Nimemtembelea Mjane Wa Daud Mwangosi...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
a1.jpg
Ndugu zangu,


Leo jioni nilifunga safari kwenda kumwona mjane wa marehemu Daud Mwangosi. Anakoishi ni maeneo ya Mwanyingo hapa Iringa.


Mjane amerudi juzi jioni kutoka msibani Tukuyu. Itika, jina la mjane wa marehemu, anawashukuru kutoka ndani ya moyo wake, wale wote waliomchangia na wanaoendelea kumchangia fedha kama pole ya msiba mkubwa uliomkuta. Na wale wote waliokuwa nae katika wakati huu mgumu.


" Mungu ndiye atakayewalipa"- Anasema Itika Mwangosi, mjane wa marehemu.

Amerudi kutoka msibani akiwa hana cha kuanzia. Leo pekee tumefanya jitihada ya ziada kuhakikisha maji hayakatwi kutokana na bili iliyochelewa kulipwa kutokana na msiba wa ghafla wa Daud Mwangosi . Kutokana na michango yenu, kesho Jumatatu familia italipa deni la maji lisilozidi shilingi laki moja na nusu.


Nilichokiona kwa mjane wa Daud Mwangosi ni uhalisia wa hali aliyo nayo sasa. Anafikiria jinsi atakavyomudu kuishi na kuitunza familia. Alifarijika sana aliposikia amechangiwa kiasi cha fedha kinachozidi shilingi milioni tano hadi sasa. Anaamini, kuwa ataweza kupata pa kuanzia ikiwamo kutumia ofisi ya marehemu Mwangosi kwa shughuli za biashara ndogo aliyoifikiria. Anafikiri pia kufuga kuku, maana nyumba anayoishi ina eneo kubwa.


Na katika kumsaidia kumwongoza kwenye shughuli hizi za ujasiri amali, Mama Mfugale, mmoja wa wajasiri amali maarufu hapa Iringa amejitolea kumpa ushauri na kumwelekeza mjane wa marehemu namna ya kwenda mbele. Na katika siku chache zijazo, mjane wa marehemu atafungua akaunti NBC ambapo pia fedha mlizomchangia zitaingizwa humo ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Dada Janet Mwenda Talawa hivi majuzi aliwasiliana nami na alikuja na ushauri wa mjane wa marehemu apewe mafunzo ya ku-edit mikanda ya video ili aweze kuitumia vema studio aliyoachiwa na marehemu mumewe kwa shughuli za namna hiyo. Nilifikisha wazo hilo, na mjane wa marehemu ameonyesha utayari wa kujifunza.

Mwana wa kwanza wa marehemu Mwangosi aitwaye Nehemia, tayari amesharipoti shuleni Malangali, huko anasoma kidato cha nne, anajiandaa na mitihani ya mwisho mwezi Oktoba. Na mtoto Hertsegovina ( Pichani) yeye yuko darasa la saba. Kesho kutwa anaanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

" Usimfikirie sana baba yako kwa sasa, fikiri kuhusu mitihani yako. Hata baba yako alitaka sana msome na mfike mbali"- Itika, mjane wa marehemu Daud anamwambia mwanawe aliyekaa kando yangu.

Naam, kama mzazi, unaingiwa na huzuni kubwa unapomsikia mzazi mwenzako aliyeondokewa ghafla na mwenziwake akiyatamka maneno hayo kwa mwanawe.


Kumsaidia mjane wa marehemu kwa sasa , ni kama hicho kilichofanywa na waliojitolea kutoa senti zao. Ndio, ni michango yenu ndiyo ambayo leo imemwezesha mjane wa marehemu awe na hakika ya kupata maji nyumbani kwake, na ndio itakayomsaidia kupata pa kusimamia kwa kuanzisha biashara, ili asije kukatiwa maji tena, na umeme pia. Na watoto nao wawe na hakika ya mlo wao. Ni matumaini yetu.

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Duh! imenihuzunisha sana hapo Mama anapomwambia kijana wake kuhusu masomo....Ahsante sana kwa kutuhabarisha na pia kwenda kuwaona wafiwa.
 
maggid Mjengwa, ningefikiria zaidi usimamizi wa uanzishaji miradi ya kujikimu mjane huyu ingesimamiwa na wewe uliyeasisi mpango huu. Nisingependekeza mwingine aingilie kati, maana ulimwengu wa leo wataka wenye moyo mkuu katika kutendea haki.
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu Kamanda Kamuhanda na wenzie, hawakuona madhara kama haya wanayosababishia hii familia? Inatia hasira sana.
 
Kila ninapoikumbuka familia hii, machozi yananibubujika, na mara zote huwa najiweka katika nafasi ya watoto hawa na mama yao, kila wanapokutana na polisi, just imagine ni hisia gani wanazopata.Hawa watoto watakuwa na attitude negative sana na mbaya sana kuhusu jeshi la polisi na kwa matatizo yoyote yale watakayokutana nayo, watakuwa wanajisemea mioyoni mwao, "Kama siyo baba yetu kuuawa na Polisi tusingepata matatizo haya". Nina imani hawa watoto kama wangaliweza wangelipiza kisasi siku moja.
 
majjid mjengwa;

vipi hakuna namna yeyote ya kuwafungulia kesi kamanda michael kamuhandaa(iddi amini) na vijana waliochangia kifo chake kwa kipigo na muuaji mwenyewe binafsi niko tayari kuchangia mfuko huo ili kuona haki inatendeka badala ya kuwaachia polisi wenyewe wahakikishe haki inatendeka wakati wao ndio waliosababisha kifo cha mhusika ???
 
nimemuona leo kwenye gazeti la nipashe Dr. Asha Migiro akicheza ngoma nikashangaa sana aliyekuwa naibu katibu wa UN

ni cheo kikubwa sana Leo hii haki za binadamu zinavunjwa hata kutoa tamko hakuna jamani angalau hata kulaani hakuna.

utetezi wa haki za binadamu unaishia Newyork tu. ukitoka kuja Tanzania unakaa kimya kuhusu haki za binadamu wakati

raia wakiuawa bila hatia. waandishi jaribuni kutusaidia kupata maoni yake tukione hicho kigugumizi chake cha kukataa

kumuhudhi jk
 
Ni muhimu sana Ndugu Mjengwa uisaidie hiyo familia kutafuta wakili wa kuwasaidia kufungua kesi ya madai dhidi ya Polisi na Serikali ya Tanzania. They should sue the state (whose agents the Police are,) for at least two billion shillings.

Sidhani watoto wao wataweza kufanya mitihani mwaka huu. Let us be realistic. Itabidi waombewe kuahirisha kwa mwaka mmoja, na wapewe counselling tu kwa sasa
.
 
Mkuu Mjengwa kwanza hongera kwa kutuwakilisha katika familia hii kwa jinsi ya kipekee kabisa. Natamani sana kuona kama kuna mtu yeyote anayeweza kutusaidia kukomesha ukatili huu wa polisi and the only way ni kuwashtaki hawa watu katika mahakama za kimataifa manake hata mahakama zetu zina walakini sana. Ukiangalia video nyingi utaona kiburi cha ajabu toka kwa huyo kamanda wa polisi. Prevention is better than cure, hatujui baada ya Mwangosi wataua nani tena by the name of utii wa sheria katika upande mmoja wa shilingi
 
Mkuu Maggid, shukrani sana kwa kuwafariji wafiwa mama na watoto. Hakika wewe ni mdau makini.
 
Kama tutashindwa kumshitaki au kumlipizia kisasi Kamuhanda na CCM basi tufunge na kumuomba Mungu aingilie kati kutenda haki. Natamani nisikie mmojawao au wote waliohusika hasa wale wa ngazi za juu wamelipuka ima na miwaya au hata ajali au ugonjwa wa moyo ili wake zao na watoto zao nao waonje adha ya ujane na uyatima.
 
Pacificius ona unavyotesa familia isiyo na makosaaaaaaaa!! Askari kabla hamjafanya upumbavu kama mlioufanya kwa mwangosi fikirini kwanza!!!! Msikubali kutumika kipumbavu,wanaharakati tumfatilie huyo pacificius inaweza akawa kama Joshua malundi.
 
Back
Top Bottom