Nimewaona leo LIVE

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Leo nimeshuhudia kitu ambacho kwa miaka mingi nilikuwa nasimuliwa tu. Mbunge wa jimbo la Tunduru kusini-Eng. Ramo Makani(CCM) ambaye alikuwa "mwenyekiti kamati ya Jairo" anafanya mkutano wake sasa. Cha ajabu mkutano umefurika akinamama, watoto na wazee, na vijana wachache sana. Malori ya kubeba mchanga yanaendelea kusomba akina mama kupeleka eneo la mkutano (maarufu kama baraza la IDI) muda huu hapa mjini Tunduru. Kubwa zaidi leo ni sherehe ya vijana wakodisha pikipiki(boda boda) kwani pikipiki karibu mia mbili zimenyweshwa mafuta na CHAMA CHA MAPINDUZI huku wakipewa pesa (10,000) kila dereva pikipiki.................MHESHIMIWA KAPIGWA SWALI "kwa nini tangu 31 octoba mwaka jana hajaja?". Mheshimiwa kajitetea kuwa haina haja ya kuja ila yeye atakaa Dar es salaam tu anahangaika mawizarani kutafuta "MISAADA". Sijui misaada gani.
 
Mkuu mbona usomeki...ebu kajipange upya! Na data zako za vijiweni
 
tunataka posho ziongezwe kutoka 70,000 kwa sikuhadi 200,000..wapiga kura wanatuomba sana tunapokuwa dodoma:mizengo pinda etal
 
Afadhali wabunge wa CCM wanajua kurudisha fadhila! Hebu tuambieni hizo za wabunge wa CDM huwa zinaenda wapi?
 
Kuna watu tukikuta mpo na mchangia wengine tunakata tamaa,maana tunajua ni maudhi matupu sasa haya ya kulinganisha posho zinakwenda wapi yamekujaje tena?ngoja nihame tu kwanza
 
Kila goti litapigwa.uki jua ya mwenzako ujue ya kwako yatajulikana tu.mimi nadhani ndugu zangu wa JF tungekuwa tunavumiliana kwa hoja zinazotolewa humu,mi naiman kama JF ikitumika vizuri itakuwa sehemu nzuri ya kujenga bongo zetu kwa kupata habari zenye mchujo wa hali ya juu,lakini pia kujua mambo mengi ya nchi yetu na dunia nzima,maneno ya kuudhi,kukashifu,kudharau hoja ya mwenzako isifikiriwe kuwa ni njia nzuri ya kutetea kile unachokiamini inawezekana kabisa ukawa ni mmoja kati ya watu wanaharibu mtazamo wa chama chako,itikadi yako,dini yako nk,nakusikia mtu anasema hawa watu wanatoa kauli hizi mbaya ni wapenzi wa chama a nk.tuvumiliane jaman JF si mahala pa kujifunzia hoja za kuudhi,Na ukweli kama ingekuwa lazima kuandika jina lako ni lazima haya yote tunayo yashuhudia humu yasinge tokea.watu wengi wa muhimu wamejitoa ktk JF kwa kuepuka matusi na maneno ya kudhi.iko siku utapatikana mtandao wa waastarabu hamtapa nafasi ya kutoa maneno ya aina yenu hii WHY THINKER's muwe hivyo tubadili kwanza sisi watanzania ndiyo kila kitu kitabadilika taifa la aina ya watu waina hii halitashinda hata kwa vita ya mbu.tubadilike.ahsante.nadhan mmenielewa
 
vitu kama ivyo vya kunyweshwa mafuta kwa vyombo vya moto huwa ni kawaida sana kwa wanaccm hasa kipindi cha kampeni sijui ndugu yangu unashangaa nini! au kuna kingine umeshuhudia hujatuambia vizuri? ila ni kawaida wanamapinduzi kunywesha mafuta na kufata watu kutoka vijiji vya mbali kuja kujazilia kwenye mkutano! KIGUMU CHAMA CHA MAPUMZI!
 
Hiyo ni fadhila eti, unawadanganya watu kwa peremende ili uendelee kushika mamlaka, Asante Lowasa kwa shule za Kata maana nimesoma hizo na nitarudi kijiji kuielimisha jamii yangu juu ya uraia, na ndipo CCM na ufisadi waoa watatambua 2015. Tuombeane uzima.
Afadhali wabunge wa CCM wanajua kurudisha fadhila! Hebu tuambieni hizo za wabunge wa CDM huwa zinaenda wapi?
 
Afadhali wabunge wa CCM wanajua kurudisha fadhila! Hebu tuambieni hizo za wabunge wa CDM huwa zinaenda wapi?
Huwa unaniudhi sana wewe, wewe kila mtu anayeuzungumza moyo wake unamrushia uanachadema.
 
nimeamini ni heri ya mjinga ajijuaye yu mjinga kuliko mjinga asiyejijua. Pole sana.

Mkuu Mk endelea kutupa updates kuhusu Ramo Makani. Tunajua hakubaliki Tunduru Kaskzni. Achana na hao akina Rejao na Wakusoma. Kwanza ww wa Kusoma si umetuambia uko unatuletea updates ndani ya Mkutano wa Nccr mageuzi. Sasa Tunduru na ww wapi na wapi?
 
Afadhali wabunge wa CCM wanajua kurudisha fadhila! Hebu tuambieni hizo za wabunge wa CDM huwa zinaenda wapi?

Kwa hiyo ulitaka wabunge wa CDM nao wafanye upuuzi kama huu? Kweli Rejao ni Mpuuzi!
 
Back
Top Bottom