Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Kubali kilichotokea kwanza,pili let it go.. Km wajisikia kulia lia tuu itasaidia kuondoa uchungu na mzigo unaousikia moyoni.. Life is too short don't let anyone still ua happiness. Watu wanakutana na changamoto nyingi ktk maisha ila wanajipa moyo na kusonga mbele. Waweza pia songa mbele... Yupo wa ubavu wako
 
u deserve it na kwa miakali ya kijinga huenda ndugu wako wa damu alihitaji msaada wakohukumsaidia kisa binti
 
kimbelembele chako hicho. kwa hayo majukumu mwenzio alikuchukulia kama mzazi atembeae na binti yake sasa kapata mume.
 
Pole yako - Maishani mwangu sitokuja kumsomesha mwanamke wangu a.k.a mpenzi wangu kamwe.! Mara nyingi ukiwasomesha baadae hukugeuka na wanaenda kuolewa eidha na watumishi wenzao au vibopa au wasomi wenzao.du nakusikitikia bure.
 
Dear brothers and sisters, uchumba sio ndoa. Usimfanyie vitu vya gharama mchumba. Anaweza kuja kuwa mume/mke wa mtu baadae huyo. Ni mke wako ama mme wako ndio unatakiwa kumgharamia kwa akili yako yote na mali zako zote Na nguvu zako zote.
 
Hey... Pole mkuu. Hayo ndio maisha, na hayo ndio mapenzi. Najua kuwa amekuumiza lakini haikuwepo uradhimu wa kumpeleka mahakamani. Hiyo kesi ifute, sahau, Cheka na endelea na maisha. Ni vitu vya kawaida hivyo hata visikuumize kichwa. Binadamu wote duniani hapa tunapita. Siku ukija kujua dhumuni la sie kuumbwa na kuishi hapa duniani, basi utaanza kuwaelewa binadamu wote mazuri na mapungufu yao. Samehe, Cheka na jaribu kusambaza upendo kwa kadri uwezavyo. Ndio ushauri wangu huo
 
Mimi niliwahi kuumia sana, du kweli mapenzi ysnaumiza!!! Pole ndugu I do remember ila siku hizi nimewadharau sipendi nawapiga mno siku hizi alafu wanaongezeka tu .
Nakushauri upotezeeee tu, kaaa mwaka m1 single accumulate your wealth then utapata mwingine.
 
Pole sana mkaka kwakuingia chaka, ushauri wangu samehe mwachie Mungu malipo hapa hapa duniani iko siku utaleta mlejesho, omba uzima tu fanya maombi utampata akupendaye lakini usifanye haraka kutafuta tulia kwanza pressure ipungue la sivyo utaangukia chaka lingine, nakushauri kama mwanamke ninaye jitambua, hata wanawake huachwa sana anakataa wachumba wengi kisa mchumba anasoma siku isio kuwa na jina mchumba anakuja na mke, piga moyo konde wewe si wakwanza kisasi cha Mungu je! Kama Mungu kuepusha na janga kubwa zaidi ya hilo achana naye piga maombi.
 
Pole aiseee.

Haya mambo ya kuchukia yapo kote kote.

Kuna mtu anakufanyia vituko hadi unawaza huyu shetani au binadamu, lakini unakumbuka mwanzo hakuwa tu binadamu ila malaika mwema kabisa.

Me nawachukia wanaume hakuna mfano ila mwisho wa siku wapo wenye tabia nzuri na wasiobadilika kabisa kutoka malaika binadamu hadi shetani. Hawa wakibadilika saaaaaanaaaaaa wanaishia kwenye ubinadamu
 
Sikujua laiti ningejua.... Najuta

Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani... katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda.. mzuri kisura na kitabia...very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma.

Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa.. na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake.. ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni.

Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua imeingia huko. Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo.. nakumbuka binti alilia yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi kusahau... ilikua best sex ever.

Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa.. Nauli.. hosteli ada matumizi kila kitu ilikua mimi ,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi yanachanua.. likizo naenda likizo zao anakuja.. mama mtu alinishukuru sana. Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga sim naambiwa yuko library.mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo

kufupisha...Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"

Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani. Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafaham. Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na anaishi na mwanaume mwingine. nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu... basi angefanya nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja ya mitaa Dar.. yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake. na kibaya zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio kamchukua binti yake.

Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.. Love is blind inakuwaje sikuona yote hayo?? Why me..Why.. najiuliza sipati majibu. sikuwahi kupenda kama nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye mataa na nyodo juu.. kuna muda natamani ningekua na bastola nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha yake tumbo kule na namba yake nikafuta

NILICHOFANYA

Nimepeleka hii kesi mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo.. kufuta maumivu naona is the least i can do for my self... wakuu nifanyaje au nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu aliyetokea upande wao . Nimetokea kuwachukia wanawake saaaana... kwanini mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.

Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.

Adios.


Wewe ni Mwanamke au Mwanaume? Na ni born town au umetoka Tarime?
 
Nawashangaa sana watu wanajitwika mizigo ya kuwasomesha wanawake wasiokuwa na nasaba nao.....!
Labda tu Unaweza msomesha mkeo wa ndoa lakini eti mtu anaingia gharama kusomesha girlfriend, mchumba au sijui hawara au nyumba ndogo hapo baadae yakija kutokea ya kutokea utamlaumu nani kama si kujilaumu mwenyewe tu...!
Somesha mwanao wa kike au dadako kwani hao hata wakijaolewa ni watu ambao wanakuhusu na hata ikitokea bahati mbaya wameachika au kufiwa na wenzi wao basi hawataweza kunyanyasika au kukusumbua sana kwani watakuwa na elimu ambayo itawasaidia kuwa na kipato...
 
Bahati mbaya Nimechelewa kujua
Relax...jipe muda na amini utasahau tu. Kupelekana mahakamani sizan kama no sulihisho zaidi zaidi unaweza ongeza machungu na ukapoteza tu muda wakom. Ts truly hurt but just believe its never meant for you. Am very sory for you!
 
Wanawake bhana hawana maana sometime ...ingekuwa wao uone wanavyopiga majungu ...Anyway MWALIMU WA WAONGO,WAHUNI,WANAWAKE NA WANAUME NI MMOJA DUNIA NZIMA....Kaka huyo hiyo ndoa yao haina miaka sita maadamu kakusaliti mungu atakulipa, vumilia piga kazi zako forget and move on..
 
Hesabu hiyo kama hasara ktk investment. Kama amekukukera sana na kukuondoa kwenye fomu, kuendeleza kesi kutakupotezea muda, fedha, akili na maendeleo. Hesabu hiyo ni hasara, Muombe Mungu na start another episode. Pole sana lakini
 
Back
Top Bottom