Wana JF,
Magezeti yameandika habari kuhusu Waziri wetu wa Uhusiano wa kimataifa kuwageuka wenzake wa Rwanda, Congo, Burundi, Kenya, Ethiopia Uganda na Sudan Kusini kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile.
Nchi hizi za Afrika ambazo ni maskini sana ziliazimia kuongeza matumizi ya maji ya mto huo ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme na kwa ajili ya umwagiliaji. Mfumo uliokuwa umewekwa na Waingerza miaka ya ishirini ulikuwa hauna maslahi kabisa kwa nchi ambazo mto huu umepitia.
Kwa kifupi ni sawa na kwamba mto ule unamilikiwa na Egypt. Kuna wakati hata waliwahi kutamka eti nchi itakayogusa maji yale itapigana nayo vita.
Tanzania ilikuwa kati ya nchi zilizokuwa mstari wa mbele kudai mfumo huo wa kibepari na kibaguzi ubadilishwe kwa maslahi ya mataifa yote ambamo mto huu umepitia. Cha kushangaza Mh. Membe (au tuseme Tanzania) hivi karibuni imezigeuka nchi zote zenye kudai matumizi zaidi ya mto huo eti kwamba anajali zaidi maslahi ya wa-Egypt.
Nashindwa kutafakari maana ya uamuzi huo. Najiuliza hivi huu ndiyo mwendo wa kuelekea uchaguzi mwakani?? Maana inasemekana aliliongelea hata Bungeni.
Ukitaka kuona mojawapo ya maandiko kuhusu jambo hilo soma The EastAfrican la June 22-27 2014.
===========================
Chanzo: Raia mwema
Mada zaidi kuhusu Mipaka ya Ziwa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...umie-usomi-wetu-tusimame-kwenye-ukweli-2.html

HATUA ya Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kutetea taifa la Misri katika mgogoro wa matumizi ya maji ya Mto Nile imewakera mawaziri wenzake kwa vile matamshi yake yanapingana na msimamo wa Baraza la Mawaziri, Raia Mwema limeambiwa.
Hivi karibuni, Membe alikaririwa katika vyombo vya habari akieleza kwamba Taifa la Misri linapaswa kutazamwa katika suala la matumizi ya maji ya Mto Nile kwa vile bila maji hayo, nchi hiyo itaumia zaidi.
Hata hivyo, msimamo huo wa Membe umepokewa kwa mshangao na mawaziri wenzake waliozungumza na gazeti hili na kusema kwamba anachokifanya ni kupingana na Baraza zima la Mawaziri.
"Sikiliza. Membe amekosea. Mambo yote ya maji, na hususan, masuala ya Mto Nile yako chini ya Waziri wa Maji. Hili nakwambia kwa uhakika kabisa. Membe si msemaji wa serikali kwenye mambo ya maji kama anavyotaka kuaminisha umma.
"Kimsingi, mambo yote anayofanya Waziri wa Maji kuhusu Mto Nile yamejadiliwa katika Baraza la Mawaziri na yameafikiwa. Hakuna tena waziri mmoja anayeweza kutengua," alisema mmoja wa mawaziri aliyezungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki ambaye kwa sababu za wazi kabisa tunahifadhi jina lake.
Membe na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Jumanne Maghembe, wameingia katika hali ya sintofahamu kuhusu suala hilo la Mto Nile, katika namna ambayo imewashangaza wafuatiliaji wa siasa za Tanzania katika eneo hilo.
Maghembe alisema Tanzania inakaribia kuridhia Mkataba wa Matumizi Endelevu ya Maji ya Mto Nile (Nile Basin Cooperative Framework Agreement-CFA) ifikapo Novemba mwaka huu, kauli ambayo ilipingwa na Membe aliyesema hilo halitatokea.
Maghembe alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha mawaziri wa nchi zilizo kwenye Bonde la Mto Nile kilichofanyika nchini Ethiopia na Membe ndiyo akaja kuikanusha.
"Mimi ndiye Waziri wa Mambo ya Nje na suala la Mto Nile liko chini yangu. Mimi ndiye ninayewasiliana na Rais kuhusu jambo hilo kila wakati na tayari nimemwambia mwenzangu (Maghembe) kwamba kwenye hili aende taratibu," Membe alinukuliwa na gazeti la The East African akitoa kauli hiyo.
Kauli hiyo ya Membe ndiyo inayodaiwa kuwaudhi mawaziri ambao wanaona kwamba Waziri huyo wa Mambo ya Nje ameshindwa kuonyesha heshima kwa mwenzake na kwa Baraza zima.
Mmoja wa mawaziri waandamizi wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete ameliambia Raia Mwema kwamba kupishana na Baraza la Mawaziri kwa sasa ni sawa na kupingana na misingi ya Taifa.
"Hili suala la Mto Nile lina historia ndefu. Tangu enzi za Mwalimu Nyerere msimamo wetu umekuwa kwamba tupewe haki zetu za kutumia maji hayo. Haya mambo ya kuionea huruma Misri hayapo.
"Ukitaka kuamini, subiri Mkutano wa Bunge wa Novemba mwaka huu, serikali itaridhia makubaliano hayo ya CFA kama ambavyo Maghembe aliwaambia mawaziri wenzake wa Maji," alisema.
Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, wananchi wa nchi zilizo kwenye CFA wameonyesha mshangao wao kuhusu hatua ya sasa ya Tanzania wakati yenyewe ilikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kwanza wa mchakato huo ulioanza Mei, 2010.
Serikali ya Ethiopia pamoja na wananchi wa Taifa ndiyo wanaoonekana kuwa wakali zaidi; wakihisi pengine Tanzania ‘imenunuliwa' na Misri inayodaiwa kufanya hujuma za kukwamisha mchakato huo kufanikiwa.
Ethiopia imezindua ujenzi wa bwawa kubwa kuliko yote barani Afrika la kuzalisha umeme kwa njia ya maji linalofahamika kwa jina la Grand Ethiopia Renaissance Dam (GERD) litakalokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 6,000 za umeme. Bwawa hilo litakamilika mwaka 2017.
Misri inapinga ujenzi wa bwawa hilo kwa maelezo kwamba litatumia sehemu kubwa ya maji ya Mto Nile na hivyo kuathiri kiwango kinachokwenda katika Taifa hilo la Afrika Kaskazini.
Ethiopia inachangia asilimia 80 ya maji ya Mto Nile.
Wakati wa zama za ukoloni, mwaka 1929, Misri iliingia katika mkataba na Uingereza iliyokuwa bado na makoloni au ikiwa mdhamini wa baadhi ya nchi za Afrika, ulioipa nguvu na udhibiti wa maji ya mto huo mrefu kuliko yote duniani na wenye urefu wa takribani kilomita 6700.
Mojawapo ya vipengele vya mkataba huo, vinaipa Misri haki pekee ya kutumia maji kutoka katika Mto Nile wakati wa majira ya kiangazi na nchi nyingine zisitumie hadi majira hayo yamalizike.
Katika kile kinachofahamika kwa jina la The Nyerere Doctrine; ambao ulikuwa msimamo rasmi wa Tanzania wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere; "mikataba yote iliyoingiwa na wakoloni kwa niaba ya Taifa hili ni batili kwa vile hii haikuwa nchi yao."
CFA iliundwa kwa lengo la kuweka utaratibu mpya wa matumizi ya Mto Nile, kwa vile bila ya kuwepo kwa makubaliano mapya; maana yake yale yaliyokuwepo awali yanakuwa na msingi kisheria.
Nchi zinazounga mkono CFA ni pamoja na Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia na Sudan Kusini.
Sudan na Misri zinapinga makubaliano hayo kwa maelezo kwamba yatasababisha maji yanayokwenda kwenye nchi zao kupungua.
Mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje ya Misri, Nabil Fahmy, alifanya ziara hapa nchini ambapo katika mazungumzo yake na Kikwete; alidai kwamba nchi yake ni kame na inapata wastani wa siku tatu tu za mvua kwa mwaka na hivyo wanategemea zaidi maji ya mto huo.
Aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, alipata kusema kwamba japo Misri inadai kwamba ina shida ya maji; inaongoza kwa matumizi mabaya ya nishati hiyo kwa njia ya mvuke unaotoka katika Bwawa la Aswan, umwagiliaji wa zaidi ya ekari milioni mbili za mchele katika eneo la Sinai na pia kuhudumia viwanja vingi vya mchezo wa gofu vilivyopo katika Taifa hilo.
Chanzo: Raia mwema
Mada zaidi kuhusu Mipaka ya Ziwa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...umie-usomi-wetu-tusimame-kwenye-ukweli-2.html