Nimepata kazi ya mkataba ila nilikuwa na uhitaji wa kazi ya kudumu

unaacha hizo halafu unakosa na hizo unazozingoja😂, kazi zilivo za shida ivi wenzio tunatafuta hata za kufanya kwa mwezi mmoja hatuzioni😅 Shauri yako
kuna bint kakakataa kaz mshahara lak 680 nje ya nchi huku anapewa kila kitu na mshahara haukatwi kodi na kazi masaa 8 kwa kusubiria kazi asiyoijua ni lini ya uweitres..ss ukiangalia muonekano wa huo uweitres hana na wala hana uhakika na hiyo kazi. Basi namuangalia najionea kilaza kimoja.
 
Habari wana jf.

Mimi ni kijana niliyekuwa nahangaika kutafuta ajira serikalini kwa muda mrefu kidogo.

Juzi ijumaa Tamisemi wametoa majina ya ajira ila kwa muundo wa mkataba na jina langu likiwemo.
Ila imeniletea ukakasi hii hali naombeni ushauri wenu wakuu.

Ajira wanasema ni ya mkataba wa miaka miwili na utapata shtahiki zote za mtumishi wa umma na majina yametolewa na Tamisemi wenyewe.

Mimi nataka niipotezee maana kuna kibali cha ajira mama samia alishakitoa mwaka jana Nadhani mwaka huu wanatangaza watumishi elfu 23.

Hofu yangu

Kama nikienda kuripoti nadhani sitapata tena ajira za tamisemi zinazotoka mwezi ujao maana Database yao itaonesha nimepata kazi.
View attachment 2886023
Nenda kapige kazi mikataba ijayo itakufuata tu, kwanza CV yako itakuwa imeshiba.
 
Achana na hiyo halaf endelea kukaa mtaani kusubiri ya kudumu.!!!.

Vijana siku hizi sijui mnafikiriaje!! Unakosa jibu kabisa ukitafakari.

Iache mkuu. Haitakusaidia.
Unapokuwa mdogo na huna majukumu. Unaona bado una muda mrefuuu wa kufanya yote unayotaka kutimiza, ila ubaya ni katika same space, ukifanya makosa kama anayotaka kufanya kijana, miaka itaenda na hujui imeendaje. Worse enough unajikuta huna lolote na kinachobakia ni kuanza kujutia nafasi ulizopoteza

Mdogo wangu huyu 23 katoka chuo, kama ni wale exceptional and gifted human beings ambao hawategemei interviews zaidi ya simu za kazi kuwatafuta, bhasi aache ila kama ndo wale wa kusubiria interviews

Afanye hiyo kazi hadi apate ile kazi anayoitamani
 
Walio kwenye mkataba hupewa kipaumbele kwenye ajira za kudumu pale zinapopatikana. Hujapoteza kitu na wala usiwaze sana.
Pia mashirika ya kiserikali mengi huwa hayasitishi mkataba kirahisi zaidi ya kuiongeza miaka na miaka.

Namuelewa kwa sababu hana experience sana ya mtaa kwa hiyo watu wampe ushauri kutokana na level ya mawazo yake.. Japo asitake kupitia tulipopitia kaka zake maana ni vita ya damu na maji 🙏🏽
 
Shida Ajira za kudumu zinatangazwa mwezi ujao.
Una uhakika gani zitatangazwa muda huo?

Unajua hao tamisemi Muda sio mrefu akili yao yote wataipeleka kwenye maandalizi ya Uchaguzi.

Haya mambo ya Ajira wanaweza achana nayo kwanza Kwa muda?

Haya hizo Ajira za Muda unasema mliomba mwezi wa 4, halafu mmepangiwa Leo, unadhani hizo za kudumu mkitangaziwa mwezi ujao, vituo vya kazi vitapangwa mwaka gani.

Wakati hao viongozi watakuwa bize kutafuta asali, na Fedha nyingi ya serikali itaenda huko kwenye uchaguzi mwaka huu na mwakani?
 
Shida Ajira za kudumu zinatangazwa mwezi ujao.
We nenda kuna uwezekano ukapewa mkataba wa kudumu hukohuko kila kitu kinawezekana Unasubiri zitangazwe serikali ikiahirisha utafanyaje. Hakuna kazi ya kudumu hapa duniani afya yako ndiyo itakufanya udumu kazini, je ukiajiriwa kazi ya kudumu halafu ukapata ulemavu wa macho unadhani mwajiri ataendelea na wewe lazima upigwe chini.
 
Habari wana jf.

Mimi ni kijana niliyekuwa nahangaika kutafuta ajira serikalini kwa muda mrefu kidogo.

Juzi ijumaa Tamisemi wametoa majina ya ajira ila kwa muundo wa mkataba na jina langu likiwemo.
Ila imeniletea ukakasi hii hali naombeni ushauri wenu wakuu.

Ajira wanasema ni ya mkataba wa miaka miwili na utapata shtahiki zote za mtumishi wa umma na majina yametolewa na Tamisemi wenyewe.

Mimi nataka niipotezee maana kuna kibali cha ajira mama samia alishakitoa mwaka jana Nadhani mwaka huu wanatangaza watumishi elfu 23.

Hofu yangu

Kama nikienda kuripoti nadhani sitapata tena ajira za tamisemi zinazotoka mwezi ujao maana Database yao itaonesha nimepata kazi.
View attachment 2886023

Vijana mnafeli sana
 
Back
Top Bottom