Ninaomba tafsiri ya DINI na UDINI

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Naombeni tofauti kati ya maneno yafuatayo: UDINI na DINI, maana imezuka tabia humu katika jukwaa mtu akiwa anatetea dini yake anaitwa MDINI. Wataalamu tufafanulieni
 
paulss! Ukimsemeshaa mtu asiyejua lugha unayoongea ni kama unaongea peke yako. Kwa hiyo MS kama ni tusi ujue umejitusi mwenyewe na kama ni sifa ujue umejisifu mwenyewe. Siumii wala sifurahii kwa kuwa sijui maana yake.
 
Dini (kutoka Kiarabu ) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji..
Kuna dini nyingi duniani Miongoni mwazo ni;
Pamoja na hizi kuna dini mbalimbali zinazojulikana tangu karne nyingi duniani hata kama idadi ya wafuasi si kubwa sana kwa mfano:
Pia kuna imani ambazo zinafanana kwa namna fulani, hivyo mara huhesabiwa kama imani mbalimbali za pekee, mara huhesabiwa kama kundi la dini zenye misingi ya pamoja au kama matawi ya imani moja. Zikitazamiwa pamoja idadi ya wafuasi ni kubwa kiasi lakini zikihesabiwa moja-moja idadi ya wafuasi si kubwa sana, kama vile:
Udini
Ndugu zangu UDINI ni ile hali ya binadamu kuonyesha dharau na chuki isiyokuwa na sababu kwa imani au dini isiyokuwa yake. Kuonyesha kuwa hakuna dini sahihi ila dini sahihi ni dini fulani na waumini wake. Pia ni hali ya kwa kueneza hofu miongoni mwa watu wa imani au dini nyingine kuhusiana na imani au waumini hao. Udini pia ni pale mtu anapo onyesha hali ya ubaguzi kwa dini au waumini wa dini fulani kwa kuwatenga wao kiuchumi, kijamii na hata kimazingira kwa dharau au kuwaona wapo chini ya ustaarabu kulingana na tamaduni wa jamii hiyo. Zaidi ya hapo Udini ni hali ya kuwapendelea wale wanaoamini katika imani yako ya kidini

Umejibu vizuri, hongera kijana.
 
Naombeni tofauti kati ya maneno yafuatayo: UDINI na DINI, maana imezuka tabia humu katika jukwaa mtu akiwa anatetea dini yake anaitwa MDINI. Wataalamu tufafanulieni
DINI ............ Imani ya kiroho aliyonayo mtu juu ya MUNGU anayemuamini
UDINI............. Ni kutaka au kupewa jambo lolote lisilo na uhusiano na DINI kwa sababu ya DINI yako. Unayepewa ni MDINI na anayekupa ni MDINI
 
Mimi nitaeleza na kutela mifno ya Udini. kutumia wakristu na waislam ambao sisi ndio wengi tanzania

Udini ni hali ya mtu

  1. kukubaliana na kutokubaliana na hoja fulani wa kuangalia tu kama inanufaisha dini yake badla ya kuangalia maadili ya
Mfano. halisi wa mahakama ya kadhi.

  • Kwa sababu ya udini wasialam wote wanaweza kuwa wanaona ni haki na ni jambo sahihi kabisa kuwa atika katiba.
  • Kwa sabbau za uidini wakristu pia tunaona si haki na si jambo la kawaida mahaka ya kadhi kuwa katika katiba
Lakini ukweli unabaki kuwa awe muislam au mkristu au budha au mpagani akiweka maslahi ya dini yake pemebeni na kama ni mwanasheria anayefuata maadili ya taaluma ya sheria na na kufanya uchambuzi wa sheria na katiba ya tanzania then Ukweli unabaki mahakama ya kadhi haina nafasi kwenye katiba ya tanzania.

2 Kushindwa kuvumulia na kukubaliana na imani na maisha watu wa imani
nyingine pia ni udini

Mfano.

  • Jirani ana fuga nguruwe muislam kwenda kushtaki au kunungunika kwa jirani yakekufga nguruwe ni udini
  • Mkristu ajirani na msikiti kulalamika/ kushatki au kunugunikia vipasa sauti kila alfajiri na kumsumbua kwenye usingizi pia ni udini
3. Kusifia kitu au maamuzi fulani amabyo wazi yanaonekana ni mabovu sababu
tu yaemfanywa na mtu wa dini fulani. Vile Vile Kukashifu na kushindwa kusifia
hata mmauzi sahihi sabbu tu yamefanywa namtu wa dini tofauti. Kuogopa
kukosoa sababu ya dini . Au kusdhindwa kusifia sababu ya dini

Mfano
......
Ngoja niishie hapaunaweza kuwa na mfano hai
 
Back
Top Bottom