Nini kifanyike kuhusu elimu ili iwe bora

John makonda

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
212
187
MAONI YAKO KUHUSU ELIMU KWA TAIFA LETU

MAONI yangu ni kuwa;

Kwanza nirejelee nini maana ya ELIMU.
ELIMU ni maarifa/ujuzi.wa kupambana na changa Moto za shughuri zako kujiletea maendeleo.
Kumbe changa Moto za maisha ziko nyingi kutokana na mazingira husika hata siku moja mfumo mzima wa ELIMU hauwezi kufanana kutatua changa Moto hizo.

Kwa mukutaza huo ELIMU haiwezi kuchukuliwa kama fashion kua sasa ndio mtindo uliopo.
ELIMU ni hitaji kama mahitaji mengine kama chakula ukiona njaa kama maji ukihisi kiu kama nguo kukukinga na hali ya hewa.

Kwa mfano nchi yetu ina vyanzo vingi vya kumletea maendeleo mwana nchi. ELIMU yetu ijikite katika kuongeza maarifa katika kubadirisha ubora wa kazi zetu kua zenye tija. Hapo tutawavutia vijana kuigia huko kufanya Kwa tija na kutajirika.

Nchi yetu imejaliwa fursa nyingi kilimo kwa mazao mbali mbali wananchi wa eneo husika na tuachane na kilimo cha kutegemea mvua serikali iwekeze kwenye kufanikisha umwagiliaji wakulima walipie huduma hiyo kwa kuwa wanazlisha wajifunze kulima Kwa tija zao lao na wapate maarifa yake toka kulima kupanda kuvuna kuhifadhi Hadi kuongezea thamai.

Vivyo hivyo mifugo waelimishwe ufugaji wenye tija utakayo waletea faida Kwa muda muafaka na kufurahia mifugo Yao Bila kua watumwa wa mifugo na kelo Kwa wengine kwani mkulima na mfugaji wanategemeana mkulima anazalisha vyakula vya mifugo baada ya kuvuna na mfugaji anazalisha maziwa nyama na mbolea.

Wavuvi Nao waelimishwe uvuvi Bora na ufugaji wa samaki tuna maji mengi yanatiririka kwenda baharini yakitumika kuvua kwa tija na kufuga samaki na viumbe vya majini tuta mshukuru MUNGU Kwa nini alitumilikisha nchi hii.

Madini tusisahau pia kueelimisha jinsi ya kuyagundua kuchimba na kuongeza thamani. Maendeleo katika Nyanja mbalimbali yanaweza kusababisha soko la ndani la madini kupanuka.

Nipendekeze sekondari za kata zibadilike ziwe vyuo vidogo kuelimishwa shughuri za sehemu hizo kwani ndio shughuri zao za asiri wanazozijua ni maarifa kidogo Tu watakavyo ongezewa.

Kutoka hapo kama atafauru kuendelea na masomo atapata maarifa zaidi ya pale alipo pata. Kwa sasa watoto wetu wanafundishwa kusoma na kuandika toka shule ya awali mapaka kidato cha sita hawapati maarifa yeyote ni weupe.

Kujua kulima Kwa tija hakuhitaji kujua lugha ya kigeni. Kufuga mifugo mpaka ujue lugha ya kigeni vivyo hivyo uvuvi/madini nayo mpaka ujue lugha ya kigeni nenda ufukweni kama wavuvi wanaongea king'eng'e.
Wachiimbaji wanaongea lugha ya machimboni na wanaelewana hivyo na kipato chao kimeongezeka wao walau wamejitafutia maarifa na wanafanikiwa.

Tukiweza hivyo haya hoja ya ajira itapata majibu kua hatuna tatizo la ajira kinyume chake tutakaribisha waajiriwa sio kubembeleza wawekezji walete ajira si ajabu wakaleta mitaji Kwa ubia wenye kufata masharti yetu.

Karibuni kwa maoni.
 
Kwa sasa watoto wetu wanafundishwa kusoma na kuandika toka shule ya awali mapaka kidato cha sita hawapati maarifa yeyote ni weupe.
kwani na ww ulitoka mweupe mbona ss hatukutoka weupe, Basi ilikuwa ni tatzo lako
 
Mwalimu wa shule afundishe somo kutoka kichwani mwake na siyo kusoma notes.
 
Mtoto afundishwe kusoma na kuandika kiingereza na kiswahili, uzalendo na maadili, stadi za kazi, mazoezi ya viungo, elimu ya afya, elimu ya fedha na fani. Vingine ni kupotezeana muda.
 
Jamani vyakula hapa kwetu vyakula vibovu sana ugali na maharage hivyo haviwezi kujenga ubongo wa mwanafunzi tazama nchi zite zilizo endelea kielimu hawali ugali mbegu
 
Mtoto afundishwe kusoma na kuandika kiingereza na kiswahili, uzalendo na maadili, stadi za kazi, mazoezi ya viungo, elimu ya afya, elimu ya fedha na fani. Vingine ni kupotezeana muda.
Yote tuko pamoja ila sio mpaka afundishwe uzalendo .

Uzalendo ni tunda hutokana na stahiki za mwananchi kupata.

Nakumbuka miaka ya 1960-1980 hakuna aliyefundishwa uzalendo karibia wote tulikua wazarendo haki zetu tulipata ELIMU Bora toka darasani Hadi Kwa vitendo vifaa vya kusoma na kufundisha .hatukupungukiwa

Huduma mbalimbali tulipata hakukua na matabaka wote tuliitana ndugu Leo VIP kuna waheshimiwa sijui na wa......

Hao wanatumia nguvu kubwa kuimba uzalendo huku sio.

Uzalendo ni kupenda nchi yako na watu wake kuwathamini kinyume chake tunda la uzalendo litakua changa kila wakati.

Kutokuthamini vya kwenu ni kukosa uzalendo kushawishi kupenda vya nje ni kukosa uzalendo .

Hoja ya kua tulikua wachache ni mfu kwani na walipa Kodi walikua wachache tofauti na sasa
 
Kwa sasa watoto wetu wanafundishwa kusoma na kuandika toka shule ya awali mapaka kidato cha sita hawapati maarifa yeyote ni weupe.
kwani na ww ulitoka mweupe mbona ss hatukutoka weupe, Basi ilikuwa ni tatzo lako
Kujua Kusoma na kuandika Bila maarifa huo ndio weupe (huna fani)
 
Back
Top Bottom