Nimekuja kumjibu Zitto niendelee na majukumu mengine

Jamaa anadhani tumesahau kuwa yuko kwenye payroll ya Nimrod...

Jamaa anadhani tumesahau kuwa yeye ndiye alianza kumshambulia Lema kwenye Twitter mpaka Lema akakosa uvumilivu na kumwaga ugali na mboga hapa JF

Zitto ana ugonjwa wa kusahau!

Acha Nimrod tu, je RA alishalipa deni??? au ndo kazi yenyewe ndo anaiendeleza mpaka leo...! kuigawanya Chadema???
 
Haya nenda kaendelee na shughuli zako as you said! Halafu why hukumjibu huko huko twitter?
Nashukuru ngoja nikaendelee, nimeona hapa wengi tuna access na hili tulijadili kama hivi lilivyojadiliwa na naondoka sasa.
 
Jicho kwa jicho,jino kwa jino!

Teh teh teh!tweet kwa tweet,JF kwa JF

Mtu ametoa hoja kwenye tweet,wewe unakuja kumjibu JF huu ni unafiki [kwanini usimjibu kwa uwazi badala ya kutumia anonymously ?].

Hapa sio unafiki na yeye ana access hapa pia, kwani habari ikisoma kwenye TV magazeti hayaruhusiwi kuandika?? wanaoongelea makanisani, misikitini, mikutanoni tukawajibie huko huko? by the way muda wangu umeisha hapa
 
Nape Nnauye amesahau kwamba alituhakikishia mafisadi kuwavua magamba ndani ya siku 90!
 
Jicho kwa jicho,jino kwa jino!

Teh teh teh!tweet kwa tweet,JF kwa JF

Mtu ametoa hoja kwenye tweet,wewe unakuja kumjibu JF huu ni unafiki [kwanini usimjibu kwa uwazi badala ya kutumia anonymously ?].

Kwani na yeye sumaye amejitweet kwamba yeye ni msafi mpaka zitto aamue kuanzisha hoja za kinafki kwenye mtandao wa twitter?!
 
Tatizo la huyu dogo ni kujifanya anajua kila kitu na kudhani wengine wooote ispokuwa yeye ni wajinga.
 
Sasa mkuu kama kasema "watanzania TUNA ugonjwa wa kusahau, mapovu ya nini... maana na yeye kaji-includr. Angesema MNA ugonjwa wa kusahau hapo sawa...
sasa anamlalamikia nani kama sote tuna ugonjwa wa kusahau? Taifa la malalamiko hili
 
Kwenye tweet ya Zitto jana amemsema Sumaye kuwa si yule yule tuliyeaminishwa kuwa si msafi iweje leo ajifanye msafi, akamalizia kwa kusema 'watanzania tuna ugonjwa wa kusahau" ujumbe ni huo ila sijanukuuu kama alivyoandika.

Zitto, usahaulifu wetu watanzania ndio mtaji wenu wanasiasa wote, ila wenzako wakiutumia huo mtaji wewe unakasirika mpaka kufikia kututukana kuwa tuna ugonjwa wa kusahau vipi bwana. Je tusingekuwa wasahaulifu, tungekukumbusha kuwa ulisema umeacha siasa na sasa unafanya nini?, tungekukumbusha mambo mengi ambayo umekuwa ukiahidi bila kutekeleza.

Wewe ukiwa mtanzani mbona unaonekana mgonjwa zaidi ambaye unasahau hata yako wewe mwenyewe bora sisi timesahau ya watu yetu tunakumbuka. Acha hasira, kuwa mwanasiasa si kila atamkaye lazima umjibu, utajiharibia mwenyewe.

Nina wasiwasi kama mawazo ya Sumaye ni kuangalia upande wa pili ambapo huyu jamaa yupo!!?
Labda hii ndio ile wanaiita vuruga mipango kwenye foundation au?
 
Unayosema ni kweli, lakini wanavuruga. Nimemfuatilia Zitto nyendo zake hayuko OBJECTIVE, hana sura he is someone with no faces, no direction can lead us to hell.

Yupo kimaslahi yule... amesahau kuwa alitangaza kumaliza panya wetu kwa ushirikina..
 
wasiwasi wa Zitto ni kwamba Sumaye anaweza kwenda chadema akagombea Urais 2015, wakati Zitto mwenyewe anautaka Urais.

Mimi nadhani ifike mahali wati wachambue wenyewe pumba ni ipi na mchele ni upi. Ni watanzania wangapi wana tweet?
 
Zitto (CHADEMA) anamshambulia Sumayi (CCM) na wewe (CHADEMA) unamshambulia Zitto (CHADEMA) sasa hapo ni nani amepoteza mwelekeo (A sense of direction)?,Wewe au yeye (Zitto)?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom