Jamani hebu tujadili na hili,katika rasimu ya katiba mpya inayopendekeza muundo wa serikali tatu kwa kuwa na "SHIRIKISHO" la bara na visiwani kwa kumaanisha kwamba Muungano wetu utaendelea kuwepo mimi naona si sahihi kwani kama tunahitaji muungano basi tuwe na serikali moja tu.Mantiki yangu ni kwamba,maneno yaliyotumika ambayo ni "JAMHURI YA MUUNGANO" kwa sasa na "SHIRIKISHO" kwa hii rasimu ni maneno yenye maana tofauti kwani MUUNGANO haina maana sawa na SHIRIKISHO hivyo basi ni maoni yangu kwamba rasimu hii ya katiba yenye muundo wa serikali 3 pamoja na watu wote wanaopendekeza hilo shirikisho naona wanatupotosha kwani endapo tutapata katiba itakayotamka "SHIRIKISHO" wao wanasiasa watakuja na tafsiri ya kisheria ambayo itaonesha maana sahihi ya SHIRIKISHO ambayo haipo sawa na maana halisi ya neno MUUNGANO.
"TUNAWEZA KUSHIRIKIANA KUPITIA SHIRIKISHO LA NCHI MBILI LAKINI TUSIUNGANE"
HIVYO BASI KAMA TUNAUHITAJI MUUNGANO TUWE NA SERIKALI MOJA YA MUUNGANO TU.AHSANTENI wazalendo watanzania wenzangu.
"TUNAWEZA KUSHIRIKIANA KUPITIA SHIRIKISHO LA NCHI MBILI LAKINI TUSIUNGANE"
HIVYO BASI KAMA TUNAUHITAJI MUUNGANO TUWE NA SERIKALI MOJA YA MUUNGANO TU.AHSANTENI wazalendo watanzania wenzangu.