Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Mwambie huyo mchumba wako kuwa maisha ya Arusha yamekuchosha hivyo ungependa mkatafute maisha Lindi au Mtwara ili kuwa mbali na hao rafiki zako.
niko tayari nikawe mkulima wa jembe la mkono MTWARA ikiwa jamaa atakubali tuhame ARUSHA
UGUMU ni kwamba jamaa ame-base kimaisha ARUSHA kwa maana hata wazazi na wadogo zake wako AR
 
Sasa ukitaka hayo nyamaza kufa na yako moyoni ukisema tu ndoa hataiona na ukiiona utaiona chungu
MIMI kunyamaza naweza ila hawa wadada wa KIKENYA wanavyofurika Tz na nimejiuza nao ndio napowazia itakuwaje maana najua ipo siku watavujisha
 
ndo hvyo hvyo maana hao wapo na wataendelea kuwepo
ye afanyr yake tu
kimya kimya uchangudoa kitu gani bwana wee

Hajui watu wanaolewa na wana watoto wa4 na bado mume anafichwaa hhhhhhhaaaa,hajui ndoa za mahesabu siku hizi
 
MIMI kunyamaza naweza ila hawa wadada wa KIKENYA wanavyofurika Tz na nimejiuza nao ndio napowazia itakuwaje maana najua ipo siku watavujisha

Marafiki tu mbona mi hawanizishii je hiyo siri wangekua nayo mawifi zako ingekuajeee ,mama yako umemuuliza kasemajee
 
huyu uchangu bado uko kichwani make inaonyesha machangu hawana siri nadhani kwa sababu ya mazingira ya kazi yenyewe.

Ingekua amemsaliti hapo lazima roho imsutee lakin mambo ya zamani haina umyhimu kusemaa bana,ye kafichwa mangapii au akiona watu wamenyamaza anajua wapo safi
 
Inaonekana umelea kovu ambalo ni Vigumu kufutika moyoni kwasababu ulifanya hiyo kazi kutokana na hali iliyokuwepo.....kwangu mimi naona ni bora utoboe ukweli kwanza kuiweka nafsi na moyo wako huru...pia naamini kwa jinsi ulivyo sasa hivi kiimani na mafanikio(elimu) sio Vigumu kwa mtu anaekupenda kushindwa kuendelea kukuamin
kuna wakati haya mawazo yako yananijia akilini ila mama mzazi alishaniambia bora nife na uongoo wangu kuliko kusema

pls ingelikuwa ungeendelea kuniamini au hata kunioa baada ya kujua uchangudoa wangu wa NAIROBI???
 
Ukweli uliwazi ni kwamba hakuna siri ya wawili. Na wewe siri yako ni ya watu zaidi ya wawili. So jua ya kwamba huyo yero Masai atajua tu siku moja na hutakuwa na jibu LA maana LA kumpa itakuwa too late na atakuacha. Ushauri wangu ni kuwa umerudia Mungu then jua atakuwa upande wako hatakuacha uaibike wewe mwambie jamaa akiamua kusuka haya akiamua kunyoa poa!! But utakuwa huru kabisa na utapata MTU bora utashangaa mwenyewe!! Coz hayo yote yalikuwa ni Mapito tu ya Dunia
 
oky now umeshaacha huo uchanguuu au bado badooo na unafanta issue gani?
NILIFANYA uchangudoa miaka mitatu na nusu, mama alipotoka gerezani nkaachana na uchangudoa na tulirudi TANZANIA arusha na kuanza makazi mapya.
 
Ukimuambia hayo sasa utamkatisha tamaa ,ukiwasogeza hao rafiki zako ndoa utaiona kwe TBC kwenye chereko

so...which is which shosti...nateseka sana yaan utoto wangu taabu na hata ujana nao nateswa na ya utotoni
 
Ushauri wangu: Kuishi maisha mazuri na ya huru SIYO LAZIMA uolewe! Kama kisa chako ni kweli tupu, basi mungu wako na awe shahidi yako, uishi maisha ya single. Mbona ndoa nyingi ni fadhaa tu?
 
Wana ushahidi gani ??? Hata wakimuambia aamin? Kua karibu nao hao ndio watakufanya usiishi kwa amani rafiki tu uanshindwa kuwachenga kutokua nao karibu
understand!!jamaa nampenda sana sina ukakamavu wa kumbishia ikiwa ataniuliza
nimetembea na wanaume mamia haiingii akilini kama atanielewa
 
Ninachoona hapa ni hofu ya mleta mada kuvujishiwa habari za ukahaba wake na hao wakenya tu hakuna cha zaidi hapa ndio maana aliamua kuhama kanisa kwa sababu tu ya kujiweka mbali na hao watu anaodhani wanaweza kufichua mienendo yake ya nyuma.
Hapa suluhisho lipo ila ni la ki-intelligence zaidi na kucheza na akili za hao wakenya na huyo mmasai.
 
Back
Top Bottom