Ningefanya kampeni NY, Florida na California, kama uchaguzi ingekuwa ni jumla ya idadi ya wapigakura

Yethero Mgale

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
525
228
Katika kile kinachooneka kuwajibu wapinzani wake, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook

"If the election were based on total popular vote I would have campaigned in NY, Florida and California and won even bigger and more easily!"mIkumbukwe kuwa Trump alishindwa na mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Hillary Clinton kwenye kura za wananchi (Popular Vote), lakini Trump akamshinda Hillary kwenye kura za wawakilishi wa states ( Electoral college vote)

Kwa utaratibu wa Marekani, mshindi hutangazwa kwa kupata kura nyingi za wawakilishi wa States ( Electoral College Vote) ili kuepusha states zenye wapigakura wachache kuchaguliwa Rais na States zenye wapigakura wengi mfano California, New York na Florida. Yaani ukijumlisha idadi ya wapigakura wa California, New York na Florida ni kubwa kuliko idadi ya states 47 zilizosalia.
 
Back
Top Bottom