Nini Maoni yako baada ya kuisikiliza Album mpya Kendrick Lamar?

Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
6,781
10,886
Albam iliosubiriwa kwa hamu ya Nguli wa Hip Hop Kendrick Lamar imetoka rasmi na kuzua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa Hip Hop dunia

Kwa ufuatiliaji wangu mdogo nimeona watu wengi sana ni kama wamekua disappointed na album hii..... yaani hawajakuta kile walichokua wanakitarajia vichwani mwao
Wengi wanaona Kdot kacheza chini ya viwango vyake

Binafsi Nimeipenda na kuielewa sana haswa kwenye upande wa maturity, lyrics na flow

Dunia inakwenda kasi sana tatizo kubwa ninalo liona hapa ni wasikilizaji wa kizazi cha sasa wanaangalia zaidi beat na lyrics ambazo ni rahisi ku digest

Katika Album hii Kendrick anaonyesha ukomavu na theme ya album kwa kiasi kikubwa kwa mara ya kwanza ime base zaidi na personal experience za maisha yake binafsi so ili kuielewa inabidi uangalie zaidi lyrics na delivery
Kama utataka beat kali kama za akina Drake basi hakika utakua miongoni mwa watakao ona Lamar kacheza chini ya kiwango

Naipa Album 9/10
Toa maoni na rate zako

Ili kuipakua album hii pitia hapa
Telegram J.cole & kendrick Lamar Updates™
 
Nilisema Mwanza tutapanda kwenye chati
Angalia sasa huyu Konki lamaa anavyowapeleka kina Mondi mputamputa.....
 
Album ni kali....

Amejitahidi sana ila kizazi cha sasa wengi hawaezi kumuelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom