Nini cha kufanya kujinasua na tatizo la umeme tanzania !!

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Ni muda sasa nchi yetu imekuwa katika adha ya upatikanaji wa nishati itokanayo na umeme. Kwa maoni yangu nafikiri ili tuepukane na tatizo hili kama nchi tunatakiwa kufanya yafuatayo:

1) Kwanza kuepukana na dhana hii ya kila uchao ya kufikiria umeme wa maji kama ndio njia pekee ya kutupatia nishati hii. Ukiangalia listi ya vyanzo vya umeme duniani umeme utokanao na maji unachangia chini ya asilimia mbili tu. Angalia nchi zote zenye maendelea ya viwanda duniani utaona kuwa umeme wa maji unachangia sehemu ndogo saana

2) Kama nchi sasa tuelekeze jitihada zetu zote za kuzalisha umeme utokanao na makaa ya mawe. Ukiacha umeme wa Nuklia, duniani kote umeme wa uhakika unatokana na makaa ya mawe. Bahati nzuri mungu katujaalia tuna reserve ya kutosha ya makaa ya mawe na pia gesi. Basi kama nchi jitihada zetu zote tuzielekeze katika vyanzo hivyo viwili yaani makaa ya mawe na gesi.

3) Kuachana kabisa na hili lidudu liitwalo NATIONAL GRID. Hili ndilo linadumaza kabisa mawazo mengine ya kufikiria vyanzoo vingine vya umeme kama upepo, geothermal, biomass nk. Hili linaweza kufanywa kwa kuanza na kulifumulia mbali shirika la umeme la Tanesco na kuanzisha vijitanesco vingi katika kila mkoa. Ukienda nchi kama Finland kila mkoa wanashirika lao la uzalishaji umeme mfano TURKU ENERGY OY, HELSINKI ENERGY OY nk. Ukianzisha haya mashirika au makampuni kila mkoa yatajitahidi kutafuta vyanzo vingi vya umeme ndani ya mkoa wao. Kwa mikoa itakayozalisha umeme mwingi zaidi ya uwezo wa matumizi yao basi wataweza kuuza mikoa mingine.

4)Kama nchi wakati muafaka sasa umefika kama nchi sasa kuamua rasmi kuwa 20% ya mahitaji yetu yote ya nishati yatokane na vyanzo kama Biomass. Nikiongelea Biomass nina maana ya vitu kama mabaki ya mazao mashambani, mimea mbali mbali, Takataka nk. Kwa hili kama nchi tunatakiwa tu kufanya maamuzi magumu, maana kama ni technolojia ya uzalishaji nishati kutokana na biomass duniani inapatikana. Nchi kama Sweden eneo lote la Skåne CITY BUS zao zote zinatumia BIOGAS, itokanayo na takataka na mazao ya mimea. Hivyo kama nchi tukiamua tutaweza.

5) Kama nchi tuanze kufikiria kuwekeza katika kuzalisha umeme utokanao na NUklia hii ni kutokana na ukweli kuwa tuna reserve kubwa ya madini ya Uranium, japo katika hili sina matumaini saana kutokana na ukweli kuwa mataifa makubwa huenda yakatuwekea VETO.

Nafikiri tukifanya hayo adha ya mgao wa Umeme/Giza utakuwa historia

Sijui ni kwa nini watu wengi mnaponda umeme wa maji hivi mnajua kuzalisha unit moja ya umeme wa maji ni shilingi ngapi na kuzalisha unit moja ya umeme wa gesi au makaa ya mawe ni gharama kiasi gani?

kwa taarifa yako umeme wa maji ni bei nafuu sana maana hauna running cost. hebu fikiria gari lako lingekuwa lintumia maji ungekuwa unasevu kiasi gani kwenye gharama unazotumia kununulia mafuta.

unatakiwa kutambua kuwa umeme wa maji unategemea jiografia hivyo uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji unakuwa mdogo kwa sababu ya jiografia wengi haziwaruhusu.

badala ya sisi kutake advantage ya kuwa na jiografia ya kuturuhusu kuzalisha umeme wa gharama nafuu nyie mnaiponda bila kuwa na technical au financial grounds.

kwa nini tusizalishe umeme kwa kutumia maji na gesi na makaa ya mawe tukauza tukapata fedha ?

mimi nashauri umeme wa maji tuufanye ndio chanzo namba moja gesi iwe ni dharula tu pale mabwawa yanapokauka.

watafiti sasa wapendekeze kutafuta njia ya kutufanya tutumie gharama nafuu katika operation mode hiyo.

Back
Top Bottom