Nini cha kwanza kabisa kwa binadamu, humsukuma anapoamua kuoa ama kuolewa?

Umeoa/umeolewa/utaoa/utaolewa nini kitakusukuma/kilikusukuma kufanya hivyo?

kwa imani yangu mimi(uislam)unasema wazi kabisa mtu anayekidh vigezo vya kuoa aoe,,,,kuoa ni kukamilisha dini,ibada ya alooa na asooa ni tofauti kabisa,ila unapaswa kuoa iwapo tu utakua na uwezo wa kumvisha,kumlisha na kumpa mahala pa kulala mkeo,,,,usioe wakat huna uwezo huo,usije ukampa shida mkeo,,,,,,,SO KUOA NI IBADA KAMA SALA AU FUNGA YA RAMADHAN,KWA WAISLAM(nimechangia kama mwanaume ambae anapaswa kuoa na si mwanamke ambae anaolewa
 
maswali yako yamekaa katika kufanya uzi wako uonekane mreeeefu,,,,,,kama hamjaoana mnamchukiza mungu,ofcoz unalijua hili,,,,,,
Umeiangalia ktk upande mmoja tu, ndoa zisizomshirikisha mungu unaziweka kundi gani?

Nadhani ungeeleza wewe binafsi kutoka moyoni mwako kisha uchangie kwa ujumla!
Lengo ni elimu ya mahusiano mkuu, urefu wa uzi hauna mantiki ikiwa hakuna hoja na majibu mujarabu!
 
Mie ukweli nilichoka na sheria za nyumbani mpaka madukani lazima upelekwe ukichelewa kurudi utakiona kilichomtoa kuku
manyoya,nilikua nafanya kazi lakini story ikawa hiyo hiyo nikaona bora niolewe yaishe tutapenda huko huko mbele ya safari
lakini alhamdulilah namshukuru mungu mpaka hapa tulipofikia...

uliamua kujilipua loh. . .
 
nadhani sababi hizi zinachangia sana kwa mtu kupata msukuma wa kuoa/kuolewa

1.Upendo - umempenda mtu kiasi ambacho unahisi huhitaji kuwa nae mbali
2. kupata watoto na kusaidiana katika kuwalea
3. mimba - binti anapata mimba then anaamua tu kuolewa kuliko kuzalia home
4. msaada wa kipato - mkiwa wawili ni rahisi kusaidina kipato, ingawa pia kuna wengine wanaingia ktk ndoa kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao au sababu kampata mtu mwenye kipato
5. Kampani - mke na mume ni kampani nzuri sana
6. kuiga - wengine wanaiga sababu marafiki au watu wao wa karibu wameingia katika ndoa
7. kutoka nyumbani - wengine wanataka tu kutoka home
8. hofu ya kuachwa - laba asipo oa/olewa anaweza kuachwa
9. Uangalizi - kuwa na mtu karibu anayemjali
10. Ngono
 
Kampani, kusaidiana, heshima kutoka kwa jamii na kufanya tendo takatifu la ndoa.
 
Umeiangalia ktk upande mmoja tu, ndoa zisizomshirikisha mungu unaziweka kundi gani?

Nadhani ungeeleza wewe binafsi kutoka moyoni mwako kisha uchangie kwa ujumla!
Lengo ni elimu ya mahusiano mkuu, urefu wa uzi hauna mantiki ikiwa hakuna hoja na majibu mujarabu!

ndoa zisizomshirikisha mungu,,,naziweka kwenye kundi la kutomshirikisha mungu,,,,,,,na zinazomhusisha mungu zitakaa HUKO
 
nadhani sababi hizi zinachangia sana kwa mtu kupata msukuma wa kuoa/kuolewa

1.Upendo - umempenda mtu kiasi ambacho unahisi huhitaji kuwa nae mbali
2. kupata watoto na kusaidiana katika kuwalea
3. mimba - binti anapata mimba then anaamua tu kuolewa kuliko kuzalia home
4. msaada wa kipato - mkiwa wawili ni rahisi kusaidina kipato, ingawa pia kuna wengine wanaingia ktk ndoa kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao au sababu kampata mtu mwenye kipato
5. Kampani - mke na mume ni kampani nzuri sana
6. kuiga - wengine wanaiga sababu marafiki au watu wao wa karibu wameingia katika ndoa
7. kutoka nyumbani - wengine wanataka tu kutoka home
8. hofu ya kuachwa - laba asipo oa/olewa anaweza kuachwa
9. Uangalizi - kuwa na mtu karibu anayemjali
10. Ngono

Umejitahidi sana ila binadamu wote ni wanafiki kwenye hili suala. Ukweli ni kwamba hiyo uliyoiweka mwisho ndo marriage yenyewe kwa maana kwamba kama mke hana uke au mume hana uume basi ndoa haipo hapo. Kupata mtoto ni matokeo ya uwepo wa tendo hilo kwamaana kwamba mtu anayekuvutia (namaanisha jinsia tofauti) basi lengo kuu si kuenjoy hiyo sura bali kitandani (hasa kwa wanaume). Sidhani kama mama yako au kaka yako anakuvutia kiivi.
 
Hizo ndio sababu za kuwa na mwenza

-Muda umefikiwa wa kuolewa
-Nimepata kipendacho roho
-Kuanzisha familia

Kuna wanaooa au kuolewa kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, kwakweli circumstances zinapishana from person to person. Na pia malengo yanapishana kutokana na muda/wakati huo maybe my criterias will change in year to come. You really don't know!
 
Back
Top Bottom