Nimeitwa interview kupitia zoom , lakini wizi mtupu

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
HONGERA!KIBACHA COMPUTER TRAINING CENTER IMEKUCHAGUA KUINGIA KATIKA SHORT LIST YA WATU WATAKAO FANYA INTERVIEW TAR 1/12/2011.Baada ya kufanya uchambuzi wa kina, wewe umukua miongoni mwa watu sabini (70) tulioona kua wana vigezo vyote kuja kufanya kazi katika chuo chetu kama system analyst kama ulivyo omba. Hata hivyo miongoni mwa hao sabini, watu kumi na nane tu ndio watakaoajiriwa baada ya kupita interview yetu. Interview itafanyika ta 1/12/2011 kama ifuatavyo1/12/2011 – saa 2:00 asubuhi hadi saa 4: 00 asubuhi ;interview ya kuandika (writing interview). Saa 6:00 mchana hadi saa 8:00 mchana; interview ya mahijioano (oral interiew)2/12/2011 – saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni; interview ya vitendo (practical interview)3/12/2011 – kila alishiriki kwenye interview atapewa barua yenye matokeo ya interview pamoja na “kifuta jasho”.Watakaopita interview watatakiwa kureport kwa human resource manager jumatatu tar 5/12/2011saa 2:00 asubuhi ili kupewa maelekezo yote jinsi gani ya kuaanza kazi. Aidha, watakao pita interview watapewa wiki mbili kwa ajili ya kujiandaa pamoja na pesa ya kujikimu.Kwa kutambua kwamba wapo candidates wanao toka mbali, na ili kuepuka usumbufu ambao ulishawahi tokea awali, chuo kimeandaa hifadhi kwa interviewers wote katika hotel ya impala. Ili kuonyesha ukubali wako kwa wito wetu utatakiwa kufanya yafuatayo KABLA ya tar 30/11/2011 saa 10:30 jioni.Tuma jina lako kamili ulilotimia katika vyeti vyako, Namaba yako ya simu amabyo itapatikana muda wote pamoja na Tsh.10 000/- kwenye nama 0757 547874(pesa itumwe kwa M-pesa). Baada ya kufanya hayo utatumiwa SMS kukujulisha kwamba jina lako limekua recorded kwa interview. Utapigiwa simu jumanne tar 29/11 ili kukupa taratibu na namna gani ya kufika ARUSHA(pesa iliotajwa hapo juu itatumika kucover costs ndogo-ndogo ambazo hazikua kwenya badget yetu kama usafiri kutoka hotelini hadi interview center)Utatuwia radhi kwa kukushtukiza na uharaka wa namna hii. Tumefanya hivi ili kukimbizana na muda.Wako, S. K. Kihiyo 255 757 547874Human resource manager KIBACHA COMPUTER TRAINING CENTERZOOM TANZANIA KIBOKO.
icon13.png
 
Hebu weka sawa maelezo ya heading na content. "Kwamba uliomba kazi kupitia tangazo la zoom ndo ukaitwa kwa usaili au ni zoom ndo wamekutumia ujumbe uende kwenye hiyo interview?
Please ondoa ambiguity hiyo tuelewe.
 
Hakuna kitu kigumu hapo mzee, hutaki kuelewa tuu.
 
Miaka ya 80 utapeli huo walikuwa kwenye tangazo lao gazetini wanakuambia kwenye baruwa ya maombi uambatanishe na stempu kwa ajili ya kutumiwa majibu, kwahiyo watoto wa mjini walikuwa wanapokea maelfu ya baruwa na kuuzichana ila wao shida yao ni zile stempu tu na wanaenda kuziuza posta kwa mtu wao ambaye wamesuka wote dili.
Kumtapeli MATOLA yahitaji uwe na extra skills.
 
Dah!! Nakumbuka niliwahi kutapeliwa buku 6 nilipomaliza form six na jamaa fulani walikuwa wanajiita Metro Joblink pale Mtaa wa Pemba-Kariakoo kwenye jengo la Atecos. Nakumbuka form six kibao walipigwa changa macho hususani wale wa hapa dar.

Nilikuja kushituka kwamba nimeliwa baada ya kurudi nyumbani na kujiuliza wale jamaa mbona wamechukua mpunga wangu (6,000/=) halafu hawajanipa risiti?! Siku ya pili nikarudi pale na kukuta washikaji na mademu kibao "wanasubiri ajira".

Nikapita kimya kimya hadi ofisini kwao na kuanza kudai hela yangu na kuwatishia wakinizingua tu, namwaga sumu kwa washikaji hapo chini kwamba nyinyi ni matapeli!!!! Jamaa, kucheki sura yenyewe ngumu ikiwa na dalili zote za kutoka Tandika, wakaona mnh, jamaa atatuharibia huyu hivyo ikabidi wanirudishie mkwanja wangu.....taratiiiiiibu, nikasepa zangu!!!!
 
Hakuna kitu kigumu hapo mzee, hutaki kuelewa tuu.

Jambo gumu hapa ni kuelewa hizi lawama unaelekeza kwa nani, zoom tanzania (ambao kwa maoni yangu, tarishi hauwawi) au KIBACHA PC LONGOLONGO. It seems like huelewi kuwa sio zoom ndio waliokuita na kwa namna ulivyomaliza 'ZOOM TANZANIA KIBOKO' ni kuwachafua bila sababu.

Hebu kuwa makini kidogo mdau, unaweza kufungwa in future.
 
Dah!! Nakumbuka niliwahi kutapeliwa buku 6 nilipomaliza form six na jamaa fulani walikuwa wanajiita Metro Joblink pale Mtaa wa Pemba-Kariakoo kwenye jengo la Atecos. Nakumbuka form six kibao walipigwa changa macho hususani wale wa hapa dar. Nilikuja kushituka kwamba nimeliwa baada ya kurudi nyumbani na kujiuliza wale jamaa mbona wamechukua mpunga wangu (6,000/=) halafu hawajanipa risiti?! Siku ya pili nikarudi pale na kukuta washikaji na mademu kibao "wanasubiri ajira". Nikapita kimya kimya hadi ofisini kwao na kuanza kudai hela yangu na kuwatishia wakinizingua tu, namwaga sumu kwa washikaji hapo chini kwamba nyinyi ni matapeli!!!! Jamaa, kucheki sura yenyewe ngumu ikiwa na dalili zote za kutoka Tandika, wakaona mnh, jamaa atatuharibia huyu hivyo ikabidi wanirudishie mkwanja wangu.....taratiiiiiibu, nikasepa zangu!!!!

Na ukakosa ajira
 
HONGERA!

KIBACHA COMPUTER TRAINING CENTER IMEKUCHAGUA KUINGIA KATIKA SHORT LIST YA WATU WATAKAO FANYA INTERVIEW TAR 1/12/2011.
................
Wako,
S. K. Kihiyo
255 757 547874
Human resource manager
KIBACHA COMPUTER TRAINING CENTER

ZOOM TANZANIA KIBOKO.
icon13.png

Tatizo sio Zoom bana, tatizo ni wewe mwenyewe! We ushaona, jina lenyewe tu KIBACHA; wht's KIBACHA!!! Jina hata kuvutia halivutii!! Kwa jina kama hilo nisingehangaika hata kuangalia wametangaza nini. Hebu nitajie kampuni ya maana moja yenye jina la hovyo kama hilo!!! kwa watu ambao ni serious lazima wawe na Business/company name ambayo ipo sexy! Hivi wewe unaweza kutarajia demu anayeitwa Nantungwe awe mzuri?! Halafu abt Zoom, huna haja ya kuwalaumu....kwanza ushaambiwa "zoom"! kwani hujui ku-zoom ni ku-magnify image?! ukiona job post, just zoom it na ukijiridhisha kwamba ipo ok hata baada ya ku-zoom upo 1000% then apply it, otherwise, don't!

Miaka ya 80 utapeli huo walikuwa kwenye tangazo lao gazetini wanakuambia kwenye baruwa ya maombi uambatanishe na stempu kwa ajili ya kutumiwa majibu, kwahiyo watoto wa mjini walikuwa wanapokea maelfu ya baruwa na kuuzichana ila wao shida yao ni zile stempu tu na wanaenda kuziuza posta kwa mtu wao ambaye wamesuka wote dili.
Kumtapeli MATOLA yahitaji uwe na extra skills.
mjini shule kwa staili hiyo!
 
Dah!! Nakumbuka niliwahi kutapeliwa buku 6 nilipomaliza form six na jamaa fulani walikuwa wanajiita Metro Joblink pale Mtaa wa Pemba-Kariakoo kwenye jengo la Atecos. Nakumbuka form six kibao walipigwa changa macho hususani wale wa hapa dar. Nilikuja kushituka kwamba nimeliwa baada ya kurudi nyumbani na kujiuliza wale jamaa mbona wamechukua mpunga wangu (6,000/=) halafu hawajanipa risiti?! Siku ya pili nikarudi pale na kukuta washikaji na mademu kibao "wanasubiri ajira". Nikapita kimya kimya hadi ofisini kwao na kuanza kudai hela yangu na kuwatishia wakinizingua tu, namwaga sumu kwa washikaji hapo chini kwamba nyinyi ni matapeli!!!! Jamaa, kucheki sura yenyewe ngumu ikiwa na dalili zote za kutoka Tandika, wakaona mnh, jamaa atatuharibia huyu hivyo ikabidi wanirudishie mkwanja wangu.....taratiiiiiibu, nikasepa zangu!!!!
wewe ni nouma ila ulifanya ya msingi ungewaambia na wenzio bana hao jamaa matapel siwataki kabisa, mi mwenyewe natafuta kazi nimekuwa kama jinga yaan unaweza nitapeli hivi hivi, afu wanajamvi msijidanganye kuitwa kwenye kazi zinazotangazwa maana nimeona wanaitana kiundugu tuu, wanatangaza kama danganya toto tuu
 
Back
Top Bottom