haszu
JF-Expert Member
- Oct 10, 2017
- 837
- 1,550
Ni jambo lenye ukakasi ila sinabudi kulizungumza. Naomba mniwie radhi.
Nilisafiri sehemu nikakaa siku moja, yapili nikarudi, naweza sema nimekaa siku mbili, lakini zaidi ya haja dogo, sijaenda haja kubwa hata maramoja.
Niliporudi ninapoishi siku ya kwanza nikapata choo kigumu, siku ya pili ndo ikawa shida zaidi, choo kigumu sana na hakitoki, nikajikamua sana na kwa nguvu kweli kikatoka kilichotoka lakini nikawa najihisi kama kuna kitu kigumu kimekwama karibu na kutoka.
Nilipoamka asubuhi, bado hali ya kuhisi kitu kimekwama ikawa ipo, nilipoenda uani nikapata haja ya kawaida bila shida ila ile hali ya kitu kukwama ikaendelea kuepo.
Niliamua kujikamua tena, nilihisi maumivu kwa mbali, nikaona sinajinsi nikajiangalia, ndio nikaona kuna kiuvimbe kwa nje, kma kijipu.
Naomba kufahamu
1. Huu uvimbe unatokana na ugumu wa kile kilichofanikiwa kutoka kwa sababu nilijikamua sana?
Au
2. Huu uvimbe ni Bawaziri ndiyo imekuja ghafla?
Kuna aliyewahi tokewa na hii hali? Nifanyeje?