Nini tafsiri ya polisi kumficha vile polis mwenzao muuaji?

Mmmh!
Kwao huyo wanamuone kuwa ni Shujaa kwa kutimiza lengo walilopanga. Yawezekana ile ilikuwa geresha tu kuwapoza wadanganyika, huenda yeye hakuwepo.
 
Unajua wao wanazani hatumfahamu wakati picha zimejaa kila kona!
Na hii inaonesha kuwa hawa polisi they dont care on what happened!
Ni unyama wa hali ya juu muuaji kuonyesha drama za aina hii

Wasafi wote weshaondoka katika hiyo taasisi dhalimu
 
Lazima wamkinge coz huyu ndiyo Mungu wa Kamuhanda, Mwema, Nchimbi na Watu wa Ikulu up to J. K kwa sasa coz order ya kuuwa ilitoka juu sasa hawa watekelezaji inabidi wamkinge huyu aliyefanikisha zoezi lote.
Hilo nalo neno! hivi unadhani askari yule konstebo, amepata wapi ujasiri wa kuua kwa staili ile kama siyo maagizo ya wakubwa zake? sasa ijulikane, lazima hawa polisi kuna kamchezo fulani wanataka kukacheza, kama kale walikocheza kwa Zombe, upo uwezekano huyo wanayemleta hapo mahakamani siyo muuaji mwenyewe, ndiyo maana hawataki apigwe picha, ili at the end of the day, siku ya hukumu, jaji aseme namwachia huru huyu jamaa, kwa kuwa ushahidi unaonyesha siku ya tukio huyu mtu hakuwepo kabisa nchini, alikuwa Darfur! Naomba mkajipange upya, mumlete muuaji wa Mwangosi!!
 
Nadhani ni mpango mahsusi. Tafadhali mwenye picha yake halisi inayoonesha sura vizuri aiweke hapa ili iwe rahisi leo na kesho...you never know..
 
Ni mtu wao, lazima wamsitiri! Walimtuma kazi na ameikamilisha vizuri. Hiyo ni gheresha ya mashitaka tu

Unaweza kukuta hata huyo mtuhumiwa siye yule askari aliyeua. Askari aliyeua anawea kuwa yupo zake mahali anakula bata na badala yake wamemleta kibaka mmoja kutudanganyishia.
 
Alyepelekwa pale cye yeye mhuni flani tu alyejikatia tamaa na maisha
Hiyo muvi haina tofauti kabisa na ile ya Kova, na mkenya chizi, kuwa ndiye aliyemteka Dr Ulimboka, si mnakumbuka kwenye vyombo vya habari, hatukuwahi kuiona picha yake! si mnaona hiyo kesi ya mkenya wa Kova, namna ilivyokufa kimya kimya!!
 
Yule siyo mwenyewe tumeibiwa haijawahi tokea mbona mzee Mwamwindi miaka ile alimuua aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dt.KLERRUU lakini mpaka leo picha zake zote hata akiwepo mahakamani zipo huyu ana nini cha zaidi?
 
kwani madaktari si walimpa ulinzi ULIMBOKA wao!! sasa nao MAPOLISI wanampa ulizi mwenzao (MUUAJI MWENZAO)
 
kwa kufichwa huku!kesho tukisikia mtuhumiwa amefia selo!
ndio kusema kesi itakuwa imeisha au?
wanasheria nisaidieni, maana hili suala limekaa mkao wa kupotoshwa zaidi kuliko kuruhusu Haki itendeke!
RIP mwangosi
 
Ndiyo maana raia hawana imani na pliiisi, wakikamata mhalifu wanamalizana naye maana akipelekwa kituo cha pliiiisi kesho tu unamkuta mitaani. Huyo wa kwao watamficha kisha watamhamishia nchi jirani kuzima soo.Kuna mama fulani mke wa daktari kule Mbeya aliua houseboy akahukumiwa kifungo lakini baada ya muda mfupi alionekana mitaani akiwa huru. Tanzania mipango tu. Itakuwa huyo wa kwao, huyo atahamishwa tu. Haya kamhanda, Mwangosi kafa umepata nini. Dhambi hii itakuandama na laana itakwenda mpaka kwa wajukuu na vitukuu vyako. Damu ya mtu huwa haipotei bure.
 
Heshima mbele wakuu. Nimeshangazwa na drama ya mapolis wa iringa pale mahakamani. Polis mwenzao walikuwa wamemzingira huku wakizuia asipigwe picha na waandishi wa habari. Hakika action walizokuwa wakizfanya mahakamani huwa zinaonekana katika sinema tena za Adolf Hitler tu.Tumemwona mkapa akienda mahakamani,na akapigwa picha (tena akitabasamu) tunawaona kila siku kina Basil Mramba,Mgonja na yule nani sijui mzee wa 'alex stewart' wote wanapigwa picha. Nini tafsiri ya polis kufanya sinema yote ile pale mahakamani? Najiuliza...
Watanzania ndio WADANGANYIKA WENYEWE! ni nani anahakika huyo anayefichwa ndio muuaji mwenyewe? Polisi wanajua wa TZ ni watu wa kelele za dakika chache then kimya! Mnaridhishwa kwa kuwekewa kanyaboya baadasya siku 3 kukitokea story nyingine kwishney! Hawa ndio wa TZ , watu wa kushobokea story na ikitokea nyingine wanaacha!!
 
Tumewashitukia, aliyepelekwa mahakamani si yule aliyeua. Hivi siku ya hukumu watamfunika vivyo hivyo? Inafaa tukaweke pingamizi kwa mahakama kuwa aliyeua si huyu aliyekamatwa
 
Back
Top Bottom