Nini kilichofanyika hadi wewe au rafiki kuacha ulevi wa kupindukia?

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
Kuna watu sasa ulevi umesha affect maisha yao socially, spiritually, afya na economically.

Yani kuna watu hawanywi kwa ajili ya msisimuko ila wanazama ndani ya pool ya pombe.

Hebu saidia watu humu steps ulizotumia au jamaa yako alizotumia hadi kuacha uraibu mbaya wa ulevi.
 
Rehabilitation.
Huwa inafanya kazi. Kwa sababu mara nyingi anayekunywa pombe kupitiliza huwa kuna hali fulani anaipitia kwenye maisha na hata hiyo hali ikipita anakuwa anashindwa tena kurudi kawaida.

Kuna huyu mmoja yeye alikuwa anakaa hata wiki hajanywa ila siku ukiona anakunywa, ndio amefungulia hata mwezi mzima ni kunywa tu na kuzunguka kama nini sijui. Mkisema kesho ataamka vizuri kesho anaendelea.

Tangu atoke sober house ana mwaka na zaidi hajagusa pombe.
 
Ahsante ana

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
1. Usinywe na kampani sijui ya washkaji, bora uwe unaywea nyumbani au ukitoka utoke na mtu wa karibu kama mke (familia).

2. Jitahidi hata kama ni kunywa ile ni weekend tu, na isiwe mda wowote tu, iwe ni jioni.

3. Usiwe na mazoea ya kutembea na hela zote ulizo nazo either ni cash au kwenye miamala ya simu

4. Kama Kuacha moja kwa moja ni ngumu ni lazima upate support ya watu wa karibu (mke/mume) akuelewe na kukusupport kwenye harakati za kuacha.

Day by day, mpaka hali ya akili ya mwili kurudia hali ya kawaida.
 
Nilipata mpenzi mpya akaniuliza ili uache pombe unataka nikufanyie nini?
chakorii:nikamjibu naomba muda wako.
Mpenzi mpya:.akasema umepata.hakuna lingine?
Chakorii:nikasema hapana sina kingine
Mpenzi mpya: ok
Chakorii:kweli bhana akitoka kazini basi hunipatia muda wake asilimia buku mpaka sasa ninajikuta ndie Rafiki yangu mkubwa sana..nimeachana na groups zote kupitia yeye.Najua kuna watakaojiuliza kwanini sijataka pesa😃😃ndugu mtanzania mwenzangu pesa zinapatikana ndani ya muda wake alionipatia😁😁sijui mnanielewa lakini…😉
 
Kuna watu sasa ulevi umesha affect maisha yao socially, spiritually, afya na economically.

Yani kuna watu hawanywi kwa ajili ya msisimuko ila wanazama ndani ya pool ya pombe.

Hebu saidia watu humu steps ulizotumia au jamaa yako alizotumia hadi kuacha uraibu mbaya wa ulevi.
kukwepa kula, kucheki mpira au movie au kupumzika mazingira ya pombe na hii ikapelekea wokovu 🐒
 
Watu wengi wanakunywa pombe sababu ya loneliness na depression iliyotokana na trauma walizopitia

Binadamu wanapigana vita nyingi ndani ya mioyo yao
mimi nakunywa na sina stress kabisa...kuanzia ndoa,familia na hata vijisenti vya kubadilisha mboga sio haba sana...ila sasa kuanzia ijumaa jioni mpaka jumamosi saa6 ni pombe na mimi-never miss.

nakunywa weekend tuuuu...weekdays sipendi hangover kibaruani
 
Pombe mbona unaacha fresh tu, kuna hii kitu ya "Vipi DJ haupigi hewani na unasikiliza ghetto, demu wako chumbani hizi vocals zampigiaaa....." Aisee hiyo kitu ni mbaya sana!
 
Back
Top Bottom