Nimepigwa vibao na mke wa jirani yangu kwenye kituo cha basi.

pole sana nadhani ungempiga vibao na wewe kidogo ili akome tabia za kupiga wanaume wazima barabarani kha hana adabu kabisa hata ingekuwa kweli sio sawa kukupiga, anyway wanawake tunaweza kama vipi wanaume muanze na nyie kutafuta haki zenu, kama wewe umepigwa mme wake ana hali gani huko nyumbani?
 
sina la kusema, nisije kukosoa kazi za muumba
 
Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

Kwa ulivyokuwa mstaarabu kwa huyo dada, subiri tu simu ya" kaka naomba tuonane" kutoka kwa huyo dada na hasa kwa kuwa anaamini mumewe ni kicheche na hivyo huenda akafikiria kulipiza kisasi. Na mtu wa kulipiza nae kisasi uwezekanao mkubwa utachaguliwa wewe upozwe MAKOFI kwa MASHAVU . Wanawake bana!
 
duh,kumbe Buji ujanja wa JF tu?hahahaha,ungemfyatua mitama kaka othrwis tuhuma za kweli
 
Buji nilifikiri ni mjanja kiivo ka huyo mnigreia wako kwenye hyo avtr
 
Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

M2 wangu uamuzi uliofanya nakupa TANO big up nadhani umekamilisha msemo usemao dawa ya moto ni maji, maana na wewe ungejifanya ni moto nadhani hapo----------------na pia umeepusha mengi sana najua.
 
Back
Top Bottom