Nimweleze mama kuhusu huyu best friend wake?

Mi-Ann

Member
Jun 9, 2020
81
251
Salaam Aleikh

Huu uzi ni kwa ajili ya kuomba ushauri. Nina Imani wapo humu watu wenye mitazamo ya kuona kwa mapana madhara au faida ya hili jambo. Nimejaribu kuwaza kwa Zaidi ya miezi minne sasa namna nzuri ya kumweleza mama yangu kuwa rafiki yake mkubwa, yaani shosti shosti kweli, ndiye anayemzunguka kwa kutoka kimapenzi na baba.

Naomba nieleweke kuwa lengo langu sio kutoa shutuma za usaliti wa baba, maana kwanza naelewa sio mchepuko wake wa kwanza (au pekee), pili men ambao hawana nyumba ndogo hawafiki hata asilimia moja, na tatu huyu shosti wa mama hajaanza leo kutoka na mzee (don’t get me wrong, simkandii mzee. my dad is one of the best people I have ever known, sio kwa kuwa ni baba yangu, ila huyu mzee ni Zaidi ya binadamu, pamoja na mapungufu yake). Lengo langu ni atleast kuvunja huu urafiki wa mama na mchepuko wa baba (who by the way ni pisi moja kali mno).

Hii ni kwa sababu, ingawa wamekua mashost kwa muda mrefu, ila miezi ya karibuni wamekua Zaidi ya marafiki. Wameanza mipango ya kufanya investment za pamoja. Sasa hii inanipa wasiwasi mom anaweza pata Zaidi ya mshtuko akija kugundua. My plan is atleast ajue huyo sio shosti tu, ni mke mwenza. Nilishajaribu kumface huyu shosti wa mama ofisini kwake, alichonijibu niliona kabisa hana mpango wa kuachana na mzee, yeye anamuita kwa jina la kwanza, Paul (sio jina halisi).

Kwa wasiopenda stori ndefu mnaweza ishia hapa na kunipa ushauri wa nini cha kufanya. Ila kwa wanaoweza kuendelea ningependa kutoa background information ya hii triangle.

My mom alinipata mimi akiwa na miaka ishirini kamili, akiwa bado ni mwanafunzi wa diploma. My dad wakati huo alikua ndo amepata kazi serikalini. wamezidiana miaka mitano tu na kwa sasa dad ana miaka 48. Huyu shosti yake mama kanizidi mimi miaka 12 (najua nimewapa kazi ya kukokotoa hahaha, ndo lengo langu). Nilipokua na miaka nane hivi, dad alipata kazi ya uhadhiri nje ya nchi (hapahapa Africa), so baada ya kama mwaka kule, akafanya mpango mom akapata pia kazi ubalozini, so tukawa wote nje ya nchi for years.

Baadae mom akarudishwa wizarani hapa DSM, so ikanibidi nirudi nae. Lakini kabla ya uhamisho, kuna dada aliletwa kuwa mtumishi ubalozi wanchi tuliyokuepo. Huyu dada ndo huyu shostito wa mama. So urafiki wao ulianza kitambo, na hata baada ya kurudi Tz na yule dada kubaki kule, waliendelea kuwasiliana kama marafiki. Kwa kuwa kabla ya mama na mimi kuondoka kule, huyu dada alikua keshapazoea home, nadhani hata baada ya kuondoka mazoea yaliendelea na nahisi mahusiano yake na dad ndo yalianza kipindi hiki.

Mzee aliendelea kukaa huko kwa miaka kadhaa, hadi mimi namaliza form four alikua bado kule. Na kila nilipokua naenda nlikua namkuta yule dada yuko involved sana na mzee. Yaani kunipokea airport watakuja wote, kama ni shopping tunaenda wote, tukiamua kwenda dinner mahali atakuepo, yaani ingawa nilikua bado katoto ila nlijua tu mzee anakula huyu dada. Ila wala sikua na shida sana. Kwa sababu, dada mwenyewe alikua ananijali mnoo yani, nikienda nae shopping ntanunuliwa nguo za fashion current, vipodozi, viatu ….. I really liked her, so akawa kama dada ambaye sikuwa nae, ingawa mwenyewe alipenda nimuite ma’mdogo. So nikawa namuita ma’mdogo Judy (sio jina lake). So hata nikiwa home na mom, akipiga simu mara zote alitataka tuongee pia, so mama alikua ananipa simu napiga nae stori.

Nikiwa kidato cha tano ndo mzee alirudi rasmi bongo. Na wala haikupita hata mwaka, Judy nae akarudi bongo. Akaniambia ameacha kazi ili ajikite kwenye biashara. Nikaona anafocus na maisha. Ila baadae nikajua aliacha kazi ili awe karibu na mzee, ingawa ni kweli alianzisha biashara na in terms of money, anafanya vizuri. Judy aliporudi ndo ukaribu na familia yetu ukaongezeka, weekend nyingi yupo na mama, au atanipigia simu niende kwake, hii hasa nlipoanza chuo. Cha ajabu mara nyingi mzee akisafiri, na yeye after few days utasikia anasema anasafari ya kibiashara.

Ukaribu na mama umekua Zaidi ya urafiki. Kuna kipindi mama alikua na matatizo flani, Judy alijitoa utadhani ni tatizo lake, ikiwepo kutoa pesa zake, kusafiri na mama mpaka India kwa matibabu ambako alikaa Zaidi ya miezi mitatu, mpaka waliporudi wote. So she is close to her.

Siku nilipohakikisha kuwa wana uhusiano, ni jioni ya siku ya Valentine’s day nikiwa mwaka wa pili. Judy alinipigia simu kuniuliza kama nitaenda kwake, maana nilishazoea kwenda sometimes bila hata taarifa. Siku hiyo kwa kuwa kesho yake nlikua na test, nikamwambia sitaenda, basi akanitania “au utakua kwa shemeji?”, nikamwambia hapana nina mtihani, akasema sawa basi ananiondoa kwenye share ya chakula cha jioni, nikamwambia poa.

Kumbe lengo la kunipigia simu ni ili kupata uhakika wa kumleta dad home kwake. Sasa mimi baada ya ile simu nikaanza kujisikia noma, kwanza Judy alishawahi nikuta angle mbaya na jamaa mmoja hivi, ingekua sio ajabu kama angekua kijana umri sawa na wangu, ila mkaka kanizidi miaka inayoonekana kabisa hahahha(hii ni story ya siku nyingine panapo majaaliwa), so wasiwasi wangu ilikua atahisi niko kwa huyu jamaa, alafu anaeza mwambia mzee. So nikachukua uamuzi wa kwenda.

Ilikua mida ya saa mbili usiku. Cha kwanza kuona ni gari ya mzee imepaki kwa nje, nikapiga simu haikupokelewa, bahati nzuri mlango wa kupita watu kwenye geti kubwa haukua umefungwa, so nikasukuma nikaingia, nje ya mlango wa mbele ya nyumba nikaona viatu vya mzee. Ingawa sikua na sababu ya kususpect chochote, maana inaweza kuwa mzee kaja na maza kumtembelea Judy, ila kuna ka hisia ka curiosity kakanijaa, sikugonga mlango, nikazunguka dirishani (mtanisamehe jamani), ingawa sikupiga chabo, ila sauti nilisikia. Nlichofanya nikarudi mbele ya nyumba nikakaa nisubiri wamalize.

Nlivyoona activities za sebuleni na jikoni zimeanza ndo nikagonga mlango. Kama kawaida wakajidai ndo kwanza mzee kafika, alipita tu kupeleka some documents na nini, I decided to go along with their story… So ingawa nimefahamu kwa muda mzee anatoka na Judy, ila ile kuconfirm ikanifanya nianze kujihisi guilty kila nikimuangalia mama. Nahisi kama na mm namsaliti vile. But nikaona ni busara kukaa kimya, akijua ajue mwenyewe. Ila nikapunguza mazoea na Judy, sana mpaka akawa anauliza kulikoni.

Sasa miezi michache iliyopita ndo wakaanza mipango yao ya kuinvest pamoja. Na sio investment ndogo, ni zile za ukitapeliwa unaua mtu. Yaani my mom ni kama ameweka all that she has.. ninachojiuliza, akijua huyu anayeinvest nae ni mke mwenza si atachanganyikiwa akili… moyo wangu unaniambia napaswa kuvunja huu urafiki wa kinafiki, ila pia mama hana rafiki mwingine aliye close kama Judy naona kama her life itakua boring hivi…..

Niliamua kwenda ofisini kwa Judy one day, nlimwambia najua anatoka na dad na nikamuomba aache kumsaliti rafiki yake…. Judy akakaa kimya kwa muda mrefu, nikaona kabisa maneno yamemuingia maana machozi yakawa yanamdondoka, akawa hawezi sema chochote ingawa nligoma kuondoka mpaka anihakikishie atamuacha mzee. Judy akawa ameinamisha tu kichwa hasemi kitu, nikaona hapa napoteza muda nikamuaga nikimwambia she should be ashamed of herself.

Baada ya siku mbili alinitafuta akaniomba tuonane mahali, sikua na haja ya kukataa. Tulikutana moja ya fukwe za kigamboni, baada ya kufika, tumekaa muda wala hasemi kitu. Nikataka kuondoka, akanizuia…

Ann mwanangu, najua ushakua mtu mzima sasa unaelewa kuhusu hisia za mapenzi, mimi na Paul tumependana kwa muda mrefu, na usione kama najitetea ujinga ila I really love him, he is my first man na sina haja ya kuwa na mwanaume mwingine. Nawaza kila siku kuhusu my future, ila I don’t see it without him….”

sijui nikueleze vipi uelewe, maana najua kama mtoto unamfikiria mama yako Zaidi, lakini believe me, I love your mom too, I respect her Zaidi ya rafiki ni kama dada yangu. Ingekua simuheshimu ungeshaona Ann, ila haitatokea kumvunjia heshima hata siku moja…. Mara nyingi nimekua upande wa mama yako hata pale Paul anapokua kinyume nae, sometimes Paul anataka kulala kwangu lakini mm ndo nimekua namgombeza na kumwambia aheshimu mkewe….”

“Najua ni ngumu kueleweka bt please usinihukumu kwa kushindwa kuzuia hisia zangu”


nikadakia, “sawa, lakini huoni unasaliti urafiki wenu, amekua best friend kwako and ulichoona ni kumchukulia mmewe, of all the men duniani ndo ukaamua kufall kwa Paul (nikajikuta na mm natumia jina la kwanza la mzee)”

Judy akaniangalia then akasema, “so unataka nifanyeje Ann, ndo nishajikuta this deep, ingekua mwanzoni mwanzoni labda ningeweza, bt mm na mama yako tumejikuta urafiki wetu unazama sana baada ya mm pia kuwa nishazama sana kwa paul, what should I do?”

jibu lilikua ni moja tu, “chagua moja Judy, be with my dad or be with my mom, you can’t have it both ways”…….

Judy akafikiria kama dkk tano nzima, then kikaona kafunika uso wake kwa mikono akaanza kulia tena, huku akisema kwa kurudiarudia “I cant, I cant, I cant………”

nikaona hapa natwanga maji kwnye kinu.

So guys, najua siwezi tenganisha mahusiano ya Dad na Judy, bt atleast mnaweza nishauri namna ya kumuweka Judy mbali na mama…. How do I do this?
 
This is one of the things where you say GOD knows better,
According to your narrations, Judy is genuine and let this be. Just get the confirmations of Judy that she will never con your mother. On the other end, let your mother knows is not wise to mix business with friendship, and if it is a must then she should play safe on every stage of this investment.
 
Jiweke mbali na hili jambo, na kwasisi wababa tumeziwea kusema kwamba watoto wetu wa kike wanatuonea wivu Kama wake zetu.

Na huwezi jua yamkini mama yako anatambua uhusiano wa baba yako na Judy, lakini ameamu kukausha for some reasons.

Basi tuchukulie hajui, je hauoni kama ukimwambia mama anaweza pata mshtuko mkubwa ambao utaweza kuleta madhara..??

Okay, let's say mama hajui... Wewe lengo lako hasa ni nini kitokee baada ya kumwambia mama..??

And, utajiskiaje ikiwa utamwambia mama na kisha hili jambo likaleta ugomvi mkubwa hata kupelekea kuvunjika kwa ndoa ya baba na mama yako..??
 
Stori yako nzuri kweli.. nikuambie kitu kimoja tu ukikuta maji yametulia yawache hivyohivyo! Usikute na mama yako anajua ila kaamua tu kufunika kombe mwanaharamu apite!.. ninayo mengi yakuandika huyo bi mdogo umepata wa faida but anyway jukumu la kuyakoroga yapo juu yako na kuyanywa pia yapo juu yako.
 
Omba toba juu yako,juu ya Baba yako,juu ya mama yako,juu ya Judy mama yako mdogo. Kwa kile kilichosababisha baba yako akamuacha mama yako tubu, Ingia maombi ya kuwatenganisha kwa jina LA Yesu aliehai kwa kuwataja majina yao. Hakikisha unajua kusali na unasali kwa imani. Haichukui Muda wanachofanya ni wanastail mauti na wamekwisha kufa katika ulimwengu wa kiroho ni wafu wanaozikana. Mpe Yesu wataachana tu hiyo ni roho ya zinaa kwa msaada wa maombi japo utaomba wewe 0767451444 na kama we we ni mwislamu sifahamu sasa jinsi ya kutatua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom