Nimefurahi serikali kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi

TRUJILLO

Member
Jul 22, 2013
52
29
Kwanza kabisa naipongeza serikali kwa kuwaadabisha hawa Mtanzania.

Gazeti hili kwa muda lilikuwa limeshuka mno viwango kiasi cha kuwa kama gazeti la udaku tu. Ikumbukwe kuwa ni gazeti hili lililoendesha witch hunt kiasi cha kuwaunganisha wahariri ansbert ngurumo na deo balile kwenye tukio la kujeruhiwa kibanda. huu ulikuwa upuuzi wa hali ya juu.

Wao Mtanzania hawakujali kuwaumiza watu wadogo. Wameendelea kumwandama yule dogo aliyesalitiwa na chadema na kumuonyesha kuwa ndo adui wa nchi hii!! Mtoto yule maskini alilalamikia gazeti hili bila msaada kwani kutwa kuchwa aliandikwa vitu vya uongo na gazeti hili. Nakumbuka mara ya mwisho alilalamika kuwa mtanzania wanamuonea na akamwachia mungu kuwa iko siku wataandika habari za wakubwa na ndipo watakapoona, sala yake imetimia nasi tunafurahi na huyu dogo.

Habari walizoandika zinahatarisha usalama wa nchi na kwa hilo wanastahili adhabu waliyopewa. Mhariri wa gazeti hili ajue kuwa kutaka kumtundika msalabani kijana mdogo akiacha kutaja watesi wake halisi ambao amejinasibu kuwajua na kuwa ni watu wakubwa haitamsaidia kwani naye anamuuwa mtu asiye na hatia.

Poleni Mwananchi kwani nyie hakika mmeonewa. Nasubiri Tanzania Daima na hii MwanaHalisi iliyofufuka kwa jina la Mawio.
 
Hakuna mtanzania makini anayefuatilia mambo asiyejuahaya magazeti yana mlengo gani katika uandishi wake wa habari.

Mwananchi nigazeti ambalo lilijipambanua kuwa neutral lakini Mhariri wake bwana Dennis Msaki ni kibaraka mkubwa wa kambi mojawapo kati ya zile kambi zinazohasimiana za harakati za urais ndani ya CCM. Mfano mmoja wapo ulio hai ni pale huyu Dennis alipokubali kutumika kama mwigizaji mkuu katika ile tamthilia ya video ya Rwakatale iliyotengenezwa na kijana wa CCM akishirikiana na kijana wa Chadema.

Hata Mtanzania nalo limejaa waandishi wenye njaa ya kutumika na makundi ya urais ya CCM kuanzia wa wahariri wakuu wake mpakamaripota. Ndio maana hata Kibanda alipoamua kuamia rasmi kambi mojawapo yauraisi aliamua kuhamia pale Mtanzania ili atimize majukumu yake kwa ufasaha. Kilichomtokea anakijua yeye mwenyewe ila wengine tunachojua ni kwamba ana jicho moja la kondoo. Kwa hiyo Ukiliacha gazeti la Mwanahalisi ambalo lenyewe lilikuwa linafumua uozo wote uliopo serikalini bila kujali madhara yataipata kambi gani ya urais. Haya magazeti mengine yote mawili yaliyofungiwa yanaendeshwa na kambi za urais za CCM, yamejaa waandishi makanjanja wenye kuacha taaluma yao na kuendeshwa na matumbo yao.

Kwa mtazamo wangu ilikuwa ni busara kuyafungia yote mawili "indefinitely" (bila kikomo). Tatizo kubwa walilonalo waandishi wengi siku hizi ni kutaka kujipambanua wazi bila kificho kuwa wao wapo kambi ya kumtetea mgombea urais Fulani ili akitokea akachaguliwa 2015 basi wapate nafasi za kuteuliwa za ukuu wa mikoa na wilaya. Wasichokijua wao ni kuwa katiba mpya ikipita hizo nafasi hazitakuwepo na kama zikiwepo zitakuwa sio za kuteuliwa ni kupigiwa kura.
 
FUHRER usiwe mjinga kiasi hiki. sina pingamizi na mtazamo wako juu ya magazeti kufungiwa. tatizo langu lipo kwenye ushabiki wako unapoongelea video ya lwakatare. kumbuka kwenye video ile ilikuwa denis msaky aumizwe.

Wewe kwa ujinga na ushabiki wako wa kijinga vilevile kwa chadema unaona ni sawa tu kama Msaki angeumizwa. Halafu unajifanya kumsikitikia Kibanda. Wewe una matatizo nadhani. Huyo Lwakatare wenu muulizeni kama alikuwa anapanga kweli kumuumiza Msaki siyo mnaleta ujinga hapa.
 
Last edited by a moderator:
mbona ujafurai mother wako kutumia jembe la mkono kule kijiji kwenu huu mwaka wa 50 sasa acha kutumika umri unakwenda huo msaidie mother wako atoke kwenye jembe la mkono mkomboe
 
Kwanza kabisa naipongeza serikali kwa kuwaadabisha hawa Mtanzania.

Gazeti hili kwa muda lilikuwa limeshuka mno viwango kiasi cha kuwa kama gazeti la udaku tu. Ikumbukwe kuwa ni gazeti hili lililoendesha witch hunt kiasi cha kuwaunganisha wahariri ansbert ngurumo na deo balile kwenye tukio la kujeruhiwa kibanda. huu ulikuwa upuuzi wa hali ya juu.

Wao Mtanzania hawakujali kuwaumiza watu wadogo. Wameendelea kumwandama yule dogo aliyesalitiwa na chadema na kumuonyesha kuwa ndo adui wa nchi hii!! Mtoto yule maskini alilalamikia gazeti hili bila msaada kwani kutwa kuchwa aliandikwa vitu vya uongo na gazeti hili. Nakumbuka mara ya mwisho alilalamika kuwa mtanzania wanamuonea na akamwachia mungu kuwa iko siku wataandika habari za wakubwa na ndipo watakapoona, sala yake imetimia nasi tunafurahi na huyu dogo.

Habari walizoandika zinahatarisha usalama wa nchi na kwa hilo wanastahili adhabu waliyopewa. Mhariri wa gazeti hili ajue kuwa kutaka kumtundika msalabani kijana mdogo akiacha kutaja watesi wake halisi ambao amejinasibu kuwajua na kuwa ni watu wakubwa haitamsaidia kwani naye anamuuwa mtu asiye na hatia.

Poleni Mwananchi kwani nyie hakika mmeonewa. Nasubiri Tanzania Daima na hii MwanaHalisi iliyofufuka kwa jina la Mawio.

Lazima ufurahi kwa kuwa mnamuogopa sana MHANDO
 
binafsi napinga vikali kwa hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuyafungia magazeti, km wahariri wamekiuka au kampuni husika kwanini wanakimbilia kuyafungia na cyo kuyapeleka mahakamani? niwakumbushe kidogo wakati bwana tido mhando akiwa TBC aliazisha midahalo ya wazi ambayo ilikuwa ni mwiba kwa mgombea wa ccm bwa kikwete kwenye kampen za 2010 wakamfukuza. amehamia mwananchi pia wamefungia gazeti, je hamuoni km uadilifu na uwazi wake ndo unaomponza?
 
Hata mm naipongeza sana

Hizi salaam ziwafikie tanzania daima na jamaa wote wenye mrengo wa aina hiyo
 
Hakuna kitu kama kumuonea mhando, serikali haimuonei mtu. Kama ingewasumbua hao watu individually ndo mgesema Mhando anasakamwa. Bali sasa magazeti na hasa mtanzania limestahili hata kufutwa kabisa
 
It Sucks...kuendelea kuwa na watu wenye mawazo mgando kama mleta mada.
 
Hakuna mtanzania makini anayefuatilia mambo asiyejuahaya magazeti yana mlengo gani katika uandishi wake wa habari.

Mwananchi nigazeti ambalo lilijipambanua kuwa neutral lakini Mhariri wake bwana Dennis Msaki ni kibaraka mkubwa wa kambi mojawapo kati ya zile kambi zinazohasimiana za harakati za urais ndani ya CCM. Mfano mmoja wapo ulio hai ni pale huyu Dennis alipokubali kutumika kama mwigizaji mkuu katika ile tamthilia ya video ya Rwakatale iliyotengenezwa na kijana wa CCM akishirikiana na kijana wa Chadema.

Hata Mtanzania nalo limejaa waandishi wenye njaa ya kutumika na makundi ya urais ya CCM kuanzia wa wahariri wakuu wake mpakamaripota. Ndio maana hata Kibanda alipoamua kuamia rasmi kambi mojawapo yauraisi aliamua kuhamia pale Mtanzania ili atimize majukumu yake kwa ufasaha. Kilichomtokea anakijua yeye mwenyewe ila wengine tunachojua ni kwamba ana jicho moja la kondoo. Kwa hiyo Ukiliacha gazeti la Mwanahalisi ambalo lenyewe lilikuwa linafumua uozo wote uliopo serikalini bila kujali madhara yataipata kambi gani ya urais. Haya magazeti mengine yote mawili yaliyofungiwa yanaendeshwa na kambi za urais za CCM, yamejaa waandishi makanjanja wenye kuacha taaluma yao na kuendeshwa na matumbo yao.

Kwa mtazamo wangu ilikuwa ni busara kuyafungia yote mawili "indefinitely" (bila kikomo). Tatizo kubwa walilonalo waandishi wengi siku hizi ni kutaka kujipambanua wazi bila kificho kuwa wao wapo kambi ya kumtetea mgombea urais Fulani ili akitokea akachaguliwa 2015 basi wapate nafasi za kuteuliwa za ukuu wa mikoa na wilaya. Wasichokijua wao ni kuwa katiba mpya ikipita hizo nafasi hazitakuwepo na kama zikiwepo zitakuwa sio za kuteuliwa ni kupigiwa kura.

Ama kweli nimeamini
Even Adolph Hitler was elected democratically - Barrack Obama
 
mbona ujafurai mother wako kutumia jembe la mkono kule kijiji kwenu huu mwaka wa 50 sasa acha kutumika umri unakwenda huo msaidie mother wako atoke kwenye jembe la mkono mkomboe
Acha uvivu wa kufikiri ww. Tumia kichwa kupambanua mambo. Km umeshindwa kufanya kazi umkomboe mother wako wengine wameshahama hiyo hatua
 
Mleta mada ana idiocy kubwa sana kama yule director assah mwambene.4 real mhando hata mumtafute vp,u wont get him.ana intergrity ya juu sana na ndo maana ameuplift cfa ya mwananchi.currently ndo gazeti linaloongoza kwa vigezo vyote!hii serikali watu wanapenda kujikomba komba,bla kujua ni nn wanafanya,ili wapate vyeo.hvi is there any logic kuyafungia haya magazeti?kweli nchi hii,akili ndogo inataka kuongoza akili kubwa,ila ngojeni tuu.yatakwisha haya yote!aliyeinitiate hii mada ni mbumbumbu na inaonekana umbumbumbu wake ni wa clan yao nzima,inheritable!
 
Kwanza kabisa naipongeza serikali kwa kuwaadabisha hawa Mtanzania.

Gazeti hili kwa muda lilikuwa limeshuka mno viwango kiasi cha kuwa kama gazeti la udaku tu. Ikumbukwe kuwa ni gazeti hili lililoendesha witch hunt kiasi cha kuwaunganisha wahariri ansbert ngurumo na deo balile kwenye tukio la kujeruhiwa kibanda. huu ulikuwa upuuzi wa hali ya juu.

Wao Mtanzania hawakujali kuwaumiza watu wadogo. Wameendelea kumwandama yule dogo aliyesalitiwa na chadema na kumuonyesha kuwa ndo adui wa nchi hii!! Mtoto yule maskini alilalamikia gazeti hili bila msaada kwani kutwa kuchwa aliandikwa vitu vya uongo na gazeti hili. Nakumbuka mara ya mwisho alilalamika kuwa mtanzania wanamuonea na akamwachia mungu kuwa iko siku wataandika habari za wakubwa na ndipo watakapoona, sala yake imetimia nasi tunafurahi na huyu dogo.

Habari walizoandika zinahatarisha usalama wa nchi na kwa hilo wanastahili adhabu waliyopewa. Mhariri wa gazeti hili ajue kuwa kutaka kumtundika msalabani kijana mdogo akiacha kutaja watesi wake halisi ambao amejinasibu kuwajua na kuwa ni watu wakubwa haitamsaidia kwani naye anamuuwa mtu asiye na hatia.

Poleni Mwananchi kwani nyie hakika mmeonewa. Nasubiri Tanzania Daima na hii MwanaHalisi iliyofufuka kwa jina la Mawio.
Mimi nashangaa sana , mtu akiumizwa kisiasa anaanza kuandika udaku, so what? Bashe kaumizwa kisiasa sasa anaona njia pekee ni kujidakusha. Safi sana lingepigwa ban ya milele kama MWANAHALISI tu, wafie mbali huku wote, H.b, E.L na R.A , hawa kwa sasa ndiyo sumu ya maendeleo ya Taifa hili.
 
Mleta mada ana idiocy kubwa sana kama yule director assah mwambene.4 real mhando hata mumtafute vp,u wont get him.ana intergrity ya juu sana na ndo maana ameuplift cfa ya mwananchi.currently ndo gazeti linaloongoza kwa vigezo vyote!hii serikali watu wanapenda kujikomba komba,bla kujua ni nn wanafanya,ili wapate vyeo.hvi is there any logic kuyafungia haya magazeti?kweli nchi hii,akili ndogo inataka kuongoza akili kubwa,ila ngojeni tuu.yatakwisha haya yote!aliyeinitiate hii mada ni mbumbumbu na inaonekana umbumbumbu wake ni wa clan yao nzima,inheritable!

huwezi kuona logic ya kufungiwa kwa magazeti haya sababu hujui nini maana ya viashiria vya uvunjifu wa amani katika taifa lolote, unachojua wewe ni kushabikia politics tu and nothing as.
 
Acha uvivu wa kufikiri ww. Tumia kichwa kupambanua mambo. Km umeshindwa kufanya kazi umkomboe mother wako wengine wameshahama hiyo hatua

hapo sasa, na kama anamhurumia sana mama yake alitakiwa abaki kijijini aendelee kuuma naye kwenye jembe au basi amtoe kwenye hilo jembe la mkono kwa hicho kidogo anachokipata huku mjini.
 
yanafunguliwa lini haya magazeti? sasa washindi wa droo ya mwananchi inakuwaje?
 
Kwanza kabisa naipongeza serikali kwa kuwaadabisha hawa Mtanzania.

Gazeti hili kwa muda lilikuwa limeshuka mno viwango kiasi cha kuwa kama gazeti la udaku tu. Ikumbukwe kuwa ni gazeti hili lililoendesha witch hunt kiasi cha kuwaunganisha wahariri ansbert ngurumo na deo balile kwenye tukio la kujeruhiwa kibanda. huu ulikuwa upuuzi wa hali ya juu.

Wao Mtanzania hawakujali kuwaumiza watu wadogo. Wameendelea kumwandama yule dogo aliyesalitiwa na chadema na kumuonyesha kuwa ndo adui wa nchi hii!! Mtoto yule maskini alilalamikia gazeti hili bila msaada kwani kutwa kuchwa aliandikwa vitu vya uongo na gazeti hili. Nakumbuka mara ya mwisho alilalamika kuwa mtanzania wanamuonea na akamwachia mungu kuwa iko siku wataandika habari za wakubwa na ndipo watakapoona, sala yake imetimia nasi tunafurahi na huyu dogo.

Habari walizoandika zinahatarisha usalama wa nchi na kwa hilo wanastahili adhabu waliyopewa. Mhariri wa gazeti hili ajue kuwa kutaka kumtundika msalabani kijana mdogo akiacha kutaja watesi wake halisi ambao amejinasibu kuwajua na kuwa ni watu wakubwa haitamsaidia kwani naye anamuuwa mtu asiye na hatia.

Poleni Mwananchi kwani nyie hakika mmeonewa. Nasubiri Tanzania Daima na hii MwanaHalisi iliyofufuka kwa jina la Mawio.

Kwani Gazeti la MTANZANIA bado lilikuwa Sokoni hadi sasa? Mimi tangu kununuliwa kwa KAMPUNI ya HABARI corporation na watu fulani, nilishaacha kabisa kusoma RAI , MTANZANIA na ndugu wengine wa Kampuni hiyo baada ya kuona UANDISHI usiozingatia Maadili na usio na ADABU kwa Serikali.

Hakuna Serikali makini ingeweza kuvumilia upuuzi wa GAZETI hilo. Tena mnaolaumu Serikali someni Sheria ya USALAMA WA TAIFA YA MWAKA 1970 KIFUNGU cha 5(a) na(b) kuhusu ADHABU ya kutoa SIRI ZA SERIKALI!

Adhabu iliyotolewa na Serikali ni nafuu sana na inastahili kupongezwa. Hatuwezi kuwa na Taifa la watu kuongea chochote, muda wote, mahali popote na bila sheria wala taratibu zozote!

BRAVO SERIKALI.
 
Back
Top Bottom