Nimeufunga mwaka 2022 kwa kupokea zawadi nzuri na tamu kutoka kwa Zitto Zuberi Kabwe. Mitandao ya kijamii itumiwe vyema

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Nianze Kwa kuusema ukweli, Nimewai kupata zawadi nyingi sana Mosi ni uhai kutoka Kwa Mwenyezi Mungu.

Pili ni zawadi ya Elimu kutoka msingi mpaka Chuo kikuu namshukuru sana Mama yangu Mzazi.

Zawadi ya Tatu ni penzi Tamu kutoka kwa Mke wangu mpenzi (likivurugika naweza kuwa mwehu Bure).

Zawadi ya Nne nimeipokea Leo Kutoka kwa mtu ambaye sikuwai fikiria kamwe anaweza fanya jambo la namna hii Huyu SI mwingine ni Ndugu Ta Mwami Zitto Zuber Kabwe.

Zawadi yenyewe ni kitabu kizuri sana na Cha gharama ya Hali ya juu sana ambacho Kwa kuwa mwazi ni Watanzania wachache wanaweza nunua kitabu hiki.

Jina la kitabu ni "38 Reflections on Mwalimu Nyerere".

Nina fahamu kabisa Kwa kizazi chetu hama Cha Leo kikisikia nimepewa zawadi ya namna hii kitalalamika, maana kizazi Cha Leo ni Cha wale walikusanyika kwenye ziara za Mwendazake na kuishia kurushiwa marobota ya Pesa wakidhani wamesaidiwa kumbe looooo!hata Mungu alichukizwa na hili la kujikusanyia pesa Ikulu kuzitoa kwenye mizunguko, na kuzigeuza fedha zote Mali ya mtu mmoja na kuishia kuwarushia watu barabarani mithili ya kuku warushiwao mahindi.

Naomba awali ya mengi nimshukuru Kiongozi wa chama Cha Act Wazarendo, ndugu Ta Mwami Zitto Zuberi Kabwe Kwa zawadi hii,''popote ulipo ndugu yangu Ta Mwami,Mimi kijana wako unae nitambua Kwa jina Kifimbo cheza kwenye ukurasa wa Tweeter,ninakushukuru sana Kwa kukuomba zawadi ya kitabu hiki na wewe bira ya hiyana ulielekeza uongozi wa Duka la Mkuki na Nyota wanipe kitabu hicho Kwa bill ya Yako ya 70,000 hii SI pesa ndogo ni pesa kubwa sana Nina kushukuru mkuu wangu,Nimekabidhiwa kitabu changu na mdada mzuri na mrembo ambaye ni mtumishi wa Duka la Mkuki na Nyota kutoka idara digital kama sikosei, nashukuru sana mkuu.

Wapo watakao fananisha tukio Ili na pengine siasa niseme kweli kutoka moyoni mie ni mfuasi wako ila sio mwanachama wa chama chako, it's matter of time wakati wa bwana ukifika tunaweza tembea juu ya maji yenye rangi moja.

Funzo Kwa vijana wa kitanzania, vitabu vizuri kama hiki Tanzania hasa chama tawala na serikali yake haitaki visomwe na kizazi chetu,taarifa kama hizi imezigeuza nyara za serikali, ni vyema tukatumia mitamdao ya kijamii vizuri kuwasiliana na wadau kama Hawa Ili tupate madini ya namna hii.

Narudia Tena hakuna mwanasiasa yoyote aliye tayari kutoa zawadi za namna hii Kwa kizazi chetu mi nimemwona Ta Mwami Zitto Zuberi Kabwe, Sina cha kukulipa Mgurusi Mungu abariki kazi ya Mikono Yako abariki ulipo toa pawe hivyo milele na milele.

Popote ulipo nakutakia kheri ya Mwaka mpya Ta Mgurusi! Waitu kasinge.
 
Kama mliwasiliana huko Twitter na ukapewa ofa huko mbona tena umekuja huku?Si ilikuwa umshukuru hukohuko tena Inbox au Lengo ni nini?
 
Back
Top Bottom