Nini tatizo with Bunge, Wabunge na serikali..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Baada ya kusikia wabunge wanalalamikia sheria mbaya ndipo nimejua kuwa kuna matatizo Bungeni! Kiasi cha Spika kuwakumbusha wabunge kuwa wao ndio watunga sheria wenyewe!

- Kukataliwa sheria ya usalama wa taifa
- Kupitishwa kwa sheria ya "Mbwembwe" na kuirudisha tena
- Sheria Madini ambayo inalalamikiwa

Na vituko vingine vya huko Bungeni miaka hii ya karibuni. Nina wasiwasi yawezekana tatizo letu la kiuongozi ni kubwa kweli kuliko tunavyofikiria ndio maana wabunge wachache wanaoonekana kufuatilia vitu kwa ukaribu wanaonekana ni mishumaa kati ya giza.


On the other hand.. yawezekana tatizo si la wabunge bali ni la serikali maana huko nyuma walikuwa wanapush sheria mbalimbali wakijua zitapiga kiulaini tu lakini sasa hivi mambo siyo hivyo tena kwa sababu wabunge wanasoma na hata wale wasiosoma sana wanafuatilia usomaji wa watu wengine na kupata mwanga wa nini cha kusimamia?

Kama tatizo ni serikali itakuwaje tena wakati serikali ndio ya chama hicho hicho chenye wabunge wengi?
 
M.M,

Ngumu kuja na conclusion lakini tatizo ni "uongozi wetu". Huenda kama wangekuwa wanaujua uongozi hata hao wanaosoma wasingependa kuwa viongozi au mshumaa kama walivyo. Ukiona majibu mepesi kwenye hoja nzito ujue kuna tatizo, ukiona unaharibu hapa unapelekwa pale jua kuna tatizo na ukiona mtu unapewa uongozi kwa kujuana ujue hapo hakuna pefrtomance.

Utajiuliza haya? Mi nshajichokea ila sijakata tamaa.
 
Mimi nadhani uko sahihi tatizo liko kwa owte Bung na Serikali.Bunge letu limajaa vihiyo na hata wasomi waliopo hawasomi between lines..wanapita juu tu.Serikali nayo inafanya makusudi kuleta vitu vibovu Bungeni kwa maslahi ya wachache kwa kuwa wanajua wabunge wengi hawasomi..Ni vema ile hoja ya kuabdili katiba kuhusu sifa za kuwa mbunge kwa kipengele cha usomi kikazingatiwa katika siku za usoni.
 
Baada ya kusikia wabunge wanalalamikia sheria mbaya ndipo nimejua kuwa kuna matatizo Bungeni! Kiasi cha Spika kuwakumbusha wabunge kuwa wao ndio watunga sheria wenyewe!

- Kukataliwa sheria ya usalama wa taifa
- Kupitishwa kwa sheria ya "Mbwembwe" na kuirudisha tena
- Sheria Madini ambayo inalalamikiwa

Na vituko vingine vya huko Bungeni miaka hii ya karibuni. Nina wasiwasi yawezekana tatizo letu la kiuongozi ni kubwa kweli kuliko tunavyofikiria ndio maana wabunge wachache wanaoonekana kufuatilia vitu kwa ukaribu wanaonekana ni mishumaa kati ya giza.


On the other hand.. yawezekana tatizo si la wabunge bali ni la serikali maana huko nyuma walikuwa wanapush sheria mbalimbali wakijua zitapiga kiulaini tu lakini sasa hivi mambo siyo hivyo tena kwa sababu wabunge wanasoma na hata wale wasiosoma sana wanafuatilia usomaji wa watu wengine na kupata mwanga wa nini cha kusimamia?

Kama tatizo ni serikali itakuwaje tena wakati serikali ndio ya chama hicho hicho chenye wabunge wengi?

Naanza na kukupongeza kwa kuliona hilo me zamani pia nilikuwa nime kali tu kuitizama IKULU na kupenda kutaka kujua na huko nako kuana matatizo gani pia.

Sasa basi minadhani kuwa Bungeni pia wana mapungufu yao te sio madogo ni makubwa ni kama ulivyosema kuna viongozi wachache ambao ni mishumaa kwenye giza uchache wao ni unakuwa vigumu sana wao kulikamata bunge ipasavyo ili hizo kanuni na sheria zipitishazo zika fanyiwe kazi vyema na serikali ni kweli wanakosa nguvu hapo,

huko bungeni kunatakiwa kuwe na watu makini wachukuapo miswaada ya sheri iliyopitishwa na wabunge kwenda IKULU kusaini. iweje tu huko njiani tiali mtu mmoja anamamlaka ya kuongeza kipengere? huo ni uzembe usio kubalika hata kidogo huyo mtu mie namwona kama anahujumu nchi na kuipeleka shimoni hatufai hata kidogo.

Kwa upande wa serikali nadhani inatupasa tuelewe kuwa nini maana ya uongozi kwakweli tumepotea sana jamani imefika hatua ati twajifanya tumesahau uongozi sio kiburudisho jamani nikuwajibika kwa wananchi wako waliokuteuwa na ulitambue hilo ulipoenda kuwaomba kura, sasa wengi wetu wamefanya mtaji wao bure kabisa kwa viongozi wanofanya hivyo na hii ndio imekithili ndani CCM yetu viongozi wengi wamepoteza mwelekeo na amini nawambieni ni viongozi vijana wachache sana wanao penda maendeleo ya dhati na wenye uzalendo 70% ya vijana wanao taka uongozi ni uchu wa madaraka umewajaa mioyoni mwao na tamaaa na sio wako tu kwakutaka uongozi ni kwa kujineemesha hilo nimeliona vyema kwenye kamati nyingi na mikutano mingi ya UVCCM, sasa hawa ndio waje kugombea ubunge kweli na wawekwe kwenye serikali yetu ndi tutapotea kabisa mie nilitegemea vijana watakuwa na moto NAPE vile kumbe hakuna kabisa ni wachache ambao ni wazalendo na hawana nafasi ndani ya UVCCM na ukiibuka kuwa ndio chachu ya maendeleo utapingwa vibaya sana, Imefika wakati tuwaogope wapiga kura wetu tuwaheshimu jamani.

Hivyo basi hata serikalini pia kuna mapungufu tena makubwa sana maana huko ndiko utekerezaji watakiwa kufanyika kwa umakinifu, maadili ya uongozi yamepotea sana, Me sijui tumeingiliwa na kichaa gani kama kujiroga kweli tumejiroga, % kubwa ya wapiga kura ni vijana lakini ukitizama statistic yetu ni ndogo sana katika bunge hata nyanja mbali mbali hatupo kweli tutaliongoa taifa letu lini??
 
Tatizo ni both wabunge na srikali. Serikali inapeleka bungeni sheria ambazo hazina maslahi kwa wananchi bali kwa eidha serikali yenyewe, wabunge au pressure kutoka kwa wafadhili. Halafu kibaya zaidi waandishi wa sheria wanakuwa hawako makini sana na kama wako makini wanashindwa kuiadvise serikali kuwa imekosea.

Kuna sheria ukiangalia unaweza kucheka sana angalia hii ambayo NCCR waliizungumzia asubuhi ambayo inasema uchaguzi utakuwa kuziba vacancy hivyo ili uchaguzi ufanyike lazima kuwe na vacancy na raisi lazima ajiuzulu ili kuwe na vacancy kwa yoyote anayejua kiingereza argument yao ni valid. Hili ni tatizo la kuandika sheria walisahau practical side wakati wa kuweka defination ya election.

Sheria zingine zinakuja kwa pressure ya wafadhili, sheria ya watoto ya mwaka jana hakukuwa na haja ya kutungia sheria cha msingi ni kuwawezesha wazazi wawe na nyenzo za kuleawatototo wao. Kama kuku anaweza kumparura binadamu akisogelea kifaranga kwa nini binadamu asifanye zaidi ya anavyofanya kuku. Kutotunza watoto hakutokani na kutokuwa na mapenzi na watoto wetu bali kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kuwatunza.

Sheria ya Loans Board ni pressure nyingine mnatunga copy and paste lakini utekelezaji wake unakuwa na mashaka, kwa nini sheria inasema mtanzania anayesoma chuo cha elimu ya juu anastahili mkopo halafu mtu anakuja na kusema mkopo itatolewa kwa wanafunzi sayansi na education na kwenye fani nyingine ni wenye division 2 ndio wanaostahili, hii haipo kwenye sheria wala regulations. Sheria ipo shauri wafadhali walisema, tukifika utekelezaji tunakwama.

Sheria zingine kama BOT Act, Basic Duties and Rights enforcement Act zilitungwa ili kutetea maslahi ya serikali bila kuangalia mbeleni kutakuwa nini.

Fair competion Act ni mfano mwingine ambapo sheria ilitungwa 1994 ikaanza kazi 1996, mwaka 2001 vikaongezwa vifungu nane A to H kila kimoja kikiwa na subsection zaidi ya 3, actually ilikuwa sawa na kutunga sheria nyingine kabisa. Hii ni situation ya bunge kutokuwa makini kuona baadhi ya loopholes. Wabunge hawasomi kabisa miswada( bills). Kuwe na at least qualifications za juu kwenye ubunge ili waweze kudigest contents za bills.
 
Wabunge hawasomi kabisa miswada( bills). Kuwe na at least qualifications za juu kwenye ubunge ili waweze kudigest contents za bills.
Ngambo Ngali
Mbunge kama Kapteni Komba anayeingia bungeni kwa sababu ya kuimba sana unategemea nini kutoka kwake na kwanza ana hata huo muda wa kusoma hizo bills?
 
Mimi nadhani uko sahihi tatizo liko kwa wote Bunge na Serikali.Bunge letu limajaa vihiyo na hata wasomi waliopo hawasomi between lines..wanapita juu tu.Serikali nayo inafanya makusudi kuleta vitu vibovu Bungeni kwa maslahi ya wachache kwa kuwa wanajua wabunge wengi hawasomi..Ni vema ile hoja ya kuabdili katiba kuhusu sifa za kuwa mbunge kwa kipengele cha usomi kikazingatiwa katika siku za usoni.

Hapa naunga na wewe 100%, kinachoangamiza nchi hii ni SIASA. Sasa hivi wabunge hawatutumikii wananchi wala nchi as well as Mawaziri wako on behalf of CCM, inawezekana kabisa na ninaamini malengo ya CCM yaliyoko kwenye makaratasi yana manufaa kwa nchi hii, ila tatizo liko kwa hao wanasiasa wetu hawana intergrity na kucover udhaifu huo wako willing hata kumtetea mwizi ili kulinda chama. Kijana Manara ndio naona wamemtoa kafara ana tuhuma mahakamani kimtindo wamemwambia ajiuzuru nyadhifa zake, sasa babu Chenge anashindwa nini kujiuzuru ili kuweka uwanja huru wa kumchunguza? hiyo miswada inatoka within kamati za bunge kabla ya kuwasilishwa,na wanatakiwa wapeleke hata kwa stake holders before kupeleka matumboz bungeni. Aghhhhhh ngoja niishie hapo. Naunga mkono hoja 100 kwa 100.
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi. Everybody, the government, chama and individual MPs, is oput to save his skin before the judgement day
 
Mi nazani ni Motives zinazotumika kutunga hizi sheria ndio tatizo, nimewahi kuhudhuria baadhi ya public hearing za baadhi ya sheria, kiukweli sio wabunge wanaotunga sheria lazima hii iwe wazi,wao wanapitisha sheri zilizotungwa na serikali, ndio maana unakuta wakati mwingine wanaweza kupinga kila kitu kwenye muswaada unapoletwa kwa sababu hawakushiriki kwenye kutunga ila wao wanatakiwa wapitie na wapitishe.....hata ukiangalia elimu za waheshimiwa wetu wengi si za kuqualify kutunga sheria.
kwahiyo mimi tatizo naona ni serikali na motives wanazokuwa nazo wakati wanaandaa muswaada wa sheria ukajadiliwe bungeni ili upitishwe, kama Mkulu anasuala anataka kufanya au chama chake na akiambia anabanwa na sheria au utekelezaji wake utakuwa mgumu mpaka kuwe na sheria itakayosimamia suala hilo au mpaka sheria fulani ibadilishwe then ndio watunga sheria wataalamu wa serikali wanaohusika na eneo hilo hupewa kazi hiyo ya kutunga sheria ili ikapitishwe na wabunge na kusainiwa na rais.

ndio maana hata kama wabunge wanaweza sana kupinga muswaada fulani lakini kama motive ya serikali lazima itimie muswaada ule utapita tu na kuwa sheria....
 
Back
Top Bottom