Nimrod Mkono ajitangazia ubunge maisha!Butiama kuwa kama washington DC!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
mbunge fisadi nimrod mkono amejitangazia kuwa mbunge wa maisha musoma vijijini pia ameahidi butiama kuwa kama wash dc
 
Mkuu naomba ufafanuzi! Kayasema hayo wapi? Kwenye tukio gani mkutano/warsha/harambee? Ukijibu hayo yatafuata haya hapa chini...... Kwahiyo hakutakuwa na uchaguzi au hakutakuwa na wagombea wa vyama vingine?
 
Sina uhakika na maneno yako.

Ila namkubali huyo mzee kwa juhuhdi anazofanya kuendeleza jimbo lake. Magamba wote wangekuwa kama huyo mzee tungekuwa mbali sana
 
Sidhani kama ni kweli , labda haya magazeti uchwara yamemnukuu vibaya

ni kweli kasema!!,yani aisee madikteta yapo hadi majimboni?Watz tumekwisha,eti wanasema kuna utawala bora na demokrasia ndo hv?Kazi ipo.
 
ni kweli kasema!!,yani aisee madikteta yapo hadi majimboni?Watz tumekwisha,eti wanasema kuna utawala bora na demokrasia ndo hv?Kazi ipo.
Mkuu Jero ili kuweza.kuchangia kwa uzuri zaidi itabidi kesho.atoe kauli kuthibitisha ama kukanusha , kwa maana hiki ni kituko cha karne
 
Acha aijenge musoma anawarudishia watanzania alichowaibia bila kujijua akimaliza tu mungu ataichukua roho yake kwenda kumhukumu, always huwa nasema majibu ni hapa hapa duniani, hii akili ya kizee sasa inaanza kurudisha mali za watu.
 
Katika wabunge wanaojenga ushawishi kwa wananchi wake huyu mzee anajitahidi kiasi chake. Ila wakati tulionao ni lazima mabadiliko yafanyike hakuna jinsi. 2015 for Peoples Power!
 
Katika wabunge wanaojenga ushawishi kwa wananchi wake huyu mzee anajitahidi kiasi chake. Ila wakati tulionao ni lazima mabadiliko yafanyike hakuna jinsi. 2015 for Peoples Power!
Peoples Power maana yake ni nini mkuu naomba unielimishe
 
Ila namkubali huyo mzee kwa juhuhdi anazofanya kuendeleza jimbo lake. Magamba wote wangekuwa kama huyo mzee tungekuwa mbali sana

Hii falsafa nashindwa kuielewa, mbunge kutumia hela na rasilimali zake binafsi kuendeleza jimbo lake! Maanake ni nini? Inajenga picha gani kwa baadaye? Yaani ni kwamba hata kama alikuwa ni mwizi, akizitumia hela za wizi kuendeleza jimbo lake, basi madhambi yake yote husamehewa, sawa? Je siku ama yeye, au wanawe au hata vitukuu vyake vitakapodai vya kwao, jamii itapata wapi ujasiri wa kuwakatalia?

Naambiwa na yule mbunge wa Rorya, Kihiyo Lameck Airo, naye sasa baada ya kutumia hela zake binafsi kutengeneza barabara, sasa anaanza kukubalika jimboni Rorya! Hakuna tena mzalendo anayeulizia chanzo cha utajiri wake! Hapa sasa tunajenga taifa la namna gani? CCM inatupeleka wapi? Hata jizi Mkapa haoni tena aibu kusimama mbele ya wananchi na kutamba, sasa kwa nini Lowassa yeye anapigiwa kelele?

Kwa nini Chenge apigiwe kelele na hela anazo za kusafisha jina lake? Anachohitaji si ni kuigeuza tu Bariadi iwe kama Bandar Seri Begawan, Brunei? Je, kama CCM imeamua nchi iongozwe na wezi mradi wanatuletea maendeleo, kwa nini wanahangaika kuvuana magamba? Tunachosahau wananchi, ni kwamba hawa jamaa ni wafanya biashara na wanawekeza tu, tusipoangalia tutajikuta wengi ni watwana tu ndani ya taifa letu, thanks to CCM!
 
Masikini watanzania wanaendelea kupigwa kamba mpaka basi, wanasiasa wanatakiwa kuwa facilitator tu wa kuhamasisha maendele ili wananchi wapewe fursa ya kujiletea maendeleo wenyewe mtu mmoja kusema atageuza butiama washington mbona haiwezeekani na umri wa mzee mbona kama anakaribia kustaafu jamani.

Wanasiasa na media zao wanaendelea kututawala tena bora utawala wa kikoloni ulikuwa kuna uwekezaji hawa wa sasa hivi no nouma wao matumbo yao, vimada vyao na jamii zao tu. Kama kweli anaweza kugeuza butima kuwa DC mbona yuko huko kitambo au ikifika 2200 wakati na yeye hayupo?

May be miss quote manake media bongo ina viazi vingi sana.
 
Licha ya kutowapenda Magamba na licha ya kwamba watu wa Mkoa wa Mara wana damu ya kimageuzi kiasilia na licha ya kwamba jimbo hilo lilishawahi kuchuliwa na NCCR Mageuzi na Mbunge akawa Balozi Paul Ndobho, lakini kwa hakika kwa sasa hakuna mwenye uwezo wala ushawishi wa kumng'oa Nimrod Mkono katika jimbo lile. Huu ndio ukweli mchungu mnapaswa kuufahamu.
Nimrodi Mkono ndiyo Mbunge bora kabisa kuwahi kupatikana katika jimbo la Musoma vijijini. PERIOD.
 
Probably ndie mbunge bora kabisa kuwa kutokea
 
Back
Top Bottom