Nimemsikiliza JK Jana; Tafsiri Yangu...

Hivi wemgine wapo ktk sayari ipi?Hivi kutembelewa na Rais wa dunia ni tija?au wa India wakati kenya na uganda wahindi ni kama kwao?Rasilimali hizo zinakwenda.Jikalie tu kaja fulani kaondoka kenge.
 
Ndugu yangu haina ya kugombana. Nikuombe utumie akili yako kidogo kutafakari manaeno machache kati ya menghi ya hotoba ya JK.
Nanukuu:
"Mheshimiwa Spika;
Kwa mujibu wa matamko ya pamoja (Communique) yaliyotolewa baada ya mikutano hiyo, kuna mambo yapatayo manane ya msingi yaliyoamuliwa kufanywa na nchi hizo kwa lengo la kuendeleza utengamano wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
(1)Kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Kampala, Kigali na Bujumbura.
(2)Ujenzi wa Bomba la Mafuta la kutoka Kenya hadi Uganda na Sudani ya Kusini.
(3)Kujenga Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.
(4)Kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutekeleza vipengele vyote;
(5)Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki na kwamba itaundwa Kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho.
(6)Kuharakisha uanzishwaji wa Visa ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Single East African Community Tourist Visa);
(7)Kuandaa utaratibu wa kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao; na
(8)Kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme."

Mwisho wa kunukuu.
Kati ya fursa zote hizo wenzetu wapo tayari ila sisi hatupo tayari, zaidi ukiangalia fursa no.7 utaona udhaifu mkubwa wa serekali yetu, kwani mpaka sasa ukiuliza mchakato wa kutoa vitambulisho vya kiraiya limefikia wapi? jibu ni kitendawili kigumu.
YOU HAVE A LOT TO LEAN

Agreeed!

Tunao viongozi walioishia kula kulala..na kutafuta visingizio na kuomba huruma ili waonekane kama wapo sahihi saana kumbe wanatetea uzembe na uvivu wao wa kufikiri na kwenda kasi kama wengine.

Tunalo tatizo la kudanganyana sana, na Serikali yetu inatumia sana mwanya huo ili wananchi waone kuna juhudi au umakini sana ktk kuingia EAC!.. WAPI?

Ukifuatilia undani ktk 'BIG RESULTS NOW' utagundua ni matokeo ya kuwafanya wananchi wafurahie kisichokuwepo....au wafarijike na hali waliyo nayo..hata kama wote tunapelekwa ktk udhaifu...tubaki kuangalia tu! NO WAY...tunao viongozi wazembe mno..wanatakiwa kutambua kuwa wao ndio kiini cha matatizo yote ya ndani na ktk EAC...!

Kwa Utawala wetu huu..hakuna kiongozi anayeweza kuliambia taifa 'WHERE ARE WE NOW...NA where we want to be in the next 5Years!! Usanii mtupu na kulalama tu kuomba huruma ya umma..!

Nawasilisha!
 
Ndugu yangu mi nadhani unaangalia maslahi ya kwako binafsi zaidi (nahisi unashabikia tu urahisi wa kusafiri ndani ya nchi hizi kwa sababu wewe unasafiri) kama sivyo utaniwia radhi!
Hoja ya msingi hapa ni kwamba Watanzania watanufaikaje na jumuiya hii. Katika vipengele vyote hivi nane hakuna hata kimoja chenye physical impact kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida. Jumuiya hizi zinakuwepo na kupita pia kama ilivyokuwa East African Community ya zamani, angalau tulibakia na mabaki yake hadi leo. Katika hii mpya bado hakuna mahali Tanzania inapoonekana kuwa na base zaidi ya kuwa njia ya kunufaisha wenzetu....KWA HILI HADANGANYIKI MTU HAPA...RAISI YUKO SAHIHI KABISA
 
Kuna tatizo kubwa sana katika negotiation team yetu. Katika mambo hayo nane(8) kuna mambo takribani matatu ni specific kwa baadhi ya nchi, sadly hakuna hata jambo moja specific kwa Tanzania. Hao tunaowatuma huko wanamuwakilisha nani? Wakati wenzao wakichomekea nchi zao katika miradi kama hiyo kwa nini sisi hatuchomekei ya kwetu?

Makubaliano number 1 hadi 3 hayana kabisa linkage na Tanzania, vipi tuyaite ya jumuiya na kuwekwa ndani ya hiyo communique? Angalau hata team yetu ingefanya lobbying ili miji yetu ijumuishwe katika hiyo miradi, nahisi tuliowatuma hawakutimiza wajibu wao hapa. Binafsi naamini kuna tatizo kubwa katika timu ya wawakilishi wetu. Tujitathimini.
 
Nilimsikiliza Rais mwanzo mwisho. Sikuona sababu ya msingi ya kusemea hotuba kama ile bungeni kwa hakuna chochote katika hotuba yake hiyo inahitaji mhilimi wa bunge kufanyia kazi. Sikuona.

Kuhusu masuala ya Jumuiya ya Africa Mashariki, sikuona hoja yoyote ambayo ina mashiko aliyoitoa Rais ya kuonyesha kuwa Tanzania tunatengwa. Katika mambo nane aliyoyazungumzia ni kweli kuwa Rais wa Uganda, Kenya na Rwanda wanayo miradi ambayo ni lazima iwakutanishe kama alivyobainisha Rais Kikwete. Alichomeka tu Rais kuwa kwani wangetushirikisha kungekuwa na shida gani? na mimi nauliza kwa kutokutushirikisha kuna shida gani?

Kimsingi sikuona kuwa Tanzania tumetengwa bali watu wenzetu wanatekeleza wajibu na wanaloona lina manufaa kwao. Kwa hotuba ya Rais Kikwete nimeshawishika kuona hakuna kosa lolote linalotendwa na marais wa Uganda, Kenya na Rwanda.

Kitu ambacho kimenishangaza ni kwa nini Rais Kikwete hakutumia utaratibu wake wa kawaida wa kuhutubia Taifa na kutoa hotuba ile. Ilikwa na umuhimu gani kutolewa bungeni? Sijaona sababu ya msingi hata kidogo kwa hotuba ile kutolwa kwa watunga sheria wa nchi hii.
 
Ndugu yangu haina ya kugombana. Nikuombe utumie akili yako kidogo kutafakari manaeno machache kati ya menghi ya hotoba ya JK.
Nanukuu:
"Mheshimiwa Spika;
Kwa mujibu wa matamko ya pamoja (Communique) yaliyotolewa baada ya mikutano hiyo, kuna mambo yapatayo manane ya msingi yaliyoamuliwa kufanywa na nchi hizo kwa lengo la kuendeleza utengamano wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
(1)Kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Kampala, Kigali na Bujumbura.
(2)Ujenzi wa Bomba la Mafuta la kutoka Kenya hadi Uganda na Sudani ya Kusini.
(3)Kujenga Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.
(4)Kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutekeleza vipengele vyote;
(5)Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki na kwamba itaundwa Kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho.
(6)Kuharakisha uanzishwaji wa Visa ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Single East African Community Tourist Visa);
(7)Kuandaa utaratibu wa kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao; na
(8)Kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme."

Mwisho wa kunukuu.
Kati ya fursa zote hizo wenzetu wapo tayari ila sisi hatupo tayari, zaidi ukiangalia fursa no.7 utaona udhaifu mkubwa wa serekali yetu, kwani mpaka sasa ukiuliza mchakato wa kutoa vitambulisho vya kiraiya limefikia wapi? jibu ni kitendawili kigumu.
YOU HAVE A LOT TO LEAN
Kama kweli haya ndo malengo ya EA Cmm, mbona hakuna tunalonufaika nalo? wala hakuna haja ya kuongea mate yanamwagika kumbe ni kwa ajili ya wanyarwanda!
 
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako mazuri. Na siku zote jambo la msingi ni kujitasmini wewe kwanza ya kumtasmini mwenzio. Je! Tanzania chini ya Raisi Kikwete na Serekali ya ccm ilishawai kutoa tasmini kwa upande wa tanzania jinsi tunafanya ndani ya jumuiya?
Na hili ndilo tatizo kubwa ndani ya viongozi wa TZ, na pengine hii serikali haijui nini wanapaswa kufanya ndani ya shirikisho.

Nimegundua kuwa katika Tanzania yeyote anaweza kuwa Rais wa nchi....
 
Agreeed!

Tunao viongozi walioishia kula kulala..na kutafuta visingizio na kuomba huruma ili waonekane kama wapo sahihi saana kumbe wanatetea uzembe na uvivu wao wa kufikiri na kwenda kasi kama wengine.

Tunalo tatizo la kudanganyana sana, na Serikali yetu inatumia sana mwanya huo ili wananchi waone kuna juhudi au umakini sana ktk kuingia EAC!.. WAPI?

Ukifuatilia undani ktk 'BIG RESULTS NOW' utagundua ni matokeo ya kuwafanya wananchi wafurahie kisichokuwepo....au wafarijike na hali waliyo nayo..hata kama wote tunapelekwa ktk udhaifu...tubaki kuangalia tu! NO WAY...tunao viongozi wazembe mno..wanatakiwa kutambua kuwa wao ndio kiini cha matatizo yote ya ndani na ktk EAC...!

Kwa Utawala wetu huu..hakuna kiongozi anayeweza kuliambia taifa 'WHERE ARE WE NOW...NA where we want to be in the next 5Years!! Usanii mtupu na kulalama tu kuomba huruma ya umma..!

Nawasilisha!

Uko sahii kabisa mkuu, kwani tunakumbuka serekali hii ilishasema:-

-MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA watu wakaamini,wakasubiria na mwisho wamechoka na sijui nini kitatokea
-KILIMO KWANZA- wakulima wakaamini wakaletewa power-tilar inayolima kama ng'ombe mwisho wa siku mazao machache mvua isipo nyesha hawapati kitu kilimo cha umwagiliaji ni historia, soko la mazao mkulima atajua mwenyewe, leo wamechoka na sijui nini kitafuata.
-WAFUGAJI TUTAWAPATIA MAENEO YA MALISHO YA MIFUGO YENU- wafugaji wakaamini, wakasubiria bila kupata majibu, mwisho mifugo yao ikaanza kuuawa kwa risasi za moto, waliothubutu kuitetea mifugo yao nao wakauwawa kwa staili ileile ya risasi, leo wote wamechoka na sijui nini kitatokea.
-TULIAMBIWA TUTANUFAIKA NA SHIRIKISHO LA E. AFRICA- tukaamini nakusubiria manufaa, leo picha imebadilika, sio tena faida imekuwa wanataka kutuzunguka, Waziri haeleweki, Raisi anatuchanganya eti Kenya, Uganda na Rwanda wanatuzunguka alafu hapo hapo hatutajitoa kwenye shirikisho. Watanzania tumechoka na sijui nini kitatokea.
 
Ndugu yangu mi nadhani unaangalia maslahi ya kwako binafsi zaidi (nahisi unashabikia tu urahisi wa kusafiri ndani ya nchi hizi kwa sababu wewe unasafiri) kama sivyo utaniwia radhi!
Hoja ya msingi hapa ni kwamba Watanzania watanufaikaje na jumuiya hii. Katika vipengele vyote hivi nane hakuna hata kimoja chenye physical impact kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida. Jumuiya hizi zinakuwepo na kupita pia kama ilivyokuwa East African Community ya zamani, angalau tulibakia na mabaki yake hadi leo. Katika hii mpya bado hakuna mahali Tanzania inapoonekana kuwa na base zaidi ya kuwa njia ya kunufaisha wenzetu....KWA HILI HADANGANYIKI MTU HAPA...RAISI YUKO SAHIHI KABISA

Nayaheshimu mawazo yako mkuu, Kama ulivyosema watanzania hatunufaiki na hili shirikisho na pili unamuunga mkono Mh. Raisi, Je! huoni kama unajichanganya na pengine hujitambui au kwa lugha nyingine ufahamu wako uko likizo maana Raisi kasema Tanzania haijitoi kwenye Shirikisho la E. Africa?
Ningekuwa mtoto wa mujini ningekuita KILAZA.
 
Tafssiri yako haina mashiko ni kama mipasho unapoteza muda tu haisaidii na haikusaidii ujumbe umewafikia walengwa wana macho wana masikio ata wakituita makasuku Km wakt ule ukweli utabaki kuwa waxi kuwa bila tz hakuna eac wanadanganyana tuu vinchi vidogo viongozi wezi walevi wanaendekeza njaa na tamaa
 
Huwezi ukapata mawazo kama haya kutoka kwa mtu mwenye akili timamu ata siku moja. Ila majigambo, kiburi, sifa za kijinga na kujiamini kwa mambo ya kipumbavu utayapata kwa walevi na wavuta bangi tu.
 
Ndugu zangu,

Jana saa kumi jioni nilishachukua nafasi yangu kwenye kijiwe hicho ( Pichani) cha wafanyabiashara ndogo ndogo Soko Kuu, Iringa.

Kwa kawaida, ndani ya banda hili la biashara kwa muda kama ule wa jana, watu huwa bize kuangalia mechi za Ligi Kuu zinazorushwa na Azam TV kutokea Dar. Na jana kulikuwa na Big Match; Azam dhidi ya Mbeya City.

Lakini, kwa umuhimu wa hotuba ya Rais, hata wapenzi wale wa soka waliamua kwa hiyari yao kusamehe soka na kubaki na hamu ya kufuatilia mambo muhimu kwa nchi, na kwa wakati huu.

Na hakika, aliyoanza nayo JK kwenye hotuba yake ndio haswa ilikuwa hamu ya Watanzania hawa niliojumuika nao kumsikiliza Rais wa Nchi.

Walikuwa na hamu sana ya kupata mtazamo na ufafanuzi wa Rais wao juu ya yaliyo karibu sana nao ( Proximity): Katiba na wimbi la Ujangili. Katiba inahusu mustakabali wao na watoto wao. Inahusu pia ulinzi wa rasilimali zao. Kwamba Katiba iliyo bora inaweza pia kuwazuia ' Majangili wa Kisiasa' kuingia au kubaki madarakani huku wakifanya ' ujangili' wa mali ya umma wakilindwa na mfumo dhaifu unaotokana na Katiba dhaifu.

Na Wananchi wale wanajua pia, kuwa wimbi la ujangili dhidi ya wanyamapori wetu unawahusisha pia vigogo wakiwemo wanasiasa. Wanataka kujua namna gani wahusika watadhibitiwa ili wasije kuwamaliza wanyamapori wetu kwa ' Ujangili' wao.

Suala la Afrika Mashariki na kutengwa kwa nchi yetu linawagusa na kuwakera Watanzania wengi. Wamefurahi kuwa Rais wa Nchi kalizungumzia Bungeni. Kwamba msimamo wetu kama nchi hatujitoi Afrika Mashariki.

Na ni ukweli, kuwa si ni Wana Jumuiya ya Afrika Mashariki na tutabaki kuwa hivyo. Hatuwezi kuwa jumuiya ya watu wa Afrika Magharibi, Kusini au Kaskazini.

Rais ameahidi kuendelea kuzungumza na Marais wenzake na tunaamini kuwa itafika mahali wenzake nao watatambua, kuwa hakuna Afrika Mashariki bila Tanzania.

Lakini, kwa Watanzania , Jumuiya ya Afrika Mashariki haiwaumizi sana kichwa kuliko haya ya Katiba , ujangili na mengineyo wanayokutana nayo nje ya milango yao kila kukicha. Mambo yenye kauthiri maisha yao ya kila siku.

Maana, tunajua, kuwa hakuna nchi ya Afrika Mashariki itakayotulazimisha tushirikiane kwenye tusilotaka kushirikiana. Tukiweka msimamo wetu kama taifa utabaki kuwa hivyo, hata waje na vifaru vya kivita, tutapigania msimamo wetu na tutashinda.

Na katika hili iko wazi, kuwa kwa sasa Watanzania hatutaki yaingizwe kwenye jumuiya masuala ya Uhamiaji, Ajira, Ardhi, Sarafu Moja na nchi yetu kuwa ndani ya Shirikisho la Kisiasa. Mengine yote tumesema sawa.

Na Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza duniani kuchagua mambo ya kushirikiana kwenye jumuiya. Mfano hai ni kwenye Jumuiya ya Ulaya, nchi ya Norway ni mwanachama lakini haimo kwenye ushirikiano wa masuala ya Uhamiaji ( Schengen) Hivyo hivyo kwa Uingereza.

Kwenye Jumuiya hiyo hiyo ya Ulaya, Norway, Sweden na Uingereza hawamo kwenye kushirikiana kwenye sarafu moja ya Euro. Na kuna mifano mingine. Yote haya yanatokana na matakwa ya wananchi wa nchi hizo kupitia kura za maoni. Kwamba wananchi wa nchi hizo wamekuwa tayari kuwa kwenye Jumuiya ya Ulaya lakini kuna maeneo ambayo wamekataa kuyaingiza kwenye jumuiya.

Na sisi Watanzania tutakuwa watu wa ajabu sana, katika mazingira yetu ya sasa, tukakubali kuyaingiza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki maeneo ya Uhamiaji, Ajira, Ardhi, Sarafu , na hata kuwa ndani ya Shirikisho la kisiasa.

Hivyo basi, kuhusu Afrika Mashariki, Watanzania tuko nyuma ya Rais wetu kimsimamo, na hatutasogea hata hatua moja.

Lakini, kuna ya kwetu ya kila kukicha na yenye kutuhusu na kutuathiri leo, na yatawahusu na kuwaathiri watoto na wajukuu zetu kesho na kesho kutwa.

Ni haya ya Katiba, Ujangili, kutunga sheria za kubana vyombo vya habari ilihali uporaji na kujimilikisha maelfu ya ardhi bila hata kuyatumia kunaofanywa hata na wanasiasa wetu kukiendelea.

Haya yana athari ya mbaya kwa mwananchi kila kukicha na tuendelee kupambana nayo kwa kasi zaidi...
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Katika kutetea maslahi ya Tanzania daima tutakuwa pamoja na Rais wetu. Hotuba ilijaa busara na hekima ya hali ya juu! Hongera sana Washauri wa Rais! Mungu ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom