Nimekumbuka nilichofanya siku kama leo mwaka 2019 katika safari yangu ya Mpanda

Rabonn

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
5,733
10,928
Wadau natumaini mko njema kabisa.
Heri ya Jumapili kwenu nyote.

Technology ni kitu chema sana acha tu tukipe heshima yake.

Leo kwakua nime dodge kwenda kanisani bas nilijikuta ratiba zangu ni za kutafutiza sana kwakua siku zote Jumapili kuanzia saa mbil asubuh mpaka saa Nane mchana huu muda tika nikiwa mtoto nilishafundishwa kuutoa kwa BWANA kanisani, nami nawazoesha hivyo wanangu, so ni Mambo ya ibada na baada ya hapo mtakutana kivikundi na wapendwa mpeane updates za hapa na pale kuhusu nini kinaendelea nyumbani kwa Mungu na nini kinatakiwa kifanyike basi mpaka mnamaliza yoote unajikuta mnashuka nyumbani saa Tisa hivi familia nzima then ratiba za nyumban zinaanzia hapo.

Sasa kwakua leo sijakwenda church, basi ratiba iko blank na sikua na jambo maalumu, ikabidi nichek chek simu nikakutana na notifications kibao na the one of interest ilikua ni hii ya GOOGLE PHOTO ambapo wakawa wamenikumbusha picha zote nilizopiga 3 years back siku kama ya leo yaan 15 May 2019.

As you all know, pictures are for memories basi siku hii nilipiga picha 3 tuu (mi sio mpenzi wa kujipiga piga picha hata hizi nilizopiga siku hiyo zina sababu yake ilonifanya niandike stori hii).

Hii picha bwana nilikua nimepiga kwenye basi nikiwa safarini toka Dar kwenda Mpanda ambapo jina la basi ni MAJINJA.

Nilipoiona hii picha nikatabasamu kwakua kituko nilichofanya siku hiyo sikutegemea hata mimi kama ningeweza kukomaa nacho...

Ishu ni hivii,

Safari inaanza Ubungo terminal na ilikua ni ya kikazi na tulipaswa kuondoka staff wawili.Na nilikata siti 2 kwa pesa yangu. Sikumbuki vizur nauli ila ilkua kati ya ktu kama 40k - 50k Dar kuishia Sumbawanga then hapo kuna vibasi vidogo toka Sumbawanga kufika Mpanda.

Mimi ni mapema tu Ubungo ila cha kusikitisha jamaa yangu yeye alichelewa kufika ingawa naye pia alikua na usafir na anatokea Mbweni tu hapo.

Nikaona isiwe kesi kwakua ticket ninazo mimi sikutaka kelele nikampigia tu simu mshkaji kuwa "oya ushaachwa jipange kivingine na pesa yangu ya nauli nilokata siti kwa ajili yako naomba uniingizie kwa M-pesa".Fresh, fresh akanambia tu usiwaambie ofisini kama nimechelewa, wasijue sijaondoka maana tulikua na kikao na wadau wa halmashauri kuhusu negotiations ya tenda ya ukarabati wa miundombinu flan pale stendi mpya ya mabasi ya Mizengo Pinda na sote ilikua muhimu kuwepo.

Kwakua gari huwa zina abiria vituo vya njiani kama vile Mbezi Kibamba na maili moja, nikawa mpole tu kila abiria aliyepanda akawa anakaa kwenye zingine zilizowazi.

Sasa pale Maili moja siti zote zikawa zimeenea kasoro ya kwangu tu hapo ndipo nikamuita konda kiustaarabu na kumwambia;

" e bwana ee, sasa ni hivi, mshkaji wangu mwenye hii siti kachelewa usafir Dar na mimi ndio mwenye ticketi.Tufanye jambo moja , katika pesa niliotoa,kata shilingi elfu 15, halafu inayobaki nirudishie ili uwe huru kuuza hii siti kwa mtu mwingine kwa bei kamili na wewe uwe umambulia ganji ya shilingi 15,000/= bila jasho wala bila kutia shoti hesabu zako.

Jamaa akaleta longo longo pale hakua straight ila kwa uelewa wangu hakua tayar kufany hiyo Swap lakin kwa uzoefu wake akajua atamweka tu mtu pale akae bila mimi kuleta shida.

Sikutaka maneno mengi, nikatulia tuliii safar ikaendelea. Ila nikawa namwona anaichek sana siti yangu huku wanajadiliana na mwenzake then wana reffer chati za siti kwenye makaratasi yao kisha wanawasiliana na ma agent wao vituo vya mbele.

Moyoni nikasema huyu ngoja nimwonyeshe ukenge hanijui.

Nikashusha begi yangu ndogo (back pack) toka kwenye carrier ya basi nikaiweka kwenye ile siti tupu halafu mimi nikasogea siti ya dirishani.Nikatoa glass/miwani yangu mikubwa ile myeusi nikavaa na nikatia earphone masikioni safari ikaendelea.

Shida ikaanza tulipofika Mlandizi, jamaa akapakia abiria gari ikaondoka.Fasta akamwelekeza aje akae kwangu yeye konda hakusogea.Abiria mwenzangu alipofika na kutaka kukaa, nikamwelekeza kwa upendo tu na uungwana kwamba ile siti imelipiwa na ina mtu mwenye vifaa vyake hapo kama unavyoona.

Jamaa akawa mwelewa tu akarudi kwa konda.

Konda akajua natikisa tukiberiti bas akaja mwenyewe.Sikutaka hata kumwangalia aliponigusa bega kunishtua nikamwambia "matakwa yangu yako wazi na nilishakueleza toka tuko Maili moja,nirudishie nauli ili uuze siti hii kwa mtu mwingine , kinyume na hapo tusisumbuane"..safari ikaendelea akiwa haamini kinachotokea.

Ikabidi yule abiria akamkalishe kwenye ngazi pale mlangoni wanakosimamaga karibu na dereva. Basi abiria wengine nikaona kama wananitazama kwa jicho la hasira hivi,nikasema shauri yao watajua wenyewe..

Attempt nyingine ikatokea Chalinze pia Morogoro Ila msimamo ukawa ni ule ule.Yeye kashikilia msimamo wake na mimi nikashikilia ticket yangu 😂.

Kufika mikumi pale kapakia wamasai sijui walikua wanashuka Ruaha mbuyuni basi wamesimama pale kwenye corridor ya basi huku siti yangu iko plain na mimi wala siangalii mtu nishakula miwani yangu hata sina habari ila konda namshuhudia akiwa na makasiriko yasiyo ya nchi hii na ikafika muda akazua zogo na abiria wenzangu wakaunga tera wanamsaidia kwanini watu wasimame wakati siti iko wazi. Mimi nimetulia Earphone masikioni ila nasikia kila kitu maana hata mziki nilizima.

Nilipoona kuwa kelele zimekua nyingi nakamwambia Konda kwa sauti nzuri ambayo abiria wengine pia wakanisikia bayana.Kwamba "nirudishie pesa ya siti yangu ili uwe huru kuiuza kwa abiria wengine maana nimeilipia" hapo nikaona abiria wenzangu wamekua wapole baada ya kuelewa nini kinaendelea basi siti ikasafir tupu mpaka tunafika Mbeya.

Pale kwakua tayar ni usiku muda tunafika Mbeya, Basi za sumbawanga huwa zinasimamisha sana abiria hivyo watu kibao wamesimama ambao waliendelea kukosa siti maana pale Mbeya abiria wengi hushuka so watu huwa wanakaa tu randomly bila utaratibu wa ticket.

Binafsi nikawa niko kwenye phase 2 ya operation yangu kama mrusi, "siti haikaliwi".

Nikaitisha tena mazungumzo ya kutafuta suluhu na konda kama Putin vile.
"Kwa hapa tulipofika, nirudishie nauli ya Mbeya-Sumbawanga ila hapo wewe hutaambulia hata 10 mbovu kwakua pesa ishapungua"

Jamaa nae akaendelea kugomea suluhu kama Zelensky anataka tuendlee na mgogoro. Nikaona isiwe kesi acha siti ifike sumbawanga vile vile tu.

Tulipofika TUNDUMA alipanda bibi mmoja mzee sana na mgonjwa inaonekana.Ofcz na mimi nilimwona, konda alishindwa kumwacha kwakua walikua wanakwenda kwenye matibabu, nikaona konda kawa mpole akaja kuniomba yule bibi akae pale kwakua hawez kusimama na corridor pale imejaa hawez kulala pale..
Nikamuuliza simply tu "Huyo bibi si amekupa nauli"
Akajibu ndiyo.
Nikamwambia "ilete hiyo pesa basi, ili mimi ndio niwe nimemuuzia siti".

Jamaa kishingo upande ikabidi akubali kupoteza pambano, nikaichukua ile pesa yule bibi akaletwa akakaa pale na mjukuu wake akasimama pembeni yake.Jamaa konda dhahiri shair alionyesha chuki sana juu yangu na mimi kwa amani zooote nikawa najiskia furaha kwakua nimepata iliyo haki yangu ambayo konda alitaka kunidhulumu kwa vivuli vya abiria.Et mimi nionekane nina roho mbaya kwa abiria sitaki wakae wakat yeye ndio kashikilia pesa yangu aile yoooote yeye.Hakutakata tugawane kama offer nilompa pale Maili moja kwamba akate 15,000 nyingine anipe .

HATIMAE TUKAFIKA Sumbawanga saa 8 usiku.Wakati wa kushuka nikachukua ile pesa nikamrudishia yule mjukuu wa yule bibi nikamwambia imsaidie tu kwenye movement zao maana sikua na chakupoteza kwakua mshkaji alishani refund pesa yangu ila tu sikua tayar konda anigeuze fala ale pesa yangu kwa ujanja wa kijinga.Yule dogo mjukuu wa yule bibi Akanishukuru sana maana hata hiyo walionekana kuwa na hardship flan.Ila yule konda hakujua kama ile pesa ya yule bibi nimewarudishia wenyewe

Sasa basi kwakua ni tayar saa 8 usiku na mvua ilikua inanyesha sana halaf masaa ma 4 mbele yaan saa 12 asbh gar ya kwaza kuelekea mpanda inaondoka, sikuona ulazima wa kuzungua na mabida boda na mvua ile kuchukua lodge nilale ukizingatia ilikua ni mara yangu ya kwanza kufika Sumbawanga af tayar nisha athirika kimtazamo kuhusu stori za uchawi wa sumbawanga lakin ni matumizi mabaya ya pesa kukod chumba nilipe 20k af nilale masaa mawili tu,sio kwel So nikamwambia Konda, naomba ku spend hayo masa 4 ndani ya gari mpaka kukuche 😎 ofcz nili predict responce yake...

Akanigomea kata kata 😂😂😂😂 kulipiza kisas ..nikaona isiwe shida, nikaelekea pale stend ofisi za mabasi ya mpanda nikakata ticket kabisa kisha nikawasilisha ombi langu la kukaa kwenye basi mpaka kukuche tuanze safari...EASYYYY bila kipingamizi nikapata hifadhi asbuh nikaendelea na safar yangu salamaaaa nikafika na tukafanikisha kilichotupeleka kule tukarejea salama salimin Ďar es salaam.

Kumbukizi hii ya picha toka google photo ndio ikanikumbusha sekeseke hili la 2019 , nikaishia kutabasam.

I do not understand why mtu ukiamua kusimamia yale unayoamini kwako ni sahihi basi watu wataanza kukuona we wa ajabu without even knowing the underlying factors ambazo ume consider.

Eyce

Ni hayo tu.
Ahsanteni
 
Mkuu umefanya vizuri sana kusimamia haki yako.Katika vitu ambavyo vinaweza kunifanya nipambane hadi kufa hapa Duniani (Ikibidi) ni mtu kutaka kunifanya mimi ni FALA.
Inakwaza sana chief
 
Back
Top Bottom