dadamlamayao
JF-Expert Member
- Nov 1, 2022
- 242
- 806
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, nililipia Tsh.183,000 tarehe 3 Novemba mwaka huu kama malipo ya awali ili wanifungie Sola ya Watt 120 hapa nyumbani kwetu Simiyu.
Leo ni tarehe 5 Disemba maana yake zimeshapita siku 32 hawajaja kunifungia na jitihada za kuwaambia wanirudishie pesa yangu zimeshindikana. Nimeenda kuripoti Kituo cha Polisi wameniambia hiyo ni Kesi ya Madai na si Jinai, naomba msaada mwenye uzoefu na hii Kampuni.
Na pia nawatahadharisha Watanzania wenzangu hasa waliyo vijijini ambako umeme bado haujafika, wajihadhari na kuigopa kampuni hii kwani ni matapeli makubwa kama ilivyo Kalyanda tu.