Nimepewa Risiti lakini sijazielewa

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,928
2,006
Nimeamua kuja hapa mnazi mmoja hospital inayosifiwa na wakazi wengi wa dar kutokana na huduma zao kuwa bora kuliko hospital nyengine mwananyamala,temeke,na amana.

Kama utaratibu ulivyo inakubidi kununua kadi ya kwenda nayo kwa mganga na bei yake ni shilingi 2000 taslimu za kibongo.Nimelipa na nikapewa kadi ya njano ILIYOBANWA NA RISITI MBILI NYUMA ILIYOANDIKWA MALIPO YA KUCHANGIA HUDUMA YA AFYA.

Tatizo sio elfu mbili niloitoa,tatizo langu nikiwa kama great thinker nahitaji MAELEZO kwanini sikupewa risiti moja ya elfu mbili nikapewa risiti ya aina moja yani za elfu moja moja tena zilizo sawa hapa ndipo napohitaji ufafanuzi wakuu toka kwenu,kama jambo hili ni sawa.

Najiuliza kama hizi risiti ni za mifuko miwili tofauti kwanini nipewe risiti hizi za aina moja.Wakuu nawatakia jumamosi njema,na mnapomuombea rais wetu afya yake itengamae msinisahau na mimi pia.
 
Mkuu kaulize huko huko ulikopewa hizo receipt ili wakueleweshe vizuri kwani ni kwa nia njema ya kutaka kufahamu zaidi, vinginevyo hapa tukianza kulijadili hatutapata majibu ambayo ni guinine, otherwise itakuwa ni umbea tunafanya. Nenda kaulize hivi, vipi mmemkosea kunipa hzi receipt mbili ama ni kwa sababu gani kuchukua receipt mbili tofauti wakati nimelipia huduma moja??? Or you can create tricky questioures list so that to get your desired intessions answers,
Its my opinions tusubiri wadau wengine tuwasikie wanasemaje!
 
nimeshaondoka maeneo yale mkuu,hapa jamvini kuna wadau wanaoweza kuwa na majibu ya swali langu
 
Inawezekana gharama halisi ya huduma uliyopewa ni 1000/=, na elfu ya pili ni mradi mtu.
Kwa maana hiyo kuna kitabu original na feki.

Ni mtazamo tu.
 
Mkuu hujawahi kumlipia ada mwanao au ndugu kwenye shule za kata? A/C lazima ziwe mbili, ada 20,000/= ina A/C yake ,michango ya majengo, uniform, chakula na kero zote zinazoitwa michango zinafika 300,000/= ina A/C yake na huruhusiwi kuhoji. Hii nchi ukitaka kuishi maisha marefu timiza malengo yako ukifuatilia yanayoendelea utaishia ugonjwa wa moyo na matibabu utaendelea kuyapata kwa kupokea hizo risiti mbili mbili.
 
Kuhusu hilo la a/c 2 shule 1. niliuliza wakanambia ni majukumu tofauti.Hospitali ya Tumbi kwa risiti walikuwa wanapata laki 6 kwa siku.Baada ya kuanza mfumo wa mtandao wanapata milioni 3 kwa siku.
 
Hapo hakuna tatizo ndugu yangu. In short wanaweza wasiwe na risiti za 2,000/= na badala yake ukapewa risiti mbili za elfu moja ambazo thamani yake ni sawa. Ila ukilipa elfu 2 halafu ukapewa risiti moja tu ya elfu 1 hapo wizi umefanyika. Ugua pole
 
Hizo risiti ziko printed kwenye vijitabu na wamesha-andika na kiasi. Nafikiri hapakuwa na risiti zenye denomination ya 2,000 so namna nyepesi ni kukupa mbili zenye buku buku maana ndio zilizopo. Na ndio maana zinafanana
 
Back
Top Bottom