Nini tofauti ya neno Albino na Zeruzeru?

akazuba

JF-Expert Member
May 16, 2014
533
484
Salaam

Nimesikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa na Clouds radio leo katika kuadhimisha siku ya ufahamu kuhusu ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi " albinism awareness day".

Pamoja na kujifunza vitu vingi kuwahusu nimevutiwa na wito alioutoa mgeni wa kipindi kwa Mh. Rais Magufuli kwamba aharakishe kusaini adhabu za kunyongwa hadi kufa wale waliopatikana na hatia ya kuwauwa hawa ndugu zetu kwa imani za kishirikina.

Binafsi naunga mkono jitihada za kupinga kwa nguvu zote mauaji yao(Nasikia wauaji wameshaingia Malawi na kuna mauaji yametokea huko).

Pamoja na yote nimepata shida kidogo baada ya mgeni wa kipindi kusema Zeruzeru sio jina zuri kuwaita wenzetu hao ila akapendekeza tuwaite Albino sasa najiuliza nini tofauti ya majina hayo?

Hebu wajuzi wa lugha mnidadavulie!
 
Albinism ni failure ya ngozi kutengeneza melanin ambayo inahusika na rangi/layer ya ngozi, kumwita mwenye tatizo hili zeru zeru kuna ukakasi na sawa na unyanyapaa...kama ambavyo si haki wala utu kumwita mtu mwenye mtindio wa ubongo taahira vivyo hivyo kumwita mtu mwenye tatizo la ulemavu wa ngozi zeru zeru!
 
Kama nakuelewa lakini am getting confused unaelezea maana ya albinism na ukaacha maana ya zeru zeru.... jina sahihi kwa kiswahili la albino ni lipi?
 
Zeruzeru linaumiza masikio; "watu wenye ulemavu wa ngozi" liko general mno maana si kwamba ulemavu wrote WA ngozi ni ualbino. Wataalamu wa Kiswahili watupatie jina sahihi. Lakini kuna katabia Siku hizi ka wait kuongeza neno "wenzetu" wanapotaja maneno "wenye ulemavu wa ngozi"!! Siku za usoni hili neno litakuwa na element ya unyanyapaa. Kwa mini linatumika kwao tu?
 
Albinism ni failure ya ngozi kutengeneza melanin ambayo inahusika na rangi/layer ya ngozi, kumwita mwenye tatizo hili zeru zeru kuna ukakasi na sawa na unyanyapaa...kama ambavyo si haki wala utu kumwita mtu mwenye mtindio wa ubongo taahira vivyo hivyo kumwita mtu mwenye tatizo la ulemavu wa ngozi zeru zeru!
Au mlemavu wa miguu-kiwete
 
Kama nakuelewa lakini am getting confused unaelezea maana ya albinism na ukaacha maana ya zeru zeru.... jina sahihi kwa kiswahili la albino ni lipi?
Ni zeruzeru.. Lakini inadaiwa kuwa huwa halipendezi... Albino (hilohilo la kiingereza) ndo linawapendeza
 
Kuna watu wanakuwa na ugonjwa unaofanya midomo kuwa na rangi ya pink, mikono, miguu lakini the rest of their body ni normal sasa hao kwa lugha za wengine wanasema akokibwa eirongo. Je hawa watu wana tofauti gani na hawa zeru zeru? Nawaita zeru zeru sababu si tusi wala kejeri ni jina la kiswahili. Albino ni kiingereza kilichotoholewa toka kilatini. Naomba samahani sababu kwanini basi kati ya hawa ndugu zetu wasitafute jina la kibantu kujiita kuliko kutulazimisha kuwaita kizungu. Viziwi, fipofu, viwete, vikojozi, vichaa, ila shida inakuja kwanini haya majina yaanze na V kwanini si kama walevi, wachawi, wambea??? Naomba michango yenu.
 
Kaka sioni ubaya, maana jinsi unavyotumia lugha hakuna haja ya kukulazimisha kutumia kizungu, sivyo?
 
Salaam

Nimesikiliza kipindi kilichokuwa kinarushwa na Clouds radio leo katika kuadhimisha siku ya ufahamu kuhusu ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi " albinism awareness day".

Pamoja na kujifunza vitu vingi kuwahusu nimevutiwa na wito alioutoa mgeni wa kipindi kwa Mh. Rais Magufuli kwamba aharakishe kusaini adhabu za kunyongwa hadi kufa wale waliopatikana na hatia ya kuwauwa hawa ndugu zetu kwa imani za kishirikina.

Binafsi naunga mkono jitihada za kupinga kwa nguvu zote mauaji yao(Nasikia wauaji wameshaingia Malawi na kuna mauaji yametokea huko).

Pamoja na yote nimepata shida kidogo baada ya mgeni wa kipindi kusema Zeruzeru sio jina zuri kuwaita wenzetu hao ila akapendekeza tuwaite Albino sasa najiuliza nini tofauti ya majina hayo?

Hebu wajuzi wa lugha mnidadavulie!

Albino ni mzungu zeruzeru na zeruzeru ni albino mwafrika.
 
Labda nikujibu hilo la matumizi ya V kwanza nikukumbushe tu lugha ya kiswahili ina Ngeli tisa moja wapo ni KI-VI hii hutumika kwenye vitu visivyo na uhai mfano Kijiko (umoja) na Vijiko (wingi)... neno kiziwi ni hali aliyonayo mtu aliyepoteza uwezo wa kusikia watu hao wakiwa wengi utatumia neno Viziwi ili kukamilisha upatisho wa kisarufi. Mfano.. N+U+T Juma ni kiziwi. Juma na Asha ni Viziwi
Kuna watu wanakuwa na ugonjwa unaofanya midomo kuwa na rangi ya pink, mikono, miguu lakini the rest of their body ni normal sasa hao kwa lugha za wengine wanasema akokibwa eirongo. Je hawa watu wana tofauti gani na hawa zeru zeru? Nawaita zeru zeru sababu si tusi wala kejeri ni jina la kiswahili. Albino ni kiingereza kilichotoholewa toka kilatini. Naomba samahani sababu kwanini basi kati ya hawa ndugu zetu wasitafute jina la kibantu kujiita kuliko kutulazimisha kuwaita kizungu. Viziwi, fipofu, viwete, vikojozi, vichaa, ila shida inakuja kwanini haya majina yaanze na V kwanini si kama walevi, wachawi, wambea??? Naomba michango yenu.
 
Albinism ni failure ya ngozi kutengeneza melanin ambayo inahusika na rangi/layer ya ngozi, kumwita mwenye tatizo hili zeru zeru kuna ukakasi na sawa na unyanyapaa...kama ambavyo si haki wala utu kumwita mtu mwenye mtindio wa ubongo taahira vivyo hivyo kumwita mtu mwenye tatizo la ulemavu wa ngozi zeru zeru!

Mkuu kwa jinsi nilivyo wasikia wenyewe hawataki hata kuitwa walemavu wa ngozi .

Ila zeruzeru ni kiswahili cha neno albino wakisema tusilitumiea kwa maana nyengine wanapunguza maneno ya kiswahili katika lugha yetu.

Ukakasi wa neno usisababishe tushindwe kuyatumia maneno yetu ya kisawahili basi wangefanya mbadala wa kuleta jina lengine kwa lugha yetu kuliko kutulazimisha wote tutumie lugha ya kiingereza wakati lugha yetu ina maneno mengi tu.

Tatizo hawataki kujikubali kuwa wao ni walemavu ndio maana wanapinga hata lugha inayotumika kuwaita kwa ulemavu wao.
 
Mkuu hivi huna habari kwamba hata tusi ukitukanwa kwa lugha ya malkia linapungua makali? Mfano kijijini kwetu ukiitwa Mbwiga ni lazima mtaa uchafuke kwa ngumi,ila ukiiulizwa 'are you nut?' unacheeeeka!
 
Ni aibu taifa lenye miaka 55 ya uhuru bado tu tuna mawazo ya kubagua watu wa rangi ya ngozi zao.
 
Back
Top Bottom