Nina swali kuhusu Negligence

Bob Dylan

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
207
219
Hivi mtu au fundi akija kufanya kazi kwako wakati haupo na akapatwa na majeraha au akaumia anaweza akaku sue for breach of duty of care au for any damages ?
 
Jibu ni NDIYO, unapaswa umlipe...hata hivyo inategemea na mazingira ya tukio lenyewe.
Jaji Atkinson alitoa tafsiri ya neno Uzembe katika kesi maarufu ya Donoghue v. Stephenson akifananisha na maneno toka kwenye
Biblia "mpende jirani yako kama nafsi yako" kisha akatafsiri neno jirani kuwa ni mtu yeyote ambaye ataathirika na kitendo changu au kutokutenda kwangu. Kama mazingira ya nyumbani kwako uliyaacha kihasarahasara na kusababisha mtu mwingine kuumia/ kupata
madhara basi ni lazima uwajibike, lakini ni pale tu muathirika atakapopeleka shauri lake mahakamani na kuthibitisha madhara aliyoyapata. Kumbuka hata mwizi anapokuja nyumbani kwako kukuibia hapaswi kupata madhara yeyote kwani yeye pia ni binadamu. Mfano akikuta sakafu yako inateleza sana akaanguka na kuumia itakupasa umlipe endapo atakushitaki na hakimu akaridhika kuwa unalo jukumu "Occupier's Liability", japo hapo kanuni kisheria ya "Hakuna mtu anayepaswa kufaidika kutokana na uovu wake..." yaweza kukusaidia... Endapo fundi wako amekupeleka mahakamani tafuta wakili aliyepo jirani yako akuwakilishe au akupe ushauri...KUMBUKENI NI MUHIMU KUWATUMIA MAWAKILI WETU KWANI WAMESOMA KWA AJILI HIYO....
 
Back
Top Bottom