Mysol engie kampuni ya sola ya kitapeli na kijambazi, serikali chukueni hatua

natukundamuk

Member
Jul 28, 2022
50
267
Wapendwa wana Jamii Forums,

Niliingia Mkataba na kampuni ya sola ya Engie Mysol ambayo zamani ilikuwa ikiitwa MOBISOL wanifungie Sola ya watt 200 nyumbani kwangu Biharamulo ili watoto wangu waweze kusoma vizuri kwani bado hatujapata umeme wa TANESCO.

Cha kushangaza nimeshalipia malipo ya awali ya shilingi 285,000 lakini leo ni siku ya 27 hawajaja kunifungia. Tafadhali msaada kwa aliyewahi kupata huduma za hii kampuni maana naona ni kama MATAPELI hivi. Nisije nikaenda na shoka ofisini kwao na kumwaga damu maana 285,000 maisha magumu usawa huu.

MSAADA TAFADHALI
 
mimi nililipia nikaondoka nao mguu kwa mguu kwa usafiri wangu wakanifungia na nimemaliza mkataba na mtambo wao umekufa BAADA YA MIAKA MITANO
 
Back
Top Bottom