Nina haja ya dhati Lamomy wa JF kwenye maisha na huduma yangu daima

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,154
11,560
Namshukuru Mungu kwa ajili ya yako na yangu, kwa wasaa huu muhimu, ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu kwetu sisi sote.

Tumeipewa zawadi hii bure na tuitumia bure, na kwahivyo yatupasa kuitumia vizuri kadiri tuwezavyo na kwa uaminifu, huku tukimshukuru yeye pekee daima, kila wakati tunapopata wasaa wa kufanya hivyo.

Namsalimu sana mtumishi, msaidizi wangu mpendwa sana na kipenzi cha haja ya moyo wangu Lamomy popote alipo.

Namuombea kwa Mwenyezi Mungu ulinzi mkali sana wa kiroho na kimwili uambatane nae daima kila mahali anapotekeleza majukumu, kazi na mahangaiko yake ya kila siku.

Milango yangu ya kimwili na kiroho iko wazi daima kwajili yake, na saa zingine inalala wazi usiku na mchana ikitazamia ujio wake wakati wowote maishani mwangu katika Roho na kweli ya Mungu.

Namuomba Roho Mtakatifu ahuishe nafsi yake Lamomy ilainike na ipate kuskia sauti ya wito wa Mungu kwake dhidi yangu.

Afungue moyo wake uweze kutambua na kujua vema nia, haja, makusudi na madhumuni yangu mema sana kwake na yenye baraka, neema, sifa na utukufu wa Mungu daima na milele....

Lamomy katika dhiki na faraja daima na milele.

Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
 
Ukute li id limoja linajitongoza!
Anyway mkawe na mapenzi ya dhati yasiyo na tashtwitwi na mapigano bali hamuhamu na ushawishi..
asubuh ya leo nimeskiza wimbo wa ndoa wa baraka sana, kwa wenye ndoa na wachumba wanaowaelekea kwenye ndoa....

Baadhi ya maneno ya Baraka katika wimbo huo yanasema.....

Nanukuu...

"Mke si kidude cha kujaribu miguu yako,
Mume si kipaza sauti cha kupigia kelele,
Mpendane, msichokozane Amani ya Bwana iwe ndani yenu"

Mwisho wa kunukuu.
Nimebarikiwa sana

Barikiwa sana mpendwa KENZY
 
Back
Top Bottom