Nakumbuka ilikuwa mwaka 2004, miaka 19 imepita nikiwa nimehitimu kidato Cha nne, nilikwenda kumtembelea mjomba wagu.
Nikiwa nyumbani kwa mjomba mjini Tabora mtaa wa Isebya, siku hiyo mjomba alinichukua kwa lengo la kunizungusha sehemu mbalimbali mjini Tabora. Katika pitapita tuliingia katika baa moja (jina nimelisahau) kwa ajili ya kupata angalau soda.
Basi tulimkuta mhudumu (kwa umri nahisi alikuwa kwenye miaka 30 plus) wakasalimiana na mjomba kwa kushikana mikono, na baadaye ikafika zamu yangu. Ile namshika mkono tu nilihisi kupigwa na shoti ya umeme (kitendo cha kushikana ilikuwa kama vile nimeshika waya wenye umeme), ikanibidi kuutoa mkono harakaharaka na kwa nguvu na tukabaki tunashaangaana!
Wana JF hilo tukio mpaka leo sijawahi lisahahu, na kila huwa nikipata utulivu hilo tukio hunijia hakili, na huwa nawaza kuwa ilikuwa ni hali au kitu gani?
Najua humu tuna watu wa kila aina, tafadhali kwa yeyote mwenye ujuzi wa hali kama hiyo kisayansi au namna nyingine au kukutana na jambo kama hilo anaweza kunifahamisha.