Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,334
- 14,281
Aliyekuzidi amekuzidi tu..mimi kwetu mtwara wakina mama vibarazani umbea wababa wanacheza bao, maendeleo yatakuja kweli?
Bora yako wewe umejisemea ukweli.
Aliyekuzidi amekuzidi tu..mimi kwetu mtwara wakina mama vibarazani umbea wababa wanacheza bao, maendeleo yatakuja kweli?
Kuna uzi mmoja tumezungumzia sana hili na kueleza kama unavyosema.
Ndugu yetu Mkandara akasema shule hizo zinajengwa na serikali kwa upendeleo.
Nadhani unaweza kuzungumza naye sasa maana wewe ni shahidi umeyaona kwa macho
Uzi ukihitajika tutauweka hapa
Halafu kule shule za private ni chache sana! shule za serikali wanafundisha mwanafunzi vizuri zaidi ya private shangaaaa!
Ha ha haaa.... Ume mshambulia Zio vikali sana, ila cha kuongezea wakati sehemu nyingine za Tanzania zikilia na uhaba wa bidhaa za viwandani miaka ya 1980's watu wa Kilimanjaro walikuwa wanazipata kwa urahisi via magendo tokea Kenya, na kipindi hicho wengine wakikomaa kulima maindi na kuuza kilo Tsh. 55 kahawa kilo moja ilikuwa inauzwa Tsh 1000. Na Mungu akiwabariki wote wakavuna gunia 20 nadhani mkulima wa maindi atapata pesa kidogo saaana kuliko yule wa kahawa. Na cha ziada wengine wakifuata maji makilomita sisi tulikuwa tuna maji safi kwenye mifereji yetu iliyo chimbwa na babu zetu miaka ya 1890's.
hivi mkoa wa Kilimanjaro una wabunge wa ccm wangapi na upinzani wangapi? madiwani wa ccm wangapi na wa upinzani wangapi? hizi data nafikiri ndio zitatuonyesha kwamvba wanachagua ccm au upinzani.
Huko wameweza bila ccm, Wachaga walishafuta uchafu wa ccm, ndio maana unaona mambo yanakwenda
isingekuwa wizi hao jamaa wangekuwa kama sie wengine tu.
Wewe wala hujafika Moshi vijijin !maisha ni ya kawaida Kama sehemu nyingine za Tanzania sema wewe hujafika hilo eneo umeahadidhiwa na wachagga
aisee nilikuwa sijasikia hii.. Hii ni habari njema zaidi
Kama hujui Historia ya wachagga kaa kimya mkuu..
Vijiji vya Uchaggani vilijengwa na Serikali ya Uchagga ikishirikiana na KNCU.. Ulikuwa ukiuza kahama kwa chama kuna percent inakatwa inapelekwa kwenye kuimarisha miundombinu, kujenga shule, zahanati, kusomesha wanafunzi na huduma zingine za kijamii. Badala ya Serikali kuona hivyo wakafanya juu chini kuiua KNCU na hizo kazi zake zote wanazofanya..
Baada ya KNCU kukosa nguvu, ndiyo wananchi wakaanza kuchangishana wenyewe na kuendeleza yale yaliyokuwa yanafanywa na serikali waliyokuwa wanaiamini na si serikali ya TANU+CCM.
Mbowe+CDM+Ukawa kwa ujumla wanakataa wananchi ambao wanaishi maisha magumu kuchangishwa michango ovyo angali madini yanamalizwa, gesi inaelekea kuuzwa, bado kodi wanalipa, na deni la taifa kuongezeka kila kukicha. hayo yote bado mnataka muwabane wananchi wa hali ya chini?? Watu wanaiba mabilioni, wengine wanasema million 10 ni pesa ya mboga bado mnataka mchangishe watu??
Haya pitia hiyo attachment uone harakati zilianza lini..
View attachment 275644
Ni Mara yangu ya kwanza kuja Moshi Vijijini,nipo kikazi huku nikiwa mtumishi wa Serikali nimeshazunguka vijiji vinne sasa mandhari na hali ya hewa ni nzuri sana na wenyeji ni wakarimu pia.
Naona kila Kijiji kuna shule ya sekondari nzuri tu kama sio moja ni mbili au tatu kabisa wenyeji wananiambia ni kila Kata na imejengwa kwa nguvu za wananchi na baadhi kwa kushirikiana na mashirika ya dini.
Hii nimeipenda sana kumbe ndio maana kila Sector Serikalini hukosi Mchaga hata mmoja kweli inavutia na nimejifunza kitu kutoka kwenye vinywa vya watu.
Tembea uone tembea ujifunze
Ila tatizo naona kama huu mji unakuwa bila mipangilio kuna habari nilizisikia ila sikiamini chanzo chake kwamba kuna mtaalamu wa kizungu aliwahi kusema mji wa moshi ukijengwa kwa ustadi na mipangilio mizuri unaweza kuwa mji mzuri kuliko yote Afrika Mashariki kama sio Afrika
Hlf wakuu siku hizi mbona namba 1 ya usafi tumepotea?