Nimekuja kumjibu Zitto niendelee na majukumu mengine

Kwenye tweet ya Zitto jana amemsema Sumaye kuwa si yule yule tuliyeaminishwa kuwa si msafi iweje leo ajifanye msafi, akamalizia kwa kusema 'watanzania tuna ugonjwa wa kusahau" ujumbe ni huo ila sijanukuuu kama alivyoandika.

Zitto, usahaulifu wetu watanzania ndio mtaji wenu wanasiasa wote, ila wenzako wakiutumia huo mtaji wewe unakasirika mpaka kufikia kututukana kuwa tuna ugonjwa wa kusahau vipi bwana. Je tusingekuwa wasahaulifu, tungekukumbusha kuwa ulisema umeacha siasa na sasa unafanya nini?, tungekukumbusha mambo mengi ambayo umekuwa ukiahidi bila kutekeleza.

Wewe ukiwa mtanzani mbona unaonekana mgonjwa zaidi ambaye unasahau hata yako wewe mwenyewe bora sisi timesahau ya watu yetu tunakumbuka. Acha hasira, kuwa mwanasiasa si kila atamkaye lazima umjibu, utajiharibia mwenyewe.

soma hapa tafadhali,na sijui umetumwa na nani kumjibu?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-tujadili-ni-sifa-zipi-kiongozi-awe-nazo.html
 
Duh nimeshasahau kama Jakaya anahutubia Bunge leo nimebaki nasoma huu uzi. Ngoja nikaendelee na majukumu mengine
 
Kwenye tweet ya Zitto jana amemsema Sumaye kuwa si yule yule tuliyeaminishwa kuwa si msafi iweje leo ajifanye msafi, akamalizia kwa kusema 'watanzania tuna ugonjwa wa kusahau" ujumbe ni huo ila sijanukuuu kama alivyoandika.

Zitto, usahaulifu wetu watanzania ndio mtaji wenu wanasiasa wote, ila wenzako wakiutumia huo mtaji wewe unakasirika mpaka kufikia kututukana kuwa tuna ugonjwa wa kusahau vipi bwana. Je tusingekuwa wasahaulifu, tungekukumbusha kuwa ulisema umeacha siasa na sasa unafanya nini?, tungekukumbusha mambo mengi ambayo umekuwa ukiahidi bila kutekeleza.

Wewe ukiwa mtanzani mbona unaonekana mgonjwa zaidi ambaye unasahau hata yako wewe mwenyewe bora sisi timesahau ya watu yetu tunakumbuka. Acha hasira, kuwa mwanasiasa si kila atamkaye lazima umjibu, utajiharibia mwenyewe.
kwani na wewe umesahau kuwa ni akina ROSTAM waliomnunua Zitto?
ROSTAM na Lowassa ni maadai?
 
The Investigation and the Battle

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO-KABWE
Nyaraka hii imechomolewa kwa siri toka Chadema makao makuu-
RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE----KWA-------CHADEMA--UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.

UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka.

Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe
MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.-
Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.--------
-
SEHEMU YA KWANZA 2008
Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu- vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:
Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba-+255754787550-alipokea simu kutoka kwa Ramadhani Ighondu mwenye namba-+255717760473-ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa- ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana Ramadhani Ighondu kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.
Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na Ramadhani Ighondu akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali,
Walikubaliana wakutane Sea Cliff -Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana Ramadhani Ighondu kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa…..Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia.
Chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni -Steven Wasira, Ramadhani Ighondu na Abdalla Punja (hawa wote ni TISS).Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja, akianza Mr Ighondu kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa ilikuwa ni-"bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi".
Tunaomba kujua shida yako kubwa ni nini?"-Ighondu alihoji, Katika majibu yake Zitto anajibu,--"Mimi napigania haki za watanzania, nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni wawakilishe hivyo",
Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi Zitto alilegeza msimamo wake. Katika kikao hiki kilichochukua masaa mawili, Zitto anaonekana kusita sana na anaomba apewe muda akafikirie aliyoitiwa, wote wanaafiki na kukubali ombi la Zitto na kikao kinaahirishwa.
Siku tatu tu baada ya kikao cha Hotel ya -Sea Cliff, yaani tarehe 27/6/2008 Zitto anakutana na Naibu Mkurugenzi wa TISS Ndugu Jack Zoka jijini Arusha, hiki sio kikao chao maalumu bali wamekutana -kwa mara ya kwanza wote wakiwa kwenye shughuli za kitaifa.
Katika mazungumzo yao wanaonekana ni watu wanaofahamiana japo si kwa undani, Baada ya maongezi ya dakika kadhaa wakiwa wamesimama, Mr Zoka alimuuliza-"Vipi vijana wangu walikupa ujumbe, umefikia wapi?"-Zitto aliitikia kwa kucheka na kusema"yap nipo tayari, lakini nihakikishieni usalama wangu"
Katika maongezi haya, Zoka anasikika akisema-"Ondoa shaka"-Kisha Mr Zoka anamuagiza Zitto kuwa kesho kutwa yake aende kwa Charles Kimei (Mkurugenzi CRDB Benki) pale Makao makuu, atayakuta maagizo yake huko.
Tarehe 30/6/2008 majira ya saa 12:22 za alasiri, Zitto akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Rajabu Abdala anaingia eneo la CRDB Benki mtaa wa Azikiwe, na kwenda moja kwamoja kuonana na Bw Kimei, baada ya salamu haikuchukua muda mrefu, Zitto akapelekwa katika moja ya vyumba maalumu vya bank hiyo kwenye jengo hilo hilo la Azikiwe, baada ya kufika katika chumba hicho Zitto alihamaki kuwakuta watu wawili katika chumba hicho, mmoja alikuwa ni mfanyakazi wa bank hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Maselina K. Kombe na mwingine hakuwa mgeni machoni mwa Zitto, alikuwa ni Ramadhani Ighondu yule wa TISS waliyekuwa naye kwenye kikao cha awali kule Sea Cliff -Hotel wiki chache zilizopita. Zitto alikabidhiwa Briefcase nyekundu iliyokuwa imesheheni pesa halali za kitanzania kiasi cha Shilingi milioni 250.Wakati hayo yakitendeka yule kijana aliyekuja na Zitto alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Mark 11 No T 134 AAB yenye rangi nyeupe na vioo vyeusi (Tinted). Baada ya makabidhiano yaliyochukua kama dakika 10 tu, Mr Ighondu alimwambia Zitto,-"tunataka utulivu, mengi mazuri yanakuja utafurahia kijana,"-Na kisha Zitto akatoka na begi lake (Briefcase) na kuingia nalo katiga gari ile na kutokomea.Uchunguzi umeonyesha kuwa pesa ile aliyokabidhiwa ndugu Zitto, ilitoka katika akaunti Namba-0J56708968923-yenye jina la Shani Maya, ambapo inaonyesha kuwa akaunti hii ilifunguliwa CRDB tawi la azikiwe tarehe 25/6/2008 saa 10:14 asubuhi, kisha tarehe 27/6/2008 iliingizwa kiasi cha pesa za kitanzania milioni 400. Na tarehe 30/6/2008 pesa hizo zilitolewa zote na akaunti hii ilifungwa. Madhumuni ya pesa hii kutoka CRDB kwenda kwa Zitto yanathibitishwa na kikao cha 23/6/2008 pale Hotel ya Sea Cliff kuwa ni kupunguza kasi ya Zitto kuibana serikali hasa anapo kuwa bungeni. Na kweli kasi yake iliyozoeleka kwenye kuibana serikali akiwa bungeni ikapungua na kuweka msingi wa ujenzi wa mashaka juu ya mwenendo wake wa kibunge.

SEHEMU YA PILI 2009.
Mnamo Jumatatu ya tarehe 30/11/2009 saa 04:30 asuhuhi wakati wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010,idara ya ujasusi ya ccm ilikutana kwa siri pale Moven Pick/SERENA Hotel, ndani ya idara hii wakiwamo Jack Zoka, Wilson Mkama, Kingunge Ngombale Mwiru, Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Fred Kimati, Steven Wasira, Ramadhani Ighondu, Martin Palakyo, Mwigulu Nchemba, Ahamed Msangi na Abdalla Punja. Katika kikao hiki yalijadiliwa mengi sana, lakini kubwa lilikuwa nikukabiliana na vyama vya upinzani hususani CHADEMA, -zilipangwa mbinu nyingi sana juu ya Chadema, -Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:i. Kuwanunua wagombea ubunge na Udiwani (Mtakumbuka wagombea wetu kadhaa walikuja kununuliwa na chama kina ushahidi kwenye hili).ii. Kuwanunua VIONGOZI wajuu wa CHADEMA.iii. Kutumia TISS kutisha wagombea na wanachama wa Chadema (Hii ilikuwa ni kuwakamata au kuvuruga mikutano). iv. Kuwaua baadhi ya wafuasi wa Chadema, viongozi wa Chadema na wabunge. Lakini walitilia mkazo zaidi njia ya kwanza ,ya pili na ya tatu ambapo kikao kilijiridhisha kuwa mmoja wa VIONGOZI wa Chadema ambae ni Zitto Kabwe ni mtu wao ambaye wamesha anza kumtumia, kikubwa liandaliwe fungu tu kwa ajili yakuanza mikakati yao, Waliafikiana mambo mengi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka ambao ungefuata, na wakakubaliana mambo kadhaa ambayo walimuagiza Mr Zoka akamwambie Zitto nini cha kufanya ili kupunguza nguvu ya upinzani.Kwa upande wake Zoka alikiambia kikao kuwa Zitto amemthibitishia kuwa yeye anawafuasi wakutosha ndani ya chama ambapo watamuunga mkono kwa lolote hivyo kikubwa ni pesa tu.Lakini kwanza kikao hicho kilimtaka Mr Zoka amwambie Zitto kuwa:i. taarifa zote zinazoihusu Chadema na za kila vikao vya ndani vya chama zinatakiwa pia ziifikie timu hiyo ya kijasusi ya ccm,ii. Zitto apunguze ushiriki katika majukwaa ya chama na shughuli nyingine za chama. Baada ya kikao sasa ulikuwa ni utekelezwaji wa maadhimio yao.------
Zoezi la kikao cha tarehe 30/11/2009 linaonyesha kuzaa matunda hasa baada ya kubainika mawasiliano ya karibu sana kati ya Zitto na Jack Zoka, -Kwa mfano: Jumamosi ya tarehe 6/12/2009 saa 03:43 asubuhi Zoka kupitia namba yake ya simu-+255756809535-alimpigia simu Zitto kupitia simu yake ya kiganjani ambayo ni-+255754787550,-wakati wa mawasiliano yao haya ya simu Zitto alikuwa Tabata na maongezi yao yalihusu kikao cha 30/11/2009 na kile walichoamua timu ya kijasusi ya chama (ccm) na matakwa yao kwa Zitto.

dahh...lete nyaraka ingine ilomfanya asiende arumeru kumnadi nassari
 
Usahaulifu ndio unaofanya watu wasahau kuwa Dr. Slaa alidanganya live kuhusu uwepo wa kipengele cha katiba ya Chadema.

Usahaulifu ni mtaji wa walaghai...
Kinana kashasahau meli zinazobeba meno ya tembo ni zake......
 
Amesahau kwamba aliahidi kwamba hatarudi Kigoma 2015 kuomba kura za ubunge!
 
ZITO ANATAKA KUOA MTOTO WA JM KIKWETE.
Anataka kuhakikisha ana sauti ya juu kuliko kila mtu.
 
Usahaulifu ndio unaofanya watu wasahau kuwa Dr. Slaa alidanganya live kuhusu uwepo wa kipengele cha katiba ya Chadema.

Usahaulifu ni mtaji wa walaghai...

usahaullifu ndio umetufanya tukasahau kuwa kinana ndie kinara wa pembe za ndovu tz kisha tukaenda kuwashika wachina ambao hata hawafahamu serengeti....
 
Wee ndo umekuja na habari mpya, hajawahi kuzungumzia elfu2015 kwamba ndo ataacha Siasa, ila ninachokumbuka baada ya kuahirisha adhma yake ya kuachana na Siasa mapema miaka ya 2010/11 ndipo alipo alipoamua kuanza kuonyesha nia ya urais 2015 kupitia Chadema japo alikuwa anafahamu fika kwamba kikatiba aruhusiwi kugombea urais2015, ila nia yake awaonyeshe mabosi wake wa TISS kwamba ameshaanza kukiyumbisha, hukumbuki kile kipindi MwenaHalisi wameonyesha mawasiliano yake na JackZoka akimfuatilia Zito kama anatekeleza maagizo?


Mvaa tai me ww sikuwezi hivyo cwezi kubishana na ww, kwani chuki zako na kwa Kizito unanizonesha wazi wazi
ww bandika majungu upike utakula mwenyewe yule ndo ZZK - Kigoma
 
Kwenye tweet ya Zitto jana amemsema Sumaye kuwa si yule yule tuliyeaminishwa kuwa si msafi iweje leo ajifanye msafi, akamalizia kwa kusema 'watanzania tuna ugonjwa wa kusahau" ujumbe ni huo ila sijanukuuu kama alivyoandika.

Zitto, usahaulifu wetu watanzania ndio mtaji wenu wanasiasa wote, ila wenzako wakiutumia huo mtaji wewe unakasirika mpaka kufikia kututukana kuwa tuna ugonjwa wa kusahau vipi bwana. Je tusingekuwa wasahaulifu, tungekukumbusha kuwa ulisema umeacha siasa na sasa unafanya nini?, tungekukumbusha mambo mengi ambayo umekuwa ukiahidi bila kutekeleza.

Wewe ukiwa mtanzani mbona unaonekana mgonjwa zaidi ambaye unasahau hata yako wewe mwenyewe bora sisi timesahau ya watu yetu tunakumbuka. Acha hasira, kuwa mwanasiasa si kila atamkaye lazima umjibu, utajiharibia mwenyewe.

alishasema kipindi fulani kuwa ataacha kugombea ubunge ili afanye biashara ya samaki.cha kushangaza wakati wa kugombea ulipofika naye alichukua fomu akagombea.!!!!!!!zilongwa mbali zitendwa mbali.
 
zitto asijione yeye ni bora kuliko wengine...kutumia gazeti la mwanach kumsafisha kwa kila jambo kusimpe kiburi.
Zitto atambue kuna wafi wengi zaidi yake ndani ya ccm.
 
ujinga mtupu na ninataka kuona mwisho wa haya yote.
 
Zitto moja ya wanasiasa ndumilakuwili nchi hii, anapokua anasaka mkate wake wa kila siku yuko tayari kwa lolote shari au balaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom