu neno lililozingumzwa,au kwa kusoma kurasa iliyochapishwa.Unaweza kupata faida kwa uzoefu wako binafsi tu.

'' Mtu anashajiishwa kusoma,kujifunza Misahafu,na kusikiliza kwa makini mihadhara ya wasomi. Lakini maneno yote yaliyochapishwa na yote yaliyoandikwa yawe tu nishati kwa kufanya kazi kwa akili yako ili unapopata uzoefu unaweza kuufananisha ule uzoefu na Kweli Kubwa kama zilivyopendekezwa na wengine '' Alitabasamu na kusema,''Yote hii ina maana unaweza kwenda mbele kiasi fulani tu kwa kuwa mtu wa nadharia tu,lazima uwe mtu wa vitendo pamoja na kuwa mwanafunzi wa neno lililoandikwa. Inaelezwa kwamba picha moja ina thamani ya zaidi ya maneno elfu moja,lakini nasema uzoefu wa jambo moja tu [experience moja] una thamani kuliko picha elfu.

Alisita kwa muda ,halafu akageuka na kutazama nje ya dirisha. Moyo wangu uliruka kwa sababu nilidhani labda atamuona kiongozi wangu Lama Mingyar Dondup anarudi kutoka Monasteri ya Rose Fence. Lakini hapana,alitugeukia tena na kusema,''Nitawaeleza jambo ambalo nadhani bila shaka litawashtua na kuwafanya mfikiri kuwa Wazen Buddhist ni hayawani wasio na utamaduni,na pia hawayani wanaokufuru. Wakati fulani Japan alikuwepo Mwalimu maarufu sana,mtu aliyekuwa anajulikana kwa maaadli yake mazuri,kwa elimu yake kubwa,na kwa maisha yake ya kujitesa. Wanafunzi walikuja kutoka ulimwengu wote wa Mashariki kuisujudia miguu ya yule Mwalimu na kusoma chini yake. Siku moja alikuwa anatoa mhadhara muhimu sana katika moja ya hekalu za ibada,hekalu ambalo lilikuwa limepambwa na sanamu nyingi za Buddha Elfu Moja,sanamu ambazo zimechongwa kwa umahiri kutokana na miti adimu ya porini. Yule Mwalimu aliwasisimua sana wanafunzi na walikuwa wanamsikiliza kwa makini,na katikati ya mhadhara wake alisimama na wanafunzi wake walishikilia pumzi na kujiuliza atasema nini tena,kwa sababu alikuwa na sifa,siyo ya kusingiiziwa, ya kafanya vituko sana

'' Huyu mtu mwenye hekima alipogeuka upande na kuichuka sanamu ya mbao ya Buddha iliyokuwa karibu zaidi na kuitupa kataika moto,wale wanafunzi walisimama kwa mshtuko. Kwa muda kulikuwa na zogo kubwa,malalamiko,kunyoosha mikono,na kuchezesha miguu. Lakini yule mtu mwenye hekima alisimama shwari mbele ya ule moto,ameipa mgongo ile sanamu ya Buddha iliyokuwa inawaka. Wakati vurugu ilipokwisha akasema kwamba watu wote wana sanamu akilini mwao,kila mtu anaweka mapambo,vitu vya kuabudu,vitu visivyokuwa na faida ambavyo vinachukua nafasi katika akili kama vile sanamu zisizo na faida za mbao zinavyochukua nafasi katika hekalu. Kama alivyosema,njia pekee ya kuendelea ni kuyaunguza matakataka yote katika akili yako,kutekeza kile kinachozuia maendeleo. Yule Mwalimu Mkubwa aligeuka na kukisugua kidole chake juu ya sanamu moja ya Buddha;akaligeukia darasa na kusema,'Hapa kuna vumbi,vumbi juu ya Buddha,lakini hiyo siyo mbaya kama vumbi katika akili.' Tuteketeze sanamu zote za kuchongwa,tuteketeze maoni potofu yanayoishi ndani mwetu,kwa sababu mpaka utakapoisafisha akili yako iliyochafuka kama unavyosafisha ghala iliyochafuka,huwezi kuendelea na kukifikia kilele cha juu cha Njia.''

Mwalimu wetu lama alicheka alipoona sura zetu za kustushwa. Akasema,''Oh! Nyinyi ni wahafidhina sana! Subirini tu mpaka mfike katika lamaseri nyingine. Mtaona kwamba kuna watu ambao hawaoni faida yoyote ya mafundisho ya dini,na mtaona wengine tena ambao wanaosha midomo yao kabla ya kusema neno Buddha,wanaosha midomo yao ili iwe misafi kabla ya kutaja jina takatifu. Lakini hawa ni watu wa itikadi kali,wanazidisha imani yao,wao ambao hawaoni faida ya dini na hao wanaoitukuza kupita kiasi. Dini ni nidhamu ambayo inaweza kuwa na faida kama ukitumia akili ya kawaida[common sense] na kiasi,na Njia ya Katikati,halafu dini inaweza kutanzua matatizo yako yote.''

Sijui,lakini nadhani niliguna au kutoa sauti au kufanya ishara fulani ambayo ilimfanya anione,kwa sababu alisisita kwa muda halafu polepole akaja na kusimama mbele yangu. ''Lobsang,''akasema,''unaonekana unasumbuliwa sana,leo limekutokea jambo kubwa sana.Lakini kwa jinsi ninavyokuona usoni inaelekea kuna jambo lingine kubwa zaidi linakusumbua kuliko kwamba kiongozi wako hajarudi,na hatarudi leo. Niambie ni jambo gani.''

Nilitamani ardhi ingefunguka na niaanguke chini mpaka kwenye moja ya mashimo ya volcano kwa sababu ilibidi nikubali katika nasfi yangu kwamba nilikuwa nawaza mambo ya ajabu kidogo. Kueleza kinaganaga,sikupendezewa na jinsi ilivyonibidi kuishi,na nilidhani kwamba sasa ulikuwa wakati labda. Tuifanye hii kazi tuimalize.

''Mheshimiwa Mwalimu ,' nilisema kwa wasiwasi kidogo,''ni kweli kwamba siridhiki kwa sababu naongozwa kufanya mambo ambayo siyo kufuata matakwa yangu. Nimekuwa nasumbuliwa sana,na nilipokaa katika Golden Roof nashindana na upepo mkali,nilipokuwa nadhani kwamba kifo kinanisubiri,nilikuwa nafurahi,nikifikiria kwamba kifo kitaleta mwisho wa matatizo yangu.''

Yule Mwalimu lama alinitazama kwa huruma. Alijikusanya joho lake na kukaa sakafuni pembeni yangu katika njia ya lotus. ''Lobsang,' alisema.'Tulijadili hili jambo kwa sababu sina shaka kwamba wengi wa vijana hapa wanasumbuliwa na hili wakati mmoja au mwingine. Nimekuwa katika Potala muda mrefu sana,sana,na labda matatizo yako sasa yalikuwa matatizo yangu katika siku zilizopita.''

''Mheshimiwa Mwalimu,'' nilijibu,''Sina uchaguzi,ilibidi niodoke kutoka katika nyumba yangu tajiri. Nilitimuliwa na wazazi wangu ambao walikuwa watu wakubwa sana,na niliambiwa kwamba nitafundihswa kuwa padri. Kwa sababu nilitoka familia ya juu ilibidi nipate mafunzo magumu zaidi ,ya adha kubwa zaidi kuliko kama ningetoka katika familia ya chini. Nilikuwa nina mambo mengi zaidi ya kujifunza,mambo mengi zaidi ya kuteseka. Mguu wangu wa kushoto uliunguzwa mpaka kwenye mfupa bila kosa lolote langu. Miguu yangu yote miwili ilivunjika nilipopulizwa na kimbunga kutoka kwenye mlima,lakini ingawa nachechemea kwa taabu,ingawa nasumbuliwa na maumivu makali wakati wote,bado inabidi nihudhurie darasa. Sasa,Mheshimiwa Mwalimu,sikutaka hata mara moja kuwa mtawa,lakini sikuwa na uchaguzi wowote katika kile nilichokuwa nataka,nimelazimishwa kufanya hii. Dini haina kitu chochote kwangu.''

Lama alinitazama kwa akili niyngi na kusema,''Lakini,Lobsang,hizi ni siku za mapema. Dini itakusaidia sana utakapoelewa jinsi Njia ya Katikati inavyofanya kazi na sheria za maisha haya na maisha baada ya haya. Hapo utakuwa shwari na utaelewa zaid maisha ni nini hasa. Lakini kwa kiwango chako cha sasa,unataka kuwa nini?''

''Nilitazama kutoka katika Golden Roof na nikamuona muendesha boti katika Happy River,na nikafikiri kwamba yale ni maisha huru,raha sana kupiga kasia kwenda na kurudi katika mto ambao kila mtu anaupenda,kukutana na watu wazuri,watu waliotoka India,watu wanaokwenda China,watu wanokwenda kuvuka milima na kurudi nyumbani baadaye na elimu ya ajabu na vitu vya ajabu.Lakini mimi-mimi ni mvulana tu nimekaa hapa naishi maisha ya nidhamu,sina uwezo wa kufanya ninachotaka,kila wakati inanibidi nifuate amri,kila wakati naambiwa kwamba maisha yangu yatakuwa magumu lakini kwamba nafanya kazi kwa lengo maalum,kwamba nitafanya kazi maalum.'' Nikanyamaza kwa muda na kufuta uso wangu na shati langu,halafu nikaendela,kwa nini inanibidi kila wakati kuvumila mambo haya magumu?''

Yule Mwalimu aliuweka mkono wake juu ya bega langu na kusema ,''Maisha ni kama hili darasa;mnakuja hapa,wengine sio kwa hiari yenu,wengine kwa furaha,lakini wote mnakuja hapa kujifunza mambo,na kila mmoja wenu lazima ajifunze kwa
kasi yake kwa sababu hakuna yoyote,mwalimu yoyote,ambaye anaweza kulazimisha maendeleo yako,kwa sababu akifanya hivyo itamaanisha kwamba hautakuwa na elimu iliyokamilika kuhusu somo fulani. Lazima uendelee kwa kasi yako,mbio au pole pole kufuatana na uwezo wako,kufuatana na hamu yako ya kutaka elimu. Maisha yote ni kama darasa;unakuja katika maisha haya kama unavyokuja katika darasa hili. Lakini ukiondoka darasa hili baada ya dakika chache itakuwa sawa na kufa katika maisha haya,kufa katika darasa.Labda kesho utakwenda katika darasa tofauti,ambayo ni karibu sawa na kuzaliwa tena,kuzaliwa katika mwili mpya,katika hali mpya,na masharti mapya. Haufahamu mwalimu atakufundisha nini,hufahamu kwa nini mwalimu atakufundisha,lakini katika miaka ijayo utakapoenda kwenye nchi kuvuka milima yetu utaona kwamba mambo uliyojifunza katika darasa hili na madarasa mengine yatakusaidia sana kwa njia ambazo sasa hivi huwezi kuzielewa.

''Hivyo ndivyo ambavyo kiongozi wangu ,Lama Mingyra Dondup ananiambia kila wakati,'' nilijibu ,''Lakini badosijui kwa nini niafiki kufanya jambo ambalo haliniletei furaha.''

Yule Mwalimu alitazama kuona kama wale watoto wengine walikuwa wanafanya nini,lakini wote walikuwa wamewania,walikuwa wanasikiliza kwa makini kwa sababu ilikuwa inaonekana kama wao wote walikuwa na matatizo kama yangu . Sisi wavulana wote tuliwekwa katika lamaseri si kwa hiari yetu,mimi kwa mfano niliingia nilipokuwa na umri wa miaka saba. Hawa wavulana walikuwa wanasikiliza sasa,wote tulikuwa kama watu ambao tunapita katika giza nene tunatumainia kupata nuru ya mwangaza kuongoza njia yetu.

Mwalimu wetu aliendelea:''Lazima muamue zipo njia ngapi ambazo zimefunguka mbele yenu. Wewe,Lobsang,unaweza kukaa hapa kuwa mtawa,au unaweza kuondoka na kuwa mwendesha mashua. Lakini huwezi kuwa vyote kwa wakati mmoja. Lazima uamue unataka kuwa nini. Kama unataka kuwa mwendesha mashua ,basi ondoka kutoka katika hii lamaseri,na usiifikrie tena hii lamaseri,fikiria tu jinsi ya kuendesha mashuwa. Lakini kama unataka kuwa mtawa-basi sahau kuwa mwendesha mashua,yaweke mawazo yako katika kujifunza kuwa mtawa mzuri. Na kila utakavyozidi kufikiria jinsi ya kuwa mtawa mzuri,ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako.''
Mmoja wa wavulana wengine akaingia kati,na kusema kwa msisimko,''Lakini,Mheshimiwa Mwalimu,mimi pia ilinibidi kuingia katika lamaseri si kwa hiari yangu. Nilitaka kwenda Nepal, kwa sababu nafikiri nitakuwa nina furaha zaidi nikienda Nepal.''

Yule Mwalimu wetu lama alionekana yuko makini,alionekana kama vile hili lilikuwa jambo muhimu sana na sio tu watoto tu ambao hawajui wanaongea juu ya nini. Akajibu kwa uzito mkubwa,''Lakini unawafahamu vizuri watu wa Nepal? Una uzoefu wowote ule nao zaid ya wale wachache ambao umekutana nao. Unayafahamu maisha ya watu wa chini wa Nepal?Kama sio,kama hujaenda mara nyingi kwenye nyumba zao,basi huwezi kusema kwamba unawapenda. Nasema kwamba kwamba kama unataka kubaki hapa Tibet,basi mawazo yako yote fikiria Tibet. Lakini kama unataka kwenda Nepal,basi ondoka Tibet sasa na uende Nepal na usiifikirie zaidi Tibet,kwa sababu kama ukiyagawanya mawazo yako unagawanya nguvu zako. Tunaweza kuwa na mkondo mzuri wa mawazo,au nguvu,au tunaweza kuwa na maji ya mvua yaliyotawanyika ambayo yanaanguka katika sehemu kubwa lakini hayana nguvu.. Kila mmoja wenu lazima aamue anataka kufanya nini,na baada ya kuamua,basi kila mmoja wenu azingatie kwa makini na akili ambayo haijagawanyika kufanikisha anachotaka kuwa,kwa sababu ukiamua kwenda Nepal na nusu moja ya akili yako na nusu nyingine inataka kubaki Tibet,basi unakuwa katika hali ya kushindwa kuamua wakati wote,una wasiwasi wakati wote,na huwezi wakati wowote kupata amani ya akili au shwari. Hii ndio moja ya nguvu kubwa duniani,moja ya Sheria kubwa ambayo lazima uikumbuke. Mgawanye adui na utamtawala adui,kaa mwenyewe bila kugawanyika na utamshinda adui aliyegawanyika. Adui anaweza kuwa kutoamua[indecision],woga na kutokuwa na hakika[uncertainty].''

Wote tulitazamana ,na tukafikiria kwamba huyu Mwalimu alikuwa anatuelewa vizuri. Ilikuwa ni vizuri zaidi kuwa na mtu ambaye alikuwa mtu[a man who was a man],mtu ambaye tungeweza kuongea naye na ambaye angeweza kuongea na sisi,na sio tu kutuambia mambo. Tulimfikiria yule mwalimu wa Kihindi jinsi alivyokuwa na majigambo na dharau[superscilious]. Nikasema,''Mheshimiwa Mwalimu,nina swali:Kwa nini watu wengine ni wakatili sana na wengine wana moyo wa kuelewa na ni wapole?''
Yule Mwalimu alitabasamu na kusema,''Lobsang,saa zimekwenda sana usiku kuanza kujadili maswala mazito kama hayo,lakini nakuahidi kwamba tujadili mambo kama hayo,pia tutajadili matumizi mazuri na mabaya ya dini zote.Lakini nadhani tumefanya kazi muda mrefu wa kutosha kwa siku moja,kwa hiyo wote kila mmoja aendelee na shughuli zake.'' Alisimama,na wavulana wote walisimama pamoja naye. Lama aliona kwamba nilikuwa nina matatizo kwa hiyo aliinama,na kuweka mkono wake kunizunguka,na akanisaidia kuinuka kwa urahisi na kwa shwari kama vile alikuwa amezoea kufanya hivyo kila siku ya maisha yake.

'' Nendeni sasa watoto watoto,'' alisema,''ama sivyo mtakuwa mnajikwaa na kuanguka katika giza na hatutaki watu wengine wawe na matatizo ya muda ya kuumia miguu.
 
Andy,

Nakusoma, ahsante kwa tafsiri, ila ni vigumu sana kwa engi tuliolelewa katika misingi ya kiafrika na Judeo-Christian principleskuelewa.

Ila swali moja dogo, kuna watu waasema "Mwaimu" (JKN) alikuwa anaaamini katika mambo mengi ya u buddha, na Pannasekara ameshaniambia kwamba alikuwa anatoa hata sadaka pale temple ya Upanga, magunia ya chakula kwa watawa. Na hata kiwanja alihusika sana kuwapa. Ni kweli?

Unaweza kuhakikisha.

Naendelea kukusoma, ahsante kwa tafsiri Unaweza kutoa chanzo? Naahjaribu kupitia Dhammapada na vitabu vyangu vingine vya kale vya u buddha.
 
.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}

.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;} Yule lama aliyekuwa mwalimu wetu mpya aliisukuma kando ile lectern na akakaa chini mbele yetu katika nafasi ya lotus,akakaa katika jukwaa lililoinuka kidogo ambalo lilikuwepo katika lecture room zote za Tibet. Katika milo yetu katika mabwalo ya kula tulikuwa na lectern ambapo msomaji alikaa au alisimama,kwa sababu wakati wote tulipokuwa tunakula tulisomewa ili akili zetu zijazwe mawazo ra kiroho wakati miili yetu inajazwa tsampa. Haikudhaniwa kuwa ni jambo zuri kula na kufikria chakula. Ilikuwa ni kawaida kwa lecture rasmi kutolewa na mhadhiri amesimama katika lectern,na tulikuwa wepesi kuelewa, kwa vile Mwalimu wetu mpya alikuwa amekaa mbele yetu ilionyesha kwamba alikuwa ni mtu wa aina tofauti. Akasema,''Ssa hivi mlikuwa mnajadili kuhusu Akili Sahihi,na natumaini mko kati hali sahihi ya akili kwa sababu akili ndio chanzo cha matatizo ya Binadamu karibu yote. Hamu za mwili zinaweza kuleta matatizo sana hasa katika jumuia ya monasteri ambapo wakazi wote ni waseja. Kwa hiyo ni lazima kuimiliki akili-kuwa na akili sahihi,kwa sababu tukianzisha akili sahihi tunaweza kuepukana na ukosefu wa furaha ambao unaotokea tunapotamani vitu ambavyo tunajua vizuri sana kwamba hatuwezi kuwa navyo.
''Unajua Buddha alifundisha kwamba wanaume mara nyingi wanapotoshwa na ambacho tunaweza kuita athari ya kutazama[visual impact]. Wanaume,mwanaume wa kawaida ana tabia ya kuwatukuza wanawake''. Alimtazama mvulana mkubwa kidogo,akatabasamu na kusema,''Najua kijana mdogo kama wewe,ambao wakati unaambatana na mtawa wa makamu kwenda sokoni,wakati mwingine unaweza kustahili kuitwa'Mperepesa macho',lakini Buddha alifundisha kwamba mambo kama hayo hayafai kwa mtawa kwa sababu hamu ndio baba wa matendo.'' Wazo linakufanya utende jambo ambalo unafahamu kwamba ni kosa.'' Lazima tuchukue Njia ya katikati,hata hivyo,na tusiwe wazuri sana au wabaya sana. Kuna hadithi ya msafiri moja aliyekuwa anasafiri barabarani;muda mfupi uliopita msichana mzuri alipita,na alikuwa na hamu sana ya kufahamiana naye. Kwa bahati mbaya ilibidi aende machakani mara moja kwa shughuli ambayo siyo lazima tuijadili,na alikuwa na hofu kwamba alipoondoka labda yule msichana alikuwa amempita. Alimuona mtawa mzee wa Kibuddha anakuja,na akamsimamisha na kusema,''Unaweza kunieleza,Mheshimiwa Mwalimu, kama mwanamke mzuri sana amepita njia hii katika safari zako?'' Yule mtawa mzee alimtazama na sura isiyo kuwa na hisia zozote na kujibu,''Mwanamke mzuri?Hiyo siwezi kukuambia.Mimi nimefundishwa katika kuwa na akili sahihi,kwa hiyo naweza tu kukuambia kwamba fungu la mifupa lilinipita muda mchache uliopita,kama lilikuwa la mwanaume au la mwanamke si wezi kusema,kwa sababu ilikuwa hainihusu mimi kitu chochote.''
Yule lama alicheka bila kutoa sauti[chuckle] huku akisema,''Hiyo ni Akili Sahihi ambayo imevuka mipaka,ambayo imekuwa kama kichekesho.[By the way,Buddha anabisha kabisa kwamba mtu ana lazima ya kucheka kwa sauti,yaani kucheka kwa zaidi ya 'chuckle' Buddha anacheka kwa 'chuckle',ha ha ha only three times.]Hata vivyo,tuendelee na hili somo ambalo halieleweki kabisa hata kidogo.'' Aliendelea kutueleza kwamba Njia ya Nane Takatifu ina madhumuni,madhumuni ambayo wale wanaoifuata watafikia lengo wanalolitaka,watafikia nirvana. Nirvana maana yake hasa ni kuisha kwa matamanio,mwisho wa kuwa na kutoridhishwa na tamaa. Ni mwisho wa tamaa na aina nyingine za ashiki za mwili ndio utamwezesha mwanaume au mwanamke kuwa katika hali ya raha.
Nirvana ni ukombozi kutokana na mwili,kutokana na ashiki na ulafi awa kila aina wa mwili. Haina maana hata kidogo kwamba ni mwisho wa kupata uzoefu wa aina yoyote,au mwisho wa elimu au mwisho wa maisha. Siyo sahihi kusema kwamba nirvana ni kudumu katika hali ambayo hakuna kitu chochote;hilo ni kosa ambalo limeendelezwa na watu wasiokuwa na ufahamu wanaongea kuhusu mambo ambayo hawayafahamu hata kidogo. Nirvana siyo tu kutafakuri kwa raha kubwa,ila,badale yake,ni uhitimisho wa elimu ya kiroho na uhuru kutokana na hamu za mwili. Hali ya nirvana ni hali ya kuwa katika utakaso,utakaso kwa maana ya kuwa bila ashiki kwa vitu vya mwili. Lakini hata kama ukifikia nirvana,yaani uhuru kutokana na hamu za mwili,bado unaendelea kujifunza mambo ya kiroho na kuendelea katika ngazi nyingine,ghorofa nyingine za kuishi. Wabuddha wanaamini katika Mzunguko wa Kuzaliwa tena,wanaamini kwamba binadamu anazaliwa tena Duniani,anaishi Duniani,halafu anakufa,halafu anarudi tena Duniani katika mwili mwingine,yaani anazaliwa upya Duniani ili masomo aliyojifunza katika maisha yaliyopita yaeleweke vizuri zaidi.

Nirvana siyo pahali,siyo pahali ambapo unaweza kupaonyesha kwenye ramani. Ni hali ya akili,ni hali ya mtu kuwa na mawazo;kufikiri ni moja ya thawabu kubwa za Mbuddha mzuri,na kukosa mawazo ni jambo ambalo ni la kulaaniwa kabisa.
Nirvana siyo kupoteza ufahamu wa nafsi yako binafsi unapofikia mwisho wa maisha yako Duniani,ni kinyume chake kabisa. Kuna Nirvana nyingine ambayo kwa lugha ya Kihindi inaitwa Parinirvana.

''Mbuddha mzuri'',alisema yule Mwalimu wetu lama,''ni mtu mwenye furaha sana,mtu ambaye anajishughulisha na kuwasaidia wengine,mtu ambaye anawafikiria wengine. Mbuddha mzuri ni mtu ambaye haheshimu au kutambua mgawanyiko au matabaka ambayo yipo katika nchi kama India,kwa sababu mtu haifikii hali ya furaha kwa kutegemea mashamba ya wazazi wake. Mwana wa mfalme anaweza kuwa hana furaha,wakati maskini ombaomba anaweza kuwa na furaha. Jinsi alivyozaliwa hakumwezeshi kugundua jinsi ya kuyashinda mateso,hali ya mkoba wa wazazi wake haina uhusiano wowote na hilo. Njia pekee ya kuwa huru kutokana na hamu ambazo siyo kamilifu ni kuifuata njia iliyohakikiwa ya ,Njia Nane ambayo inampa mtu elimu ya kujielewa,na mtu akijielewa anaweza kuwa na furaha ya kudumu.''

Yule lama alitutazama na kusema,'' Nadhani mnafikiria kwamba sisi Wabuddha ndio tuna idadi ya wafuasi wengi kuliko dini yoyote duniani,mnadhani sisi ni wa maana kuliko wote. Hiyo siyo sahihi,kwa sababu sasa hivi moja ya tano tu ya watu wa dunia hii ni Wabuddha. Tunao Wabuddha Thailand,Ceylon,Burma,China,Japan,Korea,Tibet,na idadi fulani India. Kuna aina nyingi za Ubuddha,na zote zinatoka katika chanzo kile kile,kwa hiyo ni wazi kwamba haipaswi uwepo msuguano kati yetu,kwa vile tunatoka kwa mzazi yule yule. Tunaweza wote kufikiri kwa njia yetu wenyewe. Baadaye katika mhadhara wetu tutajadili kuhusu matumizi ya dini,lakini kwa sasa nataka mziseme 'Kinga' tatu.''
Kinga Tatu
Nitajikinga kwa kumtumia Buddha
Nitajikinga kwa Kuyatumia Mafundisho
Nitajikinga kwa kulitumia Kanisa.[la Buddha] Sangha.

Yule lama akasema,''Nyinyi watoto lazima muiseme hiyo asubuhi na kabla ya kulala usiku. Lazima iingie katika akili yenu ya chini[subconcious mind]. Unaweza kuiita mfano wa Kukana Maisha[Great Renunciation] kulikofanywa na Mwanzilishi wa Ubuddha alipoondoka kwenye kasri ya familia na kuvaa joho la mtawa.''

'Nyinyi watoto,'' aliendelea,'' mtaachana na vishawishi vya mwili. Mtajifunza kuwa vijana wa mwenendo mzuri,tabia nzuri,vijana wenye mawazo yaliyotakasika,kwa sababu katika siku zijazo ambazo zitazoifika nchi yetu,siku ambazo uovu utatanda,kwa sababu mambo mabaya yataitokea nchi yetu tunayoipenda,itakuwa lazima kwa vijana wenye tabia nzuri kwenda nje,ambako,kwetu sisi,ni mahali ambako hakujulikani kabisa na kuudumisha utamaduni wetu uwe hai. Kwa hiyo,ni nyinyi wa kizazi kipya ambao ni lazima msome na kujitakasa,kwa sababu sisi wa kizazi cha zamani hatuwezi kuwafuata.''

Alituambia,''Katika safari zenu mtakutana na Wabudha wa aina ya Zen. Mtajiuliza kama maisha yao ya kujitesa ni lazima,kwa sababu kwa Wazen Buddhist wanaamini kwamba wote wanaofundisha na kila kitu kinachofundisha- kama vile vitabu au misahafu-ni kama tu vidole vilivyonyooshwa,vinaonyesha njia ambayo unatakiwa kuchukua. Fikiria watu ambao umewaona,fikiria unapowatazama wahujaji wanatembea hapa Katika Barabara ya Mduara,angalia jinsi ambavyo kama kiongozi fulani au gypsy akionyesha kitu,kama mmoja wetu kwenye madirisha yetu,jinsi macho ya wahujaji wakati wote yanafuata na kukitazama kidole kinachoonyesha badala ya kitu kilichoonyeshwa. Hili ni jambo ambalo limeeleweka na dhehebu ambalo likaja kuitwa Zen Buddhist. Ni imani yao unaweza kuufahamu ukweli kwa uzoefu wako binafsi tu. Ukweli hauwezi kujulikana kwa kusikiliza tu neno lililozingumzwa,au kwa kusoma kurasa iliyochapishwa.Unaweza kupata faida kwa uzoefu wako binafsi tu.

'' Mtu anashajiishwa kusoma,kujifunza Misahafu,na kusikiliza kwa makini mihadhara ya wasomi. Lakini maneno yote yaliyochapishwa na yote yaliyoandikwa yawe tu nishati kwa kufanya kazi kwa akili yako ili unapopata uzoefu unaweza kuufananisha ule uzoefu na Kweli Kubwa kama zilivyopendekezwa na wengine '' Alitabasamu na kusema,''Yote hii ina maana unaweza kwenda mbele kiasi fulani tu kwa kuwa mtu wa nadharia tu,lazima uwe mtu wa vitendo pamoja na kuwa mwanafunzi wa neno lililoandikwa. Inaelezwa kwamba picha moja ina thamani ya zaidi ya maneno elfu moja,lakini nasema uzoefu wa jambo moja tu [experience moja] una thamani kuliko picha elfu.

Alisita kwa muda ,halafu akageuka na kutazama nje ya dirisha. Moyo wangu uliruka kwa sababu nilidhani labda atamuona kiongozi wangu Lama Mingyar Dondup anarudi kutoka Monasteri ya Rose Fence. Lakini hapana,alitugeukia tena na kusema,''Nitawaeleza jambo ambalo nadhani bila shaka litawashtua na kuwafanya mfikiri kuwa Wazen Buddhist ni hayawayani wasio na utamaduni,na pia hawayani wanaokufuru. Wakati fulani Japna alikuwepo Mwalimu maarufu sana,mtu aliyekuwa anajulikana kwa maaadli yake mazuri,kwa elimu yake kubwa,na kwa maisha yake ya kujitesa. Wanafunzi walikuja kutoka ulimwengu wote wa Mashariki kuisujudia miguu ya yule Mwalimu na kusoma chini yake. Siku moja alikuwa anatoa mhadhara muhimu sana katika moja ya hekalu za ibada,hekalu ambalo lilikuwa limepambwa na sanamu nyingi za Buddha Elfu Moja,sanamu ambazo zimechongwa kwa umahiri kutokana na miti adimu ya porini. Yule Mwalimu aliwasisimua sana wanafunzi na walikuwa wanamsikiliza kwa makini,na katika ya mhadhara wake alisimama na wanafunzi wake walishikilia pumzi na kujiuliza atasema nini tena,kwa sababu alikuwa na sifa,siyo ya kusigniziwa, ya kafanya vituko sana.

'' Huyu mtu mwenye hekima alipogeuka upande na kuichuka sanamu ya mbao ya Buddha iliyokuwa karibu zaidi na kuitupa kataika moto,wale wanafunzi walisimama kwa mshtuko. Kwa muda kulikuwa na zogo kubwa,malalamiko,kunyoosha mikono,na kuchezesha miguu. Lakini yule mtu mwenye hekima alisimama shwari mbele ya ule moto,ameipa mgongo ile sanamu ya Buddha iliyokuwa inawaka. Wakati vurugu ilipokwisha akasema kwamba watu wote wana sanamu akilini mwao,kila mtu anaweka mapambo,vitu vya kuabudu,vitu visivyokuwa na faida ambavyo vinachukua nafasi katika akili kama vile sanamu zisizo na faida za mbao zinavyochukua nafasi katika hekalu. Kama alivyosema,njia pekee ya kuendelea ni kuyaunguza matakataka yote katika akili yako,kutekeza kile kinachozuia maendeleo. Yule Mwalimu Mkubwa aligeuka na kukisugua kidole chake juu ya sanamu moja ya Buddha;akaligeukia darasa na kusema,'Hapa kuna vumbi,vumbi juu ya Buddha,lakini hiyo siyo mbaya kama vumbi katika akili.' Tuteketeze sanamu zote za kuchongwa,tuteketeze maoni potofu yanayoishi ndani mwetu,kwa sababu mpaka utakapoisafisha akili yako iliyochafuka kama unavyosafisha ghala iliyochafuka,huwezi kuendelea na kukifikia kilele cha juu cha Njia.''

Mwalimu wetu lama alicheka alipoona sura zetu za kustushwa. Akasema,''Oh! Nyinyi ni wahafidhina sana! Subirini tu mpaka mfike katika lamaseri nyingine. Mtaona kwamba kuna watu ambao hawaoni faida yoyote ya mafundisho ya dini,na mtaona wengine tena ambao wanaosha midomo yao kabla ya kusema neno Buddha,wanaosha midomo yao ili iwe misafi kabla ya kutaja jina takatifu. Lakini hawa ni watu wa itikadi kali,wanazidisha imani yao,wao ambao hawaoni faida ya dini na hao wanaoitukuza kupita kiasi. Dini ni nidhamu ambayo inaweza kuwa na faida kama ukitumia akili ya kawaida[common sense] na kiasi,na Njia ya Katikati,halafu dini inaweza kutanzua matatizo yako yote.''

Sijui,lakini nadhani niliguna au kutoa sauti au kufanya ishara fulani ambayo ilimfanya anione,kwa sababu alisisita kwa muda halafu polepole akaja na kusimama mbele yangu. ''Lobsang,''akasema,''unaonekana unasumbuliwa sana,leo limekutokea jambo kubwa sana.Lakini kwa jinsi ninavyokuona usoni inaelekea kuna jambo lingine kubwa zaidi linakusumbua kuliko kwamba kiongozi wako hajarudi,na hatarudi leo. Niambie ni jambo gani.''

Nilitamani ardhi ingefunguka na niaanguke chini mpaka kwenye moja ya mashimo ya volcano kwa sababu ilibidi nikubali katika nasfi yangu kwamba nilikuwa nawaza mambo ya ajabu kidogo. Kueleza kinaganaga,sikupendezewa na jinsi ilivyonibidi kuishi,na nilidhani kwamba sasa ulikuwa wakati labda. Tuifanye hii kazi tuimalize.

''Mheshimiwa Mwalimu ,' nilisema kwa wasiwasi kidogo,''ni kweli kwamba siridhiki kwa sababu naongozwa kufanya mambo ambayo siyo kufuata matakwa yangu. Nimekuwa nasumbuliwa sana,na nilipokaa katika Golden Roof nashindana na upepo mkali,nilipokuwa nadhani kwamba kifo kinanisubiri,nilikuwa nafurahi,nikifikiria kwamba kifo kitaleta mwisho wa matatizo yangu.''

Yule Mwalimu lama alinitazama kwa huruma. Alijikusanya joho lake na kukaa sakafuni pembeni yangu katika njia ya lotus. ''Lobsang,' alisema.'Tulijadili hili jambo kwa sababu sina shaka kwamba wengi wa vijana hapa wanasumbuliwa na hili wakati mmoja au mwingine. Nimekuwa katika Potala muda mrefu sana,sana,na labda matatizo yako sasa yalikuwa matatizo yangu katika siku zilizopita.''

''Mheshimiwa Mwalimu,'' nilijibu,''Sina uchaguzi,ilibidi niodoke kutoka katika nyumba yangu tajiri. Nilitimuliwa na wazazi wangu ambao walikuwa watu wakubwa sana,na niliambiwa kwamba nitafundihswa kuwa padri. Kwa sababu nilitoka familia ya juu ilibidi nipate mafunzo magumu zaidi ,ya adha kubwa zaidi kuliko kama ningetoka katika familia ya chini. Nilikuwa nina mambo mengi zaidi ya kujifunza,mambo mengi zaidi ya kuteseka. Mguu wangu wa kushoto uliunguzwa mpaka kwenye mfupa bila kosa lolote langu. Miguu yangu yote miwili ilivunjika nilipopulizwa na kimbunga kutoka kwenye mlima,lakini ingawa nachechemea kwa taabu,ingawa nasumbuliwa na maumivu makali wakati wote,bado inabidi nihudhurie darasa. Sasa,Mheshimiwa Mwalimu,sikutaka hata mara moja kuwa mtawa,lakini sikuwa na uchaguzi wowote katika kile nilichokuwa nataka,nimelazimishwa kufanya hii. Dini haina kitu chochote kwangu.''

Lama alinitazama kwa akili niyngi na kusema,''Lakini,Lobsang,hizi ni siku za mapema. Dini itakusaidia sana utakapoelewa jinsi Njia ya Katikati inavyofanya kazi na sheria za maisha haya na maisha baada ya haya. Hapo utakuwa shwari na utaelewa zaid maisha ni nini hasa. Lakini kwa kiwango chako cha sasa,unataka kuwa nini?''

''Nilitazama kutoka katika Golden Roof na nikamuona muendesha boti katika Happy River,na nikafikiri kwamba yale ni maisha huru,raha sana kupiga kasia kwenda na kurudi katika mto ambao kila mtu anaupenda,kukutana na watu wazuri,watu waliotoka India,watu wanaokwenda China,watu wanokwenda kuvuka milima na kurudi nyumbani baadaye na elimu ya ajabu na vitu vya ajabu.Lakini mimi-mimi ni mvulana tu nimekaa hapa naishi maisha ya nidhamu,sina uwezo wa kufanya ninachotaka,kila wakati inanibidi nifuate amri,kila wakati naambiwa kwamba maisha yangu yatakuwa magumu lakini kwamba nafanya kazi kwa lengo maalum,kwamba nitafanya kazi maalum.'' Nikanyamaza kwa muda na kufuta uso wangu na shati langu,halafu nikaendela,kwa nini inanibidi kila wakati kuvumila mambo haya magumu?''

Yule Mwalimu aliuweka mkono wake juu ya bega langu na kusema ,''Maisha ni kama hili darasa;mnakuja hapa,wengine sio kwa hiari yenu,wengine kwa furaha,lakini wote mnakuja hapa kujifunza mambo,na kila mmoja wenu lazima ajifunze kwa
kasi yake kwa sababu hakuna yoyote,mwalimu yoyote,ambaye anaweza kulazimisha maendeleo yako,kwa sababu akifanya hivyo itamaanisha kwamba hautakuwa na elimu iliyokamilika kuhusu somo fulani. Lazima uendelee kwa kasi yako,mbio au pole pole kufuatana na uwezo wako,kufuatana na hamu yako ya kutaka elimu. Maisha yote ni kama darasa;unakuja katika maisha haya kama unavyokuja katika darasa hili. Lakini ukiondoka darasa hili baada ya dakika chache itakuwa sawa na kufa katika maisha haya,kufa katika darasa.Labda kesho utakwenda katika darasa tofauti,ambayo ni karibu sawa na kuzaliwa tena,kuzaliwa katika mwili mpya,katika hali mpya,na masharti mapya. Haufahamu mwalimu atakufundisha nini,hufahamu kwa nini mwalimu atakufundisha,lakini katika miaka ijayo utakapoenda kwenye nchi kuvuka milima yetu utaona kwamba mambo uliyojifunza katika darasa hili na madarasa mengine yatakusaidia sana kwa njia ambazo sasa hivi huwezi kuzielewa.

''Hivyo ndivyo ambavyo kiongozi wangu ,Lama Mingyra Dondup ananiambia kila wakati,'' nilijibu ,''Lakini badosijui kwa nini niafiki kufanya jambo ambalo haliniletei furaha.''

Yule Mwalimu alitazama kuona kama wale watoto wengine walikuwa wanafanya nini,lakini wote walikuwa wamewania,walikuwa wanasikiliza kwa makini kwa sababu ilikuwa inaonekana kama wao wote walikuwa na matatizo kama yangu . Sisi wavulana wote tuliwekwa katika lamaseri si kwa hiari yetu,mimi kwa mfano niliingia nilipokuwa na umri wa miaka saba. Hawa wavulana walikuwa wanasikiliza sasa,wote tulikuwa kama watu ambao tunapita katika giza nene tunatumainia kupata nuru ya mwangaza kuongoza njia yetu.

Mwalimu wetu aliendelea:''Lazima muamue zipo njia ngapi ambazo zimefunguka mbele yenu. Wewe,Lobsang,unaweza kukaa hapa kuwa mtawa,au unaweza kuondoka na kuwa mwendesha mashua. Lakini huwezi kuwa vyote kwa wakati mmoja. Lazima uamue unataka kuwa nini. Kama unataka kuwa mwendesha mashua ,basi ondoka kutoka katika hii lamaseri,na usiifikrie tena hii lamaseri,fikiria tu jinsi ya kuendesha mashuwa. Lakini kama unataka kuwa mtawa-basi sahau kuwa mwendesha mashua,yaweke mawazo yako katika kujifunza kuwa mtawa mzuri. Na kila utakavyozidi kufikiria jinsi ya kuwa mtawa mzuri,ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako.''
Mmoja wa wavulana wengine akaingia kati,na kusema kwa msisimko,''Lakini,Mheshimiwa Mwalimu,mimi pia ilinibidi kuingia katika lamaseri si kwa hiari yangu. Nilitaka kwenda Nepal, kwa sababu nafikiri nitakuwa nina furaha zaidi nikienda Nepal.''

Yule Mwalimu wetu lama alionekana yuko makini,alionekana kama vile hili lilikuwa jambo muhimu sana na sio tu watoto tu ambao hawajui wanaongea juu ya nini. Akajibu kwa uzito mkubwa,''Lakini unawafahamu vizuri watu wa Nepal? Una uzoefu wowote ule nao zaid ya wale wachache ambao umekutana nao. Unayafahamu maisha ya watu wa chini wa Nepal?Kama sio,kama hujaenda mara nyingi kwenye nyumba zao,basi huwezi kusema kwamba unawapenda. Nasema kwamba kwamba kama unataka kubaki hapa Tibet,basi mawazo yako yote fikiria Tibet. Lakini kama unataka kwenda Nepal,basi ondoka Tibet sasa na uende Nepal na usiifikirie zaidi Tibet,kwa sababu kama ukiyagawanya mawazo yako unagawanya nguvu zako. Tunaweza kuwa na mkondo mzuri wa mawazo,au nguvu,au tunaweza kuwa na maji ya mvua yaliyotawanyika ambayo yanaanguka katika sehemu kubwa lakini hayana nguvu.. Kila mmoja wenu lazima aamue anataka kufanya nini,na baada ya kuamua,basi kila mmoja wenu azingatie kwa makini na akili ambayo haijagawanyika kufanikisha anachotaka kuwa,kwa sababu ukiamua kwenda Nepal na nusu moja ya akili yako na nusu nyingine inataka kubaki Tibet,basi unakuwa katika hali ya kushindwa kuamua wakati wote,una wasiwasi wakati wote,na huwezi wakati wowote kupata amani ya akili au shwari. Hii ndio moja ya nguvu kubwa duniani,moja ya Sheria kubwa ambayo lazima uikumbuke. Mgawanye adui na utamtawala adui,kaa mwenyewe bila kugawanyika na utamshinda adui aliyegawanyika. Adui anaweza kuwa kutoamua[indecision],woga na kutokuwa na hakika[uncertainty].''

Wote tulitazamana ,na tukafikiria kwamba huyu Mwalimu alikuwa anatuelewa vizuri. Ilikuwa ni vizuri zaidi kuwa na mtu ambaye alikuwa mtu[a man who was a man],mtu ambaye tungeweza kuongea naye na ambaye angeweza kuongea na sisi,na sio tu kutuambia mambo. Tulimfikiria yule mwalimu wa Kihindi jinsi alivyokuwa na majigambo na dharau[superscilious]. Nikasema,''Mheshimiwa Mwalimu,nina swali:Kwa nini watu wengine ni wakatili sana na wengine wana moyo wa kuelewa na ni wapole?''
Yule Mwalimu alitabasamu na kusema,''Lobsang,saa zimekwenda sana usiku kuanza kujadili maswala mazito kama hayo,lakini nakuahidi kwamba tujadili mambo kama hayo,pia tutajadili matumizi mazuri na mabaya ya dini zote.Lakini nadhani tumefanya kazi muda mrefu wa kutosha kwa siku moja,kwa hiyo wote kila mmoja aendelee na shughuli zake.'' Alisimama,na wavulana wote walisimama pamoja naye. Lama aliona kwamba nilikuwa nina matatizo kwa hiyo aliinama,na kuweka mkono wake kunizunguka,na akanisaidia kuinuka kwa urahisi na kwa shwari kama vile alikuwa amezoea kufanya hivyo kila siku ya maisha yake.

'' Nendeni sasa watoto watoto,'' alisema,''ama sivyo mtakuwa mnajikwaa na kuanguka katika giza na hatutaki watu wengine wawe na matatizo ya muda ya kuumia miguu.

Sawasawa mzee!
 
Mwalimu alikuwa hafahamu kitu chochote kuhusu Buddhism. Inawezekana alitoa sadaka pale Buddhist Temple Dar es Salaam. Mimi nilikuwa sipo wakati huo,lakini nilisikia kwamba jambo kama hilo lilitokea. Wakati huo nilikuwa Sri Lanka,nilikuwa naishi katika Buddsit Temple.
Mwalimu pia katika safari zake mara nyingi alikwenda kutembelea Buddhist Temples na Buddhist Monasteries. Yaani siyo safari ya kuotoka Tanzania kwenda kutembelea Buddhidt Temple,isipokuwa tu kwenda kufanya Temple Gazing,to pass time.
 
Ngoja niufufue huu uzi iliwengine wafaidike, ikiwezekana Invisible tusaidie kuupeleka jamii intellegent huu uzi maana sasa hivi utapata wachangiaji wengi..
 
Back
Top Bottom