Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Wakati anakujengea hukuona anakubana,,,akakununulia gari hukuona anakubana,,,akakutafutia kazi hukuona anakubana,,,wewe dawa yako n kupewa ukilema mmoja mzuri mzuri ili upate cha kuhadithia ndugu zako

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ushauri huu ni mzuri kama ana uhakika na anachotaka kufanya na SIO wenge.I have seen many GOOD girls wakijaribu hii strategy na ikawork lakini wakaishia kuumizwa wao tena sana
Usicheze na Ukimwi wewe!!!
 
Well natambua kabisaaa what i did sio kitu cha kuwa proud nacho na nimesema kabisa. Kabla ya kuwa na huyu mume wa mtu nilikuwa kwenye toxic relationship hadi pale nilipokutana na huyu. To be honest hajawahi nifanyia baya, amenipa good times sana, nimetembea nchi nyingi kwa sababu yake. Hizi good times na kujali kwake ndiko kulinipiga upofu japo kweli kuna muda nafsi inauma kuwa sio wangu. Lakini muda mwingi sana nakuwa nae kama tu vile watu wengine wenye mahusiano wanavyokuwa.

Anyway nimechoka kuwa mchepuko wake na nafsi inazidi kunisuta ndio maana nataka niachane nae.
Hongera kwa kutambua japo wengi wanakutukana kama hawajawahi kosea lakini bado wewe ni binadamu kukosea kupo kwenye ukristo kuna mstari unasema dhambi zenu zijapo kua nyekundu sana nitazifanya kua nyeupe kama theruji.

Anza kusali kwakumanisha yaani mrudie Mungu kiukweli then mwambie huyo mtu umeamua kuacha dhambi ya uzinzi hivyo mrudishie vyake ili uwe huru,na Mungu atakutetea ktk hili.
 
Hongera kwa kutambua japo wengi wanakutukana kama hawajawahi kosea lakini bado wewe ni binadamu kukosea kupo kwenye ukristo kuna mstari unasema dhambi zenu zijapo kua nyekundu sana nitazifanya kua nyeupe kama theruji.

Anza kusali kwakumanisha yaani mrudie Mungu kiukweli then mwambie huyo mtu umeamua kuacha dhambi ya uzinzi hivyo mrudishie vyake ili uwe huru,na Mungu atakutetea ktk hili.
Kwenye kirudisha ndio kimbembe
 
Aya sasa wacha tukushauri.
Ushauri wangu hapa ni kwamba uhai ni muhimu. Ili uokoe uhai wako rudisha gari rudisha nyumba sema hivyo vyote sivitaki.
Kama unaona unataka chill with the big boys wee endelea tuu kumpa jamaa mbususu basi ule life ila sasa usije ukasaba isha kifo cha huyo kijana mwengine. So achana nae kabisaa na umwambie why. Wewe uishie kuwa na huyo mume wa mtu basi cha muhimu sii anakupa huduma bwana...security that money provides.

Out of topic. Inaelekea mrembo una tako na mbususu tamu mpaka jamaa anajenga nyumba😂😂😂😂
Hii bado ni hatari zaidi kwake.
Inaonesha jamaa amempenda mno,maana sio kwa kuwekeza huko.
Akunali kufunga nae ndoa ya bomani.
Mbona waislam na baadhi ya makabila au jamii wanaolewa mke zaidi ya mmoja kwa mume mmoja?
 
Hii bado ni hatari zaidi kwake.
Inaonesha jamaa amempenda mno,maana sio kwa kuwekeza huko.
Akunali kufunga nae ndoa ya bomani.
Mbona waislam na baadhi ya makabila au jamii wanaolewa mke zaidi ya mmoja kwa mume mmoja?
Sasa yeye mwenyewe anakwambia anataka wake wapeke yake awe na uhuru naye....tatizo wanawake wwngi wanajidanganya kuwa watapata mgegedo wa kwao peke yao.
Yeye cha msingi jamaa anamuhudumia atulize hiyo punani yake jamaa asasambue basi.
 
Sista, huyo mshua ndio "aliyekujenga".

Hiyo "akiba bank" ni kwa sababu ya huyo Mshua. Unapokea pesa ya kodi ya nyumba uliyojengewa, mekupangishia nyumba ambayo yeye ndo analipa kodi, akakutafutia kazi ambayo mshahara sio haba, akakununulia gari(ambalo pia mazaga yote kutoka mafuta mpaka service anaweza akawa nahudumia yeye), kakununulia viwanja(ambavyo pia hata kodi ya viwanja hivyo atakuwa analipia yeye), bado anakuhudumia na mishe nyingine. Pesa yako/mshahara wako unakuwa hauna kazi hapo, kila kitu unapewa. Na bado alisaidia familia yako na wanamfahamu(unafikiri ilikuwa bahati mbaya yeye kufanya hivyo?! Niamini sista hiyo ilikuwa makusudi kabisa.)
Mshua kakutoa katika level moja ya maisha kakupeleka level nyingine, ambayo kwa juhudi zako binafsi labda ingechukua zaidi ya miaka mitatu. Ndani ya miaka mitatu status yako imebadilika kabisa, wewe wa sasa ni "land lady","Land owner","mmiliki wa chimbo cha usafiri(bila shaka na driving school alikupeleka mshua, kwa hivyo akakuongezea na skill hapo, "driving")",
Mshua alikuondolea shida zako kwa asilimia 90 hadi 99(shida nyingi zinasababishwa na kutokuwa na pesa ama koneksheni), akakuondolea stress za ajabu ajabu. Uhuru wako mpya(ambao hapo kabla uliutumia kutatua shida zako) ndo huo huo unakwambia unashida mpya, ambayo ni huyo mshua.

Huyo mshua ndo kakujenga. Akiamua kukubomoa huwezi pingana nae kivyovyote vile

Unawaza kurudisha mali tu. Je, muda wake ? hisia zake? Utazirudishaje? (Usije sema ooh muda wako, hisia zako, kwa sababu kwa unchokisema huo muda wako na hisia zako ni Feki tu, hazikuwa za ukweli hata punje.)
Utasema amekutumia, la hasha, wewe ndo umemtumia. Mshua kajitoa mazima kwako, wewe unajitoa kwa kujifikiria sana.

"All is Fair in Love and War."

Nimekuelewa, na hisia zangu sio fake kwake.
 
M

Mwambie amuache mke wake Halafu akuoe wewe,
Hakika Atakataa na icho ndo unachokitaka akishakataaa unamrudishia nyumba na gari unaanza maisha mapya na huyo unayemtaka.

Akikubali kumuacha mke wake pia uta mind vilevile maana mwanaume mpumbavu ndo anaweza kuacha mke wake maana yake na wewe badae anaweza kukiacha, unamrudishia nyumba na gari halafu unaachananae.
Je yuko tayari kurudisha hizo mali?
 
Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
Rudisha kila kitu alichokupa. Kisha kuwa free kuachana nae.
 
Thread Tele Humu Watu Wanakufa Kisa Mapenzi Nawe Umeanza
Rudisha
Gari Alilokununulia
Nyumba Aliyokujengea
Kodi Anayolipa

Halafu Huyo Unayempenda Mkaanze Upya
Hapo Umenasa Mwenyewe, Huna Namna
Unadhani aliponunua gari, kujengea nyumba kulipa kodi kwamba he did it just for granted? Kwa maelezo yako nakuonea huruma sana hasa kwa hayo maamuzi unayotaka kuchukua kwani kaburi limekaribia kukumeza, unamkumbuka yule mwanamke mwenzio aliyeuawa huko dsm kisa kala vya watu afu mzigo anawapa wengine? UKITAKA KULA LAZIMA ULIWE nakuomba sana hata kama sikujui usilete ujanjajanja kwenye uwekezaji ulofanywa na mtu tena akiwa na akili timamu.

Yaani unaumia alipokwambia umzalie na akati una gari, una kazi, nyumba n.k. kwa taarifa yako huyo jamaa siyo lofa wala siyo buzi nakuomba umvumilie kama alivyojikamua na kukufanyia hayo uliyoyasema mwenyewe vinginevyo hizo mali utaziacha na huyo kiben10 wako hatakuoa ataishia kuhudhuria mazishi.
Kama hujui ukiona mtu una date naye anakujengea nyumba n.k huo ni msumari unajipigilia kwani hatokubali hiyo nyumba aingie mwanaume mwingine.
 
Kwanza kabisa hakuna mwanadam asiyefanya makosa usijione kama wewe ni mkosaji saana wote kwa namna moja au nyingine tunakosea ktk maisha.

Kama unataka kuachana na huyo mwanaume kwanza acha kujilaumu jisamehe halafu fanya maamuzi na uwe tayari kwa matokeo ya maamuzi utakayofanya.
1. Anza kupanga mipango yako na kuitekeleza kwa kutumia kipato chako.
2. Rudisha nyumba, gari na kila kitu kinachoonekana ulichopewa na huyo mwanaume hata kama kipo kwa jina lako
3. Hama kwenye nyumba unayolipiwa na huyo mwanaume anza kulipa kodi mwenyewe.

Utekelezaji wa haya upangie muda mfano jipe miezi labda 4 chukua kodi na kama una akiba anzisha biashara yako kwa siri ili ikuboost mara utakappachana na huyo mwanaume.

HAKUTAKUWA NA KUACHANA ENDAPO UTABAKI NA MALI ULIZOPEWA NA HUYO MWANAUME.
 
Back
Top Bottom