Nina dogo amemaliza Form Four, nimpeleke shule/chuo gani?

The dumb Professor

JF-Expert Member
Dec 10, 2023
660
1,401
Wakuu,

Naombeni ushauri. Nina dogo amemaliza form four, je nimpeleke shule/kozi gani kwa ajili ya future yenye uhakika?

Ana division 1 ya 10

NB: uwezo wa kumsomesha chochote popote upo.
 
Kuna watakuja kusema Anika tokeo lake hapa ndipo wakushauri.

Mpeleke veta.
 
Msikilize yeye anataka nini kisha anzia hapo. Watoto wa leo pasua kichwa, licha ya matokeo yake mazuri usije shangaa anataka aende kusoma stashahada kwenye vyuo vya kati huku wewe malengo yako ni kumpeleka kidato cha tano hatimaye chuo kikuu.

Cha msingi alenge kujiajiri baada ya masomo ili asije akaugua sonona kwani ajira pia ni changamoto.

Hongera yake kwa matokeo mazuri.
 
Me nashauri mpeleke chuo chochote anachopenda yy then akimaliza mpige na veta kdg akitoka hapo utanitafuta uje unishukuru ila akienda advance sijui huko kashapotea labda kama ww mzazi au mlezi uwe unajiweza
 
Chuo gani na kozi gani?
NB: Chochote Popote hata Mwezini uwezo upo
 
Msikilize yeye anataka nini kisha anzia hapo. Watoto wa leo pasua kichwa, licha ya matokeo yake mazuri usije shangaa anataka aende kusoma stashahada kwenye vyuo vya kati huku wewe malengo yako ni kumpeleka kidato cha tano hatimaye chuo kikuu.

Cha msingi alenge kujiajiri baada ya masomo ili asije akaugua sonona kwani ajira pia ni changamoto.

Hongera yake kwa matokeo mazuri.
Aah dogo wa form4 kwani basi anaelewa kitu?
Leo anataka udaktari kesho uinjinia, kesho kutwa uloya...haeleweki.

ila anataka akimaliza apate kazi itayomlipa 5M+
 
Wakuu,

Naombeni ushauri... Nina dogo amemaliza form four, je nimpeleke shule/kozi gani kwa ajili ya future yenye uhakika?

Ana division 1 ya 10

NB: uwezo wa kumsomesha chochote popote upo.
Acha aende acafemic path kawaida kwa ssaaa.....akasome atachopenda....mila akimaliza form 6 ...fanya aende China kwa course yyt atayopenda asirudiii bola masters....akiwa china aweze kwenda nchi mbali mbsli ulaya na US kupata ecposure......kila heri akiweza kusoma uhandisi wa ndege ......atafaidika sana huko baadae.....utanishukuru baada miaka 20 mbeleni.....
 
Binafsi nashauri mpeleke chuo akasome kozi za afya, Muhimbili ama Bugando. Asome diploma akimaliza aende chuo kikuu akasomee udaktari ama famasi.

Hakikisha mwanao ama ndugu yako unamjali hakosi kusoma zile zinaitwa Noble Professions.
1. Uhasibu
2. Udaktari/Afya.
3. Engineering.
4. Sheria.
5. ICT

Elimu ya form six haina maana yoyote kwa sasa. Ni wastage of time and resources. Msaidie apate skills, aanze kuingia kwenye soko la ajira mapema, aanze kuujua mchezo.
 
Kama umri Bado na anazo akili za kusoma pia uchumi wako unaruhusu mpeleke five na six,chuo ni kinyume na hayo.
 
Acha aende acafemic path kawaida kwa ssaaa.....akasome atachopenda....mila akimaliza form 6 ...fanya aende China kwa course yyt atayopenda asirudiii bola masters....akiwa china aweze kwenda nchi mbali mbsli ulaya na US kupata ecposure......kila heri akiweza kusoma uhandisi wa ndege ......atafaidika sana huko baadae.....utanishukuru baada miaka 20 mbeleni.....
Kama uchumi unaruhusu na utulivu wa mtoto upoje,nje ni the best.
Akapige hata coarse za ubaharia atatoboa
 
Back
Top Bottom