Nini hatima ya Ofisi ya Spika iliyojengwa Urambo?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Kipindi cha Uspika wake ndugu Samwel John Sitta alijenga Ofisi ya Spika Jimboni Mwake Urambo ( Sijui huyu alikuwa anawaza nini)

1. Je Haukuwa Ubadhirifu wa Mali ya Uma ukizingatia sasa hivi ile ofisi haitumiki?

2. Je itakuwa ni Busara kwamba Bunge liweke kigezo cha Kuwa Mbunge wa Urambo kama kimojawapo cha mtu Kugombea nafasi ya Spika ili ile ofisi iwe inatumika?

3. Nini Hatima ya ile ofisi je itumike kama Kituo cha afya?

Wapambe wa Sitta akina Malaria Sugu, FaizaFoxy, rizt, Rejao pamoja na kutambua kwamba Mgao wa Vocha Umepungua naamini mtapata nafasi ya kuja kutoa Mawazo yenu pia
 
Jamani hii nchi haiishi viroja

Yaani ofisi ilijengwa Urambo? Kwa kweli hili ni jipya kabisa masikioni mwangu na bila shaka jamaa alidhani atakuwa Spika wa kudumu

Yaani ni wizio mtupu huu, hata ukipakwa rangi gani bado utabakia kuwa wizi na kushindwa kujua vipaumbele vya taifa
 
Mkuu uko Nchi gani wewe? Mzee Sitta alijenga Ofisi ya Spika Jimboni mwake mpaka leo sijui huyu Mzee alikuwa anafikiri nini, lakini ndivyo Viongozi wa Afrika walivyo maana hata Gaddaffi alijenda Makao makuu ya AU kjiji kwao Siirte
 
Hebu tuondoleeni utata ili tuanze kuchangia!ile ni ofisi ya mbunge ama ya spika maana naskia kuna utata juu ya hilo?
 
Mwishoni mwa uspika wa Samwel Sitta, serikali ilijenga ofisi ya spika wa bunge Urambo Tabora ambako ni jimboni kwa spika wa wakati huo mheshimiwa Samweli Sitta. Maswali yangu ni haya:

1. Samweli Sitaa siyo spika tena. Je anaitumia ofisi hiyo au hapana? Na kama ndio anaitumia kama nani na kwa shughuli z
zipi?
2. Spika wa sasa Anna Makinda ameshaitumia ofisi hiyo mara ngapi? Na kama haitumii ni kwanini?!
3. Je utaratibu wa kujenga ofisi kwenye kila jimbo analotoka spika utaendelea?
4. Je ilikusudiwa Sitta awe spika wa kudumu mpaka kufa kwake?
5. Kama ofisi hiyo haitumiki na spika aliyepita na aliyepo ni ya nini? Inafaa kuendelea kuwepo? kwanini isigeuzwe darasa
shule au ghala la kuhifadhia asali?

Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170

IMG_8568.JPG
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.

IMG_8564.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta (Kushoto) ambaye pia ni Spika wa Bunge. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8583.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8456.JPG
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah.
 
Hizi siasa ngumu sana kuzielewa ndugu yangu. Mi nilienda Urambo mwaka 2010 nikaikuta hiyo ofisi cha kushangaza hakuna activity zozote zinazoashiria kuwa hiyo ofisi iko active.
Ilikua ni bad expenditures kwa government kujenga hiyo ofisi. Maswali yako ni ya msingi sana kwa upande wa pili wa shilingi. Wasiwasi wangu ni kwamba haya maswali hata yakipelekwa bungeni hakuna majibu ya msingi yatakayotolewa. Tugange yajayo
 
SITTA anatamani urais, hivyo akiupata "urahisi" atajenga Ikulu pembeni mwa hiyo ofisi. Kisha atatatangaza Tabora ndo Mji Mkuu wa nchi!

Sitta bado anatapatapa baada ya kuangukia pua kwenye uspika!
 
Naomba kujuzwa ofisi hiyo ilijengwa kwa fedha zipi!...je iliwekwa kwenye bajeti ya Bunge au ni fedha za mfuko wa jimbo?
Ni wazi ni pesa za serikali kutoka hazina, inaweza kuwa kupitia bunge kwani hata hizo za mfuko wa jimbo ni za serikali. Kwa ufupi ni kuwa imejengwa na serikali ambayo vyanzo vyake vikuu vya mapato ni kodi inaliyopwa na wananchi na misaada kutoka nje
 
Ushahidi mwingine kuwa hawa wangine tunawachekea lakini nao ni hatari, yeye alijua atadumu kwenye usipika kama Chifu Adamu Sappi Mkwawa! Na haya yote yalifanyika mbele ya macho ya maccm bila hata kutia neno!
 
Mwishoni mwa uspika wa Samwel Sitta, serikali ilijenga ofisi ya spika wa bunge Urambo Tabora ambako ni jimboni kwa spika wa wakati huo mheshimiwa Samweli Sitta. Maswali yangu ni haya:

1. Samweli Sitaa siyo spika tena. Je anaitumia ofisi hiyo au hapana? Na kama ndio anaitumia kama nani na kwa shughuli z
zipi?
2. Spika wa sasa Anna Makinda ameshaitumia ofisi hiyo mara ngapi? Na kama haitumii ni kwanini?!
3. Je utaratibu wa kujenga ofisi kwenye kila jimbo analotoka spika utaendelea?
4. Je ilikusudiwa Sitta awe spika wa kudumu mpaka kufa kwake?
5. Kama ofisi hiyo haitumiki na spika aliyepita na aliyepo ni ya nini? Inafaa kuendelea kuwepo? kwanini isigeuzwe darasa
shule au ghala la kuhifadhia asali?

Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170

IMG_8568.JPG
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.

IMG_8564.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta (Kushoto) ambaye pia ni Spika wa Bunge. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8583.JPG
Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

IMG_8456.JPG
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah.
 
Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170

Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.

Maisha Bora kwa kila mtanzania

Mahesabu yenyewe itakuwa kama hivi; 170,000,000 x239= 40,630,000,000ts

Alafu akina mama pale Muhimbili wanajifungulia wakiwa kwenye sakafu!
Wale mashabiki wa S.Siita wanatakiwa kujitambua kuwa ni mtu wa aina gani!
 
Hii inji lika mtu anajiamulia la kufanya kwani ni kama shamba la bibi hasa ukiwa mwanaCCM!inji hii imekuwa shamba la bibi ila nadhani mwisho wa haya unakaribia naona kama si mbali sana inji itakombolewa
 
Nimeona ni ofisi ya mbunge sio ofisi ya spika. Kisheria ofisi ya spika ni bungeni dodoma na ofisi ndogo jijini DSM. Ofisi yake ni ya gharama sana ya Membe pale Mtama ni nusu ya bei!
 
Back
Top Bottom