GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 306
KAMATI Kuu (CC) ya Chadema inakutana keshokutwa Ijumaa Dodoma kujadili pamoja na mambo mengine,
1. ripoti ya mgogoro ulioibuka kati ya madiwani wa chama hicho na CCM kuhusu Meya wa Jiji la Arusha
2. maadili ndani ya chama
3. kupokea taarifa ya utendaji wa chama na hali ya kisiasa ndani ya chama na nchini kwa jumla
4. ..........................
5. Mengineyo.........sakata la Shibuda?
Kauli ya Dr. Slaa
"Tuna ajenda mbalimbali katika kikao hicho cha Ijumaa wiki hii, kwanza ni kikao cha kawaida si maalumu, watu wasifikiri tunakaa kwa suala moja, lakini moja ya ajenda ni kujadili suala mgogoro wa Meya wa na Madiwani wa Arusha kwa mapana yake na kisha tutawapa taarifa,"
Alipoulizwa kama watajadili suala la Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, Slaa alisema
"Hilo suala sinalo mezani kwangu, hivyo hatuwezi kujadili kitu tusichonacho, ila Katiba iko wazi, kuna mamlaka husika ya nidhamu, kamati ya wabunge wa Chadema ndiyo hasa inashughulika na suala hilo, kwanza si sisi, likiletwa kwangu sawa, ila kabla sina cha kusema," alisisitiza Dk Slaa.
Magwanda kwa kuiga bana, eti na wao wanafanyia kikao Dodoma !