Nipeni takwimu, rekodi hii ya Yanga SC ndani ya miezi takriban 6, imewahi kufikiwa na timu yeyote duniani?

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,318
1,936
Timu ya Dar es salaam Young Africans Sports Club, au Yanga sc aka Wakimataifa ama wananchi kama wanavyotambulika kwa sasa. Ktk msimu huu wa 2023/2024 wamekuwa ktk ubora usiopimika wala kumithirika.

Yanga hii ya Gamond imekuwa timu tishio kiasi cha kuogopwa uwanjani na timu pinzani kila zinapotaka kukutana ikiwemo Simba sc.

Imefikia wakati timu pinzani zinachopambania uwanjani ni kutofungwa goli 5 🖐 kama ilivyokuwa kwa Simba sc.
Ama hakika! Yanga ni tishio....!!!

Kutokana na kiambatishi hapo chini kinachoonesha timu ambazo mpaka sasa zimekula 🖐 Mkono kutoka kwa Yanga sc ikiwemo Simba sc, hebu nipeni takwimu kama kuna timu yeyote Duniani iliwahi kufikia record hii ya Yanga sc ndani ya kipindi cha kati ya Miezi 6 hadi 8 ya kuzifunga timu pinzani goli 5🖐 timu nyingi kiasi hicho kinachoonekana pichani...!!!

NB;YANGA WAKABIDHIWE KABISA KOMBE LAO MSIMU HUU,HII NI KUONDOA USUMBUFU.
 

Attachments

  • Screenshot_20240312-091715_Facebook.jpg
    Screenshot_20240312-091715_Facebook.jpg
    281.6 KB · Views: 5
Tano tano zimetuponza...
Ndo wakaamua kutupanga na Mamelod!!?
 
Back
Top Bottom