Nini kilichofanyika hadi wewe au rafiki kuacha ulevi wa kupindukia?

mimi nakunywa na sina stress kabisa...kuanzia ndoa,familia na hata vijisenti vya kubadilisha mboga sio haba sana...ila sasa kuanzia ijumaa jioni mpaka jumamosi saa6 ni pombe na mimi-never miss.

nakunywa weekend tuuuu...weekdays sipendi hangover kibaruani
Hongera sana na usipotezee hii balance

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Nilipata mpenzi mpya akaniuliza ili uache pombe unataka nikufanyie nini?
chakorii:nikamjibu naomba muda wako.
Mpenzi mpya:.akasema umepata.hakuna lingine?
Chakorii:nikasema hapana sina kingine
Mpenzi mpya: ok
Chakorii:kweli bhana akitoka kazini basi hunipatia muda wake asilimia buku mpaka sasa ninajikuta ndie Rafiki yangu mkubwa sana..nimeachana na groups zote kupitia yeye.Najua kuna watakaojiuliza kwanini sijataka pesandugu mtanzania mwenzangu pesa zinapatikana ndani ya muda wake alionipatiasijui mnanielewa lakini…
Hahaha

Hongera boss.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Baba yangu mdogo aliacha 100%. Ni siku aliyolewa kupitiliza kwenye jumuiko la ukoo, akachukua mfuniko wa ndoo na kuufanya usukani akawa analiendesha pale kati ya watu kwa kutumia makalio. Mwaka wa kumi huu hanywi kilevi chochote..
Ahhahahahahahha

Daaah

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Rehabilitation.
Huwa inafanya kazi. Kwa sababu mara nyingi anayekunywa pombe kupitiliza huwa kuna hali fulani anaipitia kwenye maisha na hata hiyo hali ikipita anakuwa anashindwa tena kurudi kawaida.

Kuna huyu mmoja yeye alikuwa anakaa hata wiki hajanywa ila siku ukiona anakunywa, ndio amefungulia hata mwezi mzima ni kunywa tu na kuzunguka kama nini sijui. Mkisema kesho ataamka vizuri kesho anaendelea.

Tangu atoke sober house ana mwaka na zaidi hajagusa pombe.
Kuna Hawa madaktari Huwa wanalogwa au😀😀😀
 
Nilipata mpenzi mpya akaniuliza ili uache pombe unataka nikufanyie nini?
chakorii:nikamjibu naomba muda wako.
Mpenzi mpya:.akasema umepata.hakuna lingine?
Chakorii:nikasema hapana sina kingine
Mpenzi mpya: ok
Chakorii:kweli bhana akitoka kazini basi hunipatia muda wake asilimia buku mpaka sasa ninajikuta ndie Rafiki yangu mkubwa sana..nimeachana na groups zote kupitia yeye.Najua kuna watakaojiuliza kwanini sijataka pesa😃😃ndugu mtanzania mwenzangu pesa zinapatikana ndani ya muda wake alionipatia😁😁sijui mnanielewa lakini…😉
Kwahiyo nikipata mlevi nikimpa mda ataacha 😀
 
Nilipata mpenzi mpya akaniuliza ili uache pombe unataka nikufanyie nini?
chakorii:nikamjibu naomba muda wako.
Mpenzi mpya:.akasema umepata.hakuna lingine?
Chakorii:nikasema hapana sina kingine
Mpenzi mpya: ok
Chakorii:kweli bhana akitoka kazini basi hunipatia muda wake asilimia buku mpaka sasa ninajikuta ndie Rafiki yangu mkubwa sana..nimeachana na groups zote kupitia yeye.Najua kuna watakaojiuliza kwanini sijataka pesa😃😃ndugu mtanzania mwenzangu pesa zinapatikana ndani ya muda wake alionipatia😁😁sijui mnanielewa lakini…😉
Alafu akiondoka unarudi kua Liquid Chii
 
Kwanza kabla ya kuajadili kuhusu Kuacha Ulevi wa upindukia lazima tujiulize Ulevi wa kupindukia ni nini?Je ni Kiwango cha Pombe,Kiwango cha Ulevi au madhara yanayotokana kunywa Pombe?Je ni wakti gani ambao inabidi sasa utafuta msaada au uchukue Hatua?

Unywaji wowote ule ambao unazidi na ambao kuna hatua unafika huwezi kusema inatosha na ukaacha basi ni Ulevi uliokithiri au wa kupindukia.Tabia za ulevi kupindukia ni Pamoja na kuwe high wakti wote,Kunywa Zaidi ya Bia TATU au KVANT Ndogo MOJA kwa SIKU.Kunywa na kulewa wakti wote yaani asubuhi mchana,usiku na siku zote.Hii ni kwa Upande wa Mwanamke an mwanaume.Hata Hivyo ukifikia hatua ukawa na utegemezi wa alcohol wakati wote katika shughuli zetu basi unahitaji zaidi ya msaada wa kitabibu.

Alcohol kama vilivyo vilevi vingine ni Addictive(Vina Uraibu) Hii ni kutokana na kuwa na Uwezo wa kuufanya mwili uzalishe Dopamine kwa wingi.Hali hii hufanya mtu ambaye anategemea sana pombe kujikuta akiwa na Mood swings kulingana kiwango cha alcohol.Kuna wakti anakuwa na furaha na kuna wakati anakuwa Depressed.

Kuacha Alcohol au Uraibu wowote huwa kwanza kunahitaji mtu afanye maamuzi ya kuacha,kisha aache kuchukua hatua za mwanzoni za kuacha ikiwemo kuepuka maeneo ambayo alcohol inapatikana.Kuepuka Kampani ambayo inapenda kulewa,Kujitenga tabia mpaka na viburudisha vipya.Kutafuta support kutoka kwa wanafamilia,marafiki na wataalam ili waweze kukupa support.Kimsingi Kuacha Pombe ni suala linalowezekana na unachohitaji ni muda na support ya kutosha kutoka kwa wale wanaokupenda.
 
Kuna watu sasa ulevi umesha affect maisha yao socially, spiritually, afya na economically.

Yani kuna watu hawanywi kwa ajili ya msisimuko ila wanazama ndani ya pool ya pombe.

Hebu saidia watu humu steps ulizotumia au jamaa yako alizotumia hadi kuacha uraibu mbaya wa ulevi.
Uamuzi tu, hakuna kingine.
 
Hiyo kwanza ni addiction zaidi ya pombe na ulevi wowote
Huwezi amini Ulaya zimeandikwa kabisa kwenye mashine zote na makampuni yote kuwa ni mbaya kwa afya yako na ukiona imekuzidi nguvu tafuta ushauri nasaha
Kwa kweli kamari ni mbaya sana
kwa kweli haya mambo ni balaaa
 
kwa kweli haya mambo ni balaaa
Halafu wafanyabiashara hiyo ndio wanapata faida kubwa sana kupita kiasi
Kuna kampuni inajiita Bet365 mwenye mali ana watoto ila mtoto wake wa kike kwa mda wa miaka 4 tu alijipatia £1.1b kama nyongeza
Na kaka yake mshahara tu anakula £421m kwa mwaka tena hiyo ilikuwa 2020

Wachezaji ndio wana hasara hapo na hela nyingi wenye mali ndio wanafaidi na serikali inapewa kiasi na maisha yanaenda
 
Kuna utofauti gani kati ya kunywa na ulevi? Kuna ambao wanakunywa hawalewi au huwezi ona kama wamelewa, hawa tunawaweka group gani.
 
Back
Top Bottom