Wenyewe humu ndani: Kwa mara ya kwanza najitokeza ktk jukwaa hili nikiwa kama member. Nimekuwa nikisoma kwa mda mrefu sasa bila kujisajiri leo nimefanya hivyo. Hata hivyo, kabla ya kuanza kushiriki utowaji mawazo napenda kuomba ushauri kitu kimoja kutoka kwenu. Mimi ni graduate wa UDSM BA, ninarafiki yangu huko USA nilipata kumtembelea mda fulani. Sasa kanipatia offer ya kunisponsor kwenye chuo ambacho kiko katika city anayoishi. Chuo husika kimempa offerya kunilipia in-state fee. Tatizo sasa ni kwamba hakina master's d. programs na inavyoonekana jamaa yangu anapendelea zaidi nisomee pale. Ili kupunguza living costs kasema nitaishi na familia yake yenye mme, mke na watoto watatu. Je, nisome another undergr.d japokuwa ukweli fani niliyoisomea UDSM siipendi? UDSM niliondoka na degree ya heshima yenye ufaulu wa kiwango cha juu je nisiendelee nayo? Umri nao unaenda, je nifanyeje? Natarajiwa kujiunga next fall 2009. Tayari I-20 nimeipata mei 23.