Nini tofauti ya neno Albino na Zeruzeru?

Salaam

Nimesikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa na Clouds radio leo katika kuadhimisha siku ya ufahamu kuhusu ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi " albinism awareness day".

Pamoja na kujifunza vitu vingi kuwahusu nimevutiwa na wito alioutoa mgeni wa kipindi kwa Mh. Rais Magufuli kwamba aharakishe kusaini adhabu za kunyongwa hadi kufa wale waliopatikana na hatia ya kuwauwa hawa ndugu zetu kwa imani za kishirikina.

Binafsi naunga mkono jitihada za kupinga kwa nguvu zote mauaji yao(Nasikia wauaji wameshaingia Malawi na kuna mauaji yametokea huko).

Pamoja na yote nimepata shida kidogo baada ya mgeni wa kipindi kusema Zeruzeru sio jina zuri kuwaita wenzetu hao ila akapendekeza tuwaite Albino sasa najiuliza nini tofauti ya majina hayo?

Hebu wajuzi wa lugha mnidadavulie!
Tofauti ipo katika urasmi yaani tunaweza kusema neno Albino linatumika hata katika shughuli za kiserikali,katika hotuba mfano lakini neno Zeruzeru linatumika tu mtaani katika mazungumzo ya watu wa kawaida.
 
Salaam

Nimesikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa na Clouds radio leo katika kuadhimisha siku ya ufahamu kuhusu ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi " albinism awareness day".

Pamoja na kujifunza vitu vingi kuwahusu nimevutiwa na wito alioutoa mgeni wa kipindi kwa Mh. Rais Magufuli kwamba aharakishe kusaini adhabu za kunyongwa hadi kufa wale waliopatikana na hatia ya kuwauwa hawa ndugu zetu kwa imani za kishirikina.

Binafsi naunga mkono jitihada za kupinga kwa nguvu zote mauaji yao(Nasikia wauaji wameshaingia Malawi na kuna mauaji yametokea huko).

Pamoja na yote nimepata shida kidogo baada ya mgeni wa kipindi kusema Zeruzeru sio jina zuri kuwaita wenzetu hao ila akapendekeza tuwaite Albino sasa najiuliza nini tofauti ya majina hayo?

Hebu wajuzi wa lugha mnidadavulie!

Zeruzeru na albino ndiyo majina sahihi yaliyo katika lugha mbili tofauti; Kiswahili na Kingereza. Lakini 'zeruzeru' lina ukakasi kama ilivyo "kiwete', "kipofu" nk. katika kulitamka hadharani.

Kwa sababu hiyo, na kwa kutambua ubinaadamu wa watu wenye ulemavu huo, watu wamebuni majina mbadala ya heshma ya watu wenye ulemavu huo, ikiwemo kuwaita " watu wenye ulemavu wa ngozi, na wengine wameingiza king'enge katika Kiswahili kwa kuwaita ' watu wenye albinism' kana kwamba walipokwenda Baraza la Kiswahili Tanzania - BAKITA, walishindwa kutajiwa msamiati mbadala unaozingatia utu, ubinaadamu, na utamaduni wetu.

BASATA wana wajibu wa kutusaidia katika hilo, maana huwa najisikia soni na ukakasi ninaposikia wakiitwa ' Watu wenye albinism'. Kama ni kukopa msamiati ! hapo ni kulipa matanga moja kwa moja!!
 
Katika ufuatiliaji wangu wa muundo wa maneno hatujawahi kurasmisha utohoshaji wa neno Albino katika misamiati ya kiswahili.

Pili dhana ya neno zeruzeru kuwa ni la kiudhalilishaji sifahamu msingi wake. Ikiwa neno la kiingeleza lenye maana ile ile limegeuzwa tafsida ya neno Zeluzelu huu ni utumwa mambo leo. Unadharau chako unatukuza cha mgeni mtawala?!!
="el_magnefico, post: 18754221, member: 337518"]Tofauti ipo katika urasmi yaani tunaweza kusema neno Albino linatumika hata katika shughuli za kiserikali,katika hotuba mfano lakini neno Zeruzeru linatumika tu mtaani katika mazungumzo ya watu wa kawaida.
 
Back
Top Bottom