Nini maana ya nyara za serikali 'government trophy', nyara za serikali ni zipi...?????

Avatar

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
11,127
11,908
Pengine unaweza ukawa unamijusi, panya au ndege fulani nyumbani kwako kumbe masikini unaishi na nyara za serikali bila kujua.

Nyara "trophy", si neno geni masikioni mwako.. ni wazi kuwa umekua ukilisikia mara kwa mara ama mara kadhaa kwenye magazeti au taarifa za habari kuwa polisi wamemkamata mtu akiwa na nyara za serikali. Lakini pia inawezekana ukawa umelisikia ndio lakini hadi leo hii hujawahi kujua wala kujiuliza lina maana gani hasa.

"Nyara" za serikali ni sehemu ya mwili au zao la WANYAMAPORI, hivyo ni kosa kisheria kumiliki ama kubeba nyara za serikali bila kuwa na kibali maalumu kutoka Idara ya Wanyamapori Tanzania.

maana ya nyara kama zilivyo ainishwa kisheria.....

"NYARA" au TROPHY" inamanisha pembe ya ndovu, pembe za faru, meno ya kiboko, pembe za wanyama na ngozi ya mnyama yoyote aliopo katika game.

"NYARA ZA KUUNDWA" "MANUFACTURED TROPHY" inamaana ya kitu chochote kilichoundwa ama kutengenezwa kutokana na nyara au kutoka kwenye jino, pembe ya ndovu, pembe ya kawaida, mfupa, nywele, nyoya, yai, kucha, ukwato au sehemu yoyote ya mnyama yoyote.

zifuatazo zitabaki kuwa nyara za serikali;
1. Mnyama yoyote ambaye itakuwa ameuliwa katika harakati za kulinda/kuokoa maisha au mali.
2. Mnyama ambaye atakutwa amekufa.
3. Mnyama yoyote atakaye kuwa amelkamatwa ama kuuliwa bila leseni.
 
Mkuu umesahau na wanafunzi wa kike wa sec kushuka chini nao ni nyara za serikali maana adhabu ya kutembea na mwanafunzi huyo kimapenzi ni sawa au inazidi hata kukutwa na ngozi ya Twiga
 
Hii ni maana umeitoa wapi,? naomba unipe reference tafadhali
Nyara- ni kitu mfano wa Mali ya uma (serikali) chenye umuhimu kuzunguka wana-jamii husika.
 
Hahaha ardhi ni ni mali ya serikali na vilivyomo ndani yake, natural resources zote lazima ziwe chini ya uangalizi... Bange sio natural resource.

Ndio maana unaweza nunua kiwanja na bado ukawa unakilipia kwa mwaka
Wakikuta Madini kwenye Shamba lako ni Nyara za serikali ila Wakikuta BANGI ni ya Kwako,hapo ndio utajua nini maana ya NYARA za Serikali na NYARA za Kwako.
 
Hahahaha sawa sawa mkuu...

Kweli hata hii ni nyara, ila bangi sio nyara wawe makini...
Mkuu umesahau na wanafunzi wa kike wa sec kushuka chini nao ni nyara za serikali maana adhabu ya kutembea na mwanafunzi huyo kimapenzi ni sawa au inazidi hata kukutwa na ngozi ya Twiga
 
Back
Top Bottom