Nini maana ya watu kufurika kwenye mechi kubwa za football hapa nchini?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,393
Je, ni uchumi kukua kiasi kwamba watu wanapesa za kula na za anasa na burudani?

Je, ni ugumu wa maisha watu wameamua kupoteza lengo katika burudani na michezo?

Je, ni kukua kwa kiwango cha ufuatiliaji wa mpira wa ndani kwa siku za karibuni?

Nimelinganisha maudhurio yetu yanaendana na ya nchi za waarabu ila kwa weusi wenzetu tuko mbali sana.
 
Michezo ni burudani, kufatilia michezo kwa ukubwa sio kwamba uchumi umekuwa... Huko vijijini tu kuna Timu za vijiji, ambazo wanakijiji wanakusanyika mpaka unashangaa.... MICHEZO ni burudani, na michezo uongeza furaha... Na michezo imekuwepo toka enzi na enzi, huku lengo kuu ikiwa ni kuburudisha, mataifa yaliyoendelea yana michezo mbalimbali... Huku Tanzania kwa sababu ya ufinyu wa miundombinu na bajeti ndogo, inapelekea mpira kuwa ndio mchezo pekee wenye wafuatiliaji wengi.... Na timu ikiwa inafanya vizuri hususani kimataifa basi uongeza wigi wa mashabiki na hamasa
 
Je ni uchumi kukua kiasi kwamba watu wanapesa za kula na za anasa na burudani?

Je ni ugumu wa maisha watu wameamua kupoteza lengo katika burudani na michezo?

Je ni kukua kwa kiwango cha ufuatiliaji wa mpira wa ndani kwa siku za karibuni?

Nimelinganisha maudhurio yetu yanaendana na ya nchi za waarabu ila kwa weusi wenzetu tuko mbali sana.
Ni umoja wa kitaifa🙏
 
●Uwekezaji mzuri umechangia timu zetu zimeanza kufanya vizuri kimataifa hii imeanza kuwavutia mashabiki. Mfano Mo na GSM wamefanya kazi nzuri kwenye uwekezaji
●Wahamisishaji na wasemaji wa klabu wamekuwa wakifanya kazi nzuri kuhamasisha mashabiki
●Ubora wa wachezaji wanaosajiliwa hasa wa kigeni imekuwa kivutio kwa mashabiki
●Kwa upande wa TV azam apewe maua yake
●Media zimetoa airtime sana habari za michezo na matukio ya kimichezo. kwa sasa vipindi vya michezo ndiyo vyenye airtime kubwa kuliko vingine vyote, hii imechangia uhamasishaji
●Bila kusahau social media

Good news wanawake wameanza kuwa mashabiki ndakindaki wa Simba na Yanga
 
Uwekezaji mzuri umechangia;
●Timu zetu zimeanza kufanya vizuri hii imeanza kuwavutia mashabiki. Mfano Mo na GSM wamefanya kazi nzuri kwenye uwekezaji
●Wahamisishaji na wasemaji wa klabu wamekuwa wakifanya kazi nzuri kuhamasisha mashabiki
●Ubora wa wachezaji wanaosajiliwa hasa wa kigeni imekuwa kivutio kwa mashabiki
●Kwa upande wa TV azam apewe maua yake
●Media zimetoa airtime sana habari za michezo na matukio ya kimichezo. kwa sasa vipindi vya michezo ndiyo vyenye airtime kubwa kuliko vingine vyote, hii imechangia uhamasishaji

Good news wanawake wameanza kuwa mashabiki ndakindaki wa Simba na Yanga
Hilo la wanawake naona linanguvu sana japo point zako zote safii
 
●Uwekezaji mzuri umechangia timu zetu zimeanza kufanya vizuri hii imeanza kuwavutia mashabiki. Mfano Mo na GSM wamefanya kazi nzuri kwenye uwekezaji
●Wahamisishaji na wasemaji wa klabu wamekuwa wakifanya kazi nzuri kuhamasisha mashabiki
●Ubora wa wachezaji wanaosajiliwa hasa wa kigeni imekuwa kivutio kwa mashabiki
●Kwa upande wa TV azam apewe maua yake
●Media zimetoa airtime sana habari za michezo na matukio ya kimichezo. kwa sasa vipindi vya michezo ndiyo vyenye airtime kubwa kuliko vingine vyote, hii imechangia uhamasishaji

Good news wanawake wameanza kuwa mashabiki ndakindaki wa Simba na Yanga
Huku umaskini ukiendelea kudidimiza maelfu ya watanzania.
 
Back
Top Bottom