Haya ndio maadili ya Mtanzania?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
BONGO DAR ES SALAAM;AKILI KUMKICHWA UKILEMAA UMEACHWA FERRY,JE HAYA NDIO MAADILI YA MTANZANIA!?

Leo 12:15hrs 24/05/2022

Uadilifu ni moja ya nguzo kuu ya kimaadili katika Utamaduni wa Mtanzania, Watanzania tuna mila, desturi, sanaa, lugha, Elimu, Michezo, tiba, ulinzi, ujuzi, mavazi, Ngoma, utani, imani, na itikadi katika taasisi mbalimbali za kiasili na kisiasa, hivi vyote vinasimama katika mhimili wa maadili na nguzo ya kifalsafa ya uadilifu, Hayati Mzee mmoja aliyekuwa mwadilifu sana katika Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, watoto wake walimlaumu sana baadae kwa kuwa walikuwa na nyumba moja tu na hawakuwa na viwanja posta wala kumiliki utajiri wowote zaidi ya wao kusoma na kuhitimu.

Siku moja mmojawapo wa watoto hao akaitwa kwenye interview uko umoja wa mataifa, alipoingia kwenye interview akataja jina lake na mara moja Mwenyekiti kwenye ile panel akamuuliza mara ya pili wewe ni mtoto wa fulani, basi Mwenyekiti akaanza kuwaelezea wanapanel juu ya uadilifu wa huyo Mzee na interview ikaishia hapo wote wakakubaliana kijana huyo apate kazi Umoja wa mataifa, Kijana yule baada ya kutoka kwenye interview akalia sana maana hakupata muda wa kumshukuru marehemu baba yake zaidi ya kumlaumu kuwa alikuwa mjamaa sana,wakati wenzake wanaiba kuwa matajiri na kujenga mijumba yeye alibaki na uadilifu wake.

Mzee mmoja bepari yeye kwenye gari yake alikuwa na watoto wake kila alipotoka na gari yake, njiani wakisimamishwa na trafiki anachomoa elfu kumi anampa trafiki wanaachiwa safari inaendelea, vijana wakakuwa kwenda shule, shule zetu kuingia na interview kijana akafeli, Mama akabembeleza akatoa elfu kumi akampa mwalimu dogo akaingia shule, mwisho wa msimu ripoti inakuja kwa Baba, dogo kawa wa mwisho, Baba anagomba kwa nini umekuwa wa mwisho, dogo akaingia mfukoni akatoa elfu kumi akampa Baba, hivi ndivyo familia ilivyomlea kijana huyo, akiamini elfu kumi inaweza kutatua tatizo, penye uzia penyeza rupia.

-Kiini cha kukosa uadilifu

Mwaka 2008 nilikuwa benki fulani nimeisahau jina, alikuja mzungu mmoja kama Mkurugenzi mpya wa benki hiyo, kwa wakati huo benki hiyo iliongoza kwa kupoteza hela "fraud" hapa nchini, yule mzungu akajiuliza shida ni nini kwenye benki hii, akaitisha vyeti vya mabosi kumi viende kuhakikiwa, viliporudi majibu yalionesha vyeti nane vilikuwa feki, akaitisha vyeti vya wafanyakazi wote viende kuhakikiwa,majibu yalionyesha asilimia themanini ya vyeti vyote vimefojiwa,yule mzungu akasema hili ndilo tatizo la "fraud" katika benki hii akaagiza wafanyakazi wote wenye vyeti feki wafukuzwe, wazo lilipokataliwa na wakubwa basi yeye akaomba kuresign na kurudi Ulaya,

Watu wa rika mseto watakumbuka miaka ya tisini hadi elfu mbili ujanja ulisifika jinsi watu wanavyo changa vizuri akili yao/zao kwa nia mbaya ya kutapeli wengine, ili mradi kujipatia kipato haba au rukuki ili mradi wapate riziki tasa ambayo haizai pasipo kutumia akili vyema, tukiachana na utapeli wa mjini kwa mshamba au mtu ambae hajawahi kukutana na masahibu ya utapeli, miaka ya 1989 nikiwa vidudu niliwahi kukutana na mtu akaniambia nipe mia mbili nikushikie wahi kaniitie Dastan, nikampa hela nikaenda kumuita tuliporudi tulikuta kashachimba, nikajua nimetapeliwa na toka siku hiyo sikutapeliwa tena, Ila ndugu yangu mmoja aliuziwa sabuni kwenye boksi badala ya simu, alivyoniambia nilicheka sana,

Mwaka 2003 pale Salma cone, Mwanza alikuja mzungu mmoja akakodi taksi impeleke airport Mwanza, alikuwa anakuja Dar kufanya presentation kwenye semina fulani, akachukua taksi pale Salma cone kaenda zake airport, kala mwewe ile kushuka dar akakumbuka kasahau laptop na digital camera kwenye ile taksi aliyochukua Salma cone kumpeleka Airport Mwanza, akampigia simu rafiki yake Mwanza akamuelezea, rafiki yake akaenda Salma cone, kuulizia yule dreva taksi akampata, dreva wa taksi alikuwa ameenda kuvikabidhi kwa mwenyekiti wa mtaa, wakaenda wote kwa mwenyekiti wa mtaa wakampa laptop na digital camera, madereva wenzake wakamwambia utakufa masikini, ila yeye akawaambia kwani laptop na digital camera ndio utajiri!? Kesho yake yule mzungu karudi Mwanza,kumbe alikuwa Mkurugenzi wa GGM, na aliacha kuna interview za madereva zinaendelea mshahara Milioni tatu, mzungu akaenda Salma cone, akamuulizia yule dreva taksi akampata akamwambia hii taksi yako, akasema hapana, kabidhi kwa mwenyewe panda vx vuu hadi GGM, wakafika ggm akamwambia hr huyu mpe gari aanze kazi interview yake kashafaulu, integrity pays, uadilifu unalipa.

-Falsafa ya imani, nguvu na hamasa.

Maadili hujengwa kwa mtu kupitia hatua mbalimbali, hatua ya kwanza ya msingi ni malezi ya utotoni kutoka kwa Wazazi na jamii inayokuzunguka, baadae shuleni na kuendelea hadi uzeeni. Familia bora zinatoa Watanzania wenye malezi bora kabisa na ya kizalendo kwa nchi yao, watanzania wataozaliwa katika familia yenye malezi bora, utupatia ujumbe mzuri wa malezi bora na ya kizalendo kupitia hotuba zao pindi wahutubiapo hadhara mbalimbali, Raia mwema wa Tanzania ni yule aliyelelewa vyema na wazazi na jamii inayomzunguka na kuwa na nidhamu, tabia njema, kuwa mkweli, mwenye utii na kufuata taratibu za utamaduni wa Mtanzania.

Raia wa Tanzania tunategemea awe mwaminifu na mwenye kufanya mambo kwa haki,kwa maana ya kutopendelea au kukiuka sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Daima, Mtanzania ni mwenye kufanya kazi za halali, kwa bidii, kwa haki, bila unyanyasaji au upendeleo, kushiriki kazi za kujenga taifa, kuhimiza upendo, mshikamano na amani ambayo hutokana na kutoelewana, Daima Mtanzania anapaswa kuwa mvumilivu na mwenye hulka ya kuheshimiana, Mtanzania ni yule aliyelelewa kutobagua wengine kwa misingi ya kabila, dini, jinsi, au rangi mambo ambayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Komredi John Magufuli wanayasisitiza na kuyaishi.

-Maadili ya Mtanzania yanaendelezwa vyema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama nilivyoitaja misingi ya maadili ya Mtanzania ambayo inapaswa kulindwa, kuendelezwa na kuenziwa, ni lazima kutambua na kuendeleza, mila na desturi yetu sisi Watanzania kama ilivyosisitizwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuthamini elimu na mafunzo, wakati wa Mwalimu tulipata mafunzo toka Jkt, Vyuo vya Uongozi kama hombolo,na mashamba darasa katika kilimo, tunapaswa kuthamini tunu zetu za asili kama tamaduni zetu ambazo hazina mambo ya kutweza utu wa mtu au kumkufuru Mwenyezi Mungu. Uzalendo ukawe wa kwanza katika maisha yako, kuilinda nchi yako na kutimiza itikadi ya Afrika ni moja na Waafrika wote ni ndugu zangu.

Kuthamini na kutunza rasilimali za taifa, kukataa kutoa na kupokea rushwa, kutii sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa, kuthamini utu na kulinda maisha ya binadamu wengine, Uvaaji wa mavazi ya heshima yenye kusitiri miili yetu, lugha safi, kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo, kusaidia watu wenye mahitaji, kuthamini na kutunza mazingira yanayoizunguka Tanzania, haya yote ni maadili ya Mtanzania.

-Maadili ya Mtanzania huonekana katika mambo ya kijamii

Mavazi, lugha, kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano, kudumisha mila na desturi, ukarimu, upendo, heshima, na nidhamu, haya ni mambo yanaweza kuonyesha wewe ni mwenye maadili ya Kitanzania, Mila na desturi ni pamoja na kusalimia wakubwa kwa adabu na heshima,haya ni mazoea katika jamii, lakini yana maana kubwa sana kwa maana aliyeanza kuona jua basi ameona mengi ambayo kwa mdogo yanapaswa kuwa darasa tosha, Mila na desturi zimebeba hazina kubwa ya maadili ya Mtanzania, utandawazi,kasumba ya kuiga si maadili ya Mtanzania, Maadili ya Mtanzania ni kupendana kama ndugu, kuheshimiana, kukirimiana ili kuondoa chuki zilizosababishwa na ukoloni, hivyo basi kwa kumbukumbu nzuri ya maadili ya Mtanzania,turejee kumkumbuka mwanamajumui(Pan Africanist) Hayati Rais John Magufuli ambaye alikuwa mfano bora wa Mtanzania mwenye maadili mema, basi na turudi kwenye mstari wa maadili ya Mtanzania ili tuweze kulipeleka mbele taifa letu la Tanzania.

-Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma.

Kwa kuzingatia misingi ya maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, ambayo yanamtaka kila kiongozi wa umma kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu
utendaji wa viongozi wa umma.

Mimi fulani bin fulani ninauahidi umma kwamba:
1. Nitakuwa mzalendo na mtii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

2. Nitakuwa muadilifu na mfano kwa watumishi wa umma, watumishi wa Bunge, watumishi wa Mahakama na watu wengine katika kukuza na kusimamia maadili;

3. Sitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi au ya familia yangu, ndugu zangu au marafiki zangu au mtu mwingine;

4. Nitalinda na kutumia rasilimali za umma kwa maslahi ya umma;

5. Nitatekeleza majukumu yangu na kufanya maamuzi kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, taratibu, miongozo, mila na desturi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

6. Sitatenda kitendo chochote cha rushwa;

7. Sitaomba, kutoa au kupokea zawadi au fadhila isipokuwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Sheria;

8. Sitatoa shinikizo linalokiuka Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika utendaji kazi za umma;

9. Sitatoa siri ambazo nitazipata au kuzijua katika utumishi wangu isipokuwa kama Sheria itaelekeza
vinginevyo;

10. Nitatekeleza majukumu yangu kwa kuepusha mgongano wa maslahi wa aina yoyote na mara zote nitatoa uamuzi kwa kuzingatia Katiba na Sheria;

11. Nitatoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote bila kujali misingi ya dini, siasa, kabila, udugu, utaifa, ukanda, jinsia au hali ya mtu;

12. Nitazingatia na kulinda heshima ya nafasi yangu ya uongozi wa umma ninapokuwa kazini, nje ya mahali pa kazi na hata nitakapostaafu au kuacha kazi.

-Kuna mila na desturi za kitanzania hamna maadili ya kitanzania.
maadili ni ya Mungu tuu ambeye ndio muanzilishi wa maadili.

Kuna kitu kinaitwa mila na desturi,mila zinaweza kuwa ni za kikabila
lakini desturi tunaweza kuwa nazo kwa kushare yani kama taifa
kwa desturi zetu tukiwa ni watanzania desturi mojawapo ni wadogo kuanza kuamkia wakubwa,kusimama ili wakubwa wakae
kunyamaza wakubwa wanapoongea kutokujibizana na waliokuzidi umribkunyamaza wakati wa kula na mengine meengi
lakini hili la maadili kuwa yapo au hayapo na kilichofanya maadili hayo yasiwepo kwa kweli ni mada pana sana!
ukimbuka malezi tuliyokulia zamani yalikuwa ni malezi ya Ujamaa yaani malezi ya jamii moja ndo mana wakati wa kuoa kulikuwa na theory za wanawake wa mkoa huu wako hiiv ana wa kabila hili wako vile siku hizi watoto wetu tunawalea malezi huria,yaani ni mchanganyiko kwisha kazi!mtoto anazaliwa na mzazi mchaga na mngoni analelewa na housegirl mhehe au mmakonde! matokeo yake hata yale tulikuwa tunaamini ndiyo maadili ya kitanzania hayapo wakati sisi tulikuwa hatuwezi kuhoji amri za wazazi wetu na walimu au wakubwa zetu watoto wetu wanajiona wana hiyo mandate kuna kamsemo wanakatumia wenyewe mum/dad but its not fair,jamii imeanza kulizoea hili tukiamini haya ndo maendeleo zamani mama anajifungua mtoto wa kiume na mtoto anakuwa treated kama mwanaume since then siku hizi unakuta mtoto wa kiume kasukwa nywele na kavalishwa bangili,bado tunaweza kutembea kifua mbele kudai tuna maadili ya kitanzania?zamani tulikuwa tunaamini watot wanauzwa hospitali au baharini siku hizi wanetu wameenda mbali zaidi muulize Mwalimu wa Biology akiwa anafundisha biology anakuatana na maswali gani kwenye topic ya reproduction,wazazi siku hizi tumerelax sana kuhusu malezi,sana tumebaki kuwalaumu walimu na kina dada!tumewaachia uhuru hawa watoto kiasi cha kutisha kabisa!matokeo yake ndo hayo ya kutokujijua hata kama tuna maadili ya kitanzania au la!

Nimalizie kwa kusema,Maadili ya Mtanzania yamegawanyika katika makabila mbalimbali, kila kabila hapa kwetu lina maadili yake,hii ndiyo inareflect Tanzania kiujumla,nisisitize integrity pays, laptop na digital camera haziwezi kukufanya kuwa tajiri,pesa haijawahi kutosha,kila ukipata utahitaji tena,mwisho wa siku utakufa utaviacha, duniani tumekuja sokoni mwisho wa siku tutarudi nyumbani kwa Mwenyezi Mungu aliyetuumba,turudi kwenye misingi yetu kama Watanzania kwa namna ambayo Mwalimu Julius Nyerere alipenda tuje kuwa hivyo, Watanzania ni watu wenye uadilifu mkubwa kwa mfano wa Mwalimu Julius Nyerere,Siku zimepita ambapo watoto waliadhibiwa kwa makosa yoyote. Badala yake, mkazo wa malezi katika miaka michache iliyopita umehamia kwenye mbinu za kulea zinazomlenga mtoto. Matokeo yake, watoto siku hizi mara nyingi huachiliwa na mara chache huwajibishwa kwa matendo yao.

Maadili ya kuwafundisha

1. Heshima
Wazazi wengi hufanya makosa kuwafundisha watoto wao kuhusu heshima kwa wazee tu, lakini hilo ni kosa. Kila mtu anastahili heshima, bila kujali umri au hadhi ya kijamii. Heshima ni thamani muhimu ya kimaadili ambayo mtoto wako lazima aijue katika umri mdogo, kwani ina jukumu muhimu katika tabia yake karibu na wageni na wazee. Watoto wanaojifunza kuheshimu wenzao na wazee kutoka kwa umri mdogo watafaidika na hili, katika siku zijazo.

2. Uaminifu
Wakati wa kupata maadili, watoto kwa kawaida hujifunza kutokana na kile wanachotumia. Ili kukuza tabia ya ukweli kwa mtoto wako, mbinu yako bora ni kuiga uaminifu kadiri uwezavyo.

3. Uwajibikaji
Uwajibikaji kwa matendo ya mtu ni thamani muhimu kwa mtoto kujifunza, kwani huweka matarajio ya jinsi anavyopaswa kutenda katika maisha ya kila siku. Uwajibikaji hukita mizizi katika uhusiano wa mzazi na mtoto, lakini mtihani wake wa kweli huanza katika umri wa kwenda shule, wakati watoto lazima wachukue hatua zao bila mzazi kuwaelekeza njia kila mara.

4. Udadisi
Wazazi wengi wanaweza kuthibitisha kwamba karibu na umri wa miaka 4 watoto wao huanza kuuliza maswali makubwa ya "kwa nini". Ingawa wengine hawana hatia kama, "Kwa nini anga ni bluu?" watoto wachanga wanaweza kujitosa kwa haraka katika falsafa, kama vile, "Kwa nini watu huchukiana?"

5. Huruma
Uwezo wa mtoto kuelewa na kuunganishwa na hisia za mtu mwingine husaidia kujenga msingi wa mahusiano imara katika maisha yao, ndiyo sababu huruma mara nyingi ni thamani ya msingi kwa familia. Kwa Dk. Ford, kushughulikia dhana hii na mtoto wake wa miaka 2 kunahitaji mbinu thabiti zaidi.

6. Azimio
Kwa wengi, wazo la azimio mara nyingi hufafanuliwa kimakosa kuwa jasiri—sifa ambayo imetengwa kwa ajili ya wanaotoka na wanaojaribu kujishughulisha. Kwa kweli, thamani hii inakuza uwezo wa watoto kukabiliana na hali kwa azimio la kujaribu wawezavyo, hata kama wanahisi woga au woga.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-

-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Hapo umechemka eti Magufuri ni mfano wa kuigwa kwenye maadili ya Mtanzania,umechemka sana mfano ubaguzi,dharau,rushwa,utapeli,upendeleo,wizi na uuaji hizo ni sifa za hayati Magufuri.
Tatizo siasa ni game of perception (mtazamo). Yaani ukiamua kutengeneza picha kuwa wewe ni mtetea wanyonge basi beba camera kagawe pesa barabarani na wote wataamini hivyo.

Kiukweli alifanikiwa kujenga image hiyo, so propaganda Inafanya watu waamini hata mambo yasiyo na uhalisia.

Mfano alikua anajidai ni mcha Mungu ilihali wakati huo huo anaua watu na kutembea na mke wa mtu!!

So hata siku moja wanasiasa tusiwafanye ni mfano wa uadilifu maana tunachokiona kwao ni kile wanachoamua tukione ila ni tofauti na uhalisia wa maisha Yao.
 
Mkuu, kama unaamini kila kinachosambazwa mitandaoni utaishia kupotoka.
Mbona hakusaidia uchunguzi wa aliyetaka kumuua Lissu? Meaning Ali support Ile assassination attempt!!! Sasa huyo mtu ni mcha Mungu?? In fact alisema wasaliti wanapaswa kumalizwa alishangaa Wanajeshi wapo tu hawafanyi lolote!!!

Hiko Cha Lissu tu kinamdisqualify kuwa mcha Mungu, mbinguni hawezi kanyaga maana hakuwahi apologise hiyo dhambi kwa mhusika.
 
Labda aliungama dakika za mwisho, usiseme hawezi kuiona mbingu.
 
Mkuu hayo maadili hata CCM kwenyewe hakuna.
Walituchagulia na wakaona heri fafa kuwa rais kwa vile wale waliostahili walioneana wivu wa kupindukia.
 
Mbona hakusaidia uchunguzi wa aliyetaka kumuua Lissu? Meaning Ali support Ile assassination attempt!!! Sasa huyo mtu ni mcha Mungu?? In fact alisema wasaliti wanapaswa kumalizwa alishangaa Wanajeshi wapo tu hawafanyi lolote!!!

Hiko Cha Lissu tu kinamdisqualify kuwa mcha Mungu, mbinguni hawezi kanyaga maana hakuwahi apologise hiyo dhambi kwa mhusika.
mungu mtu unatoa na hukumu kabisa kuwa mbinguni hawezi kanyaga umejuaje hawezi kanyaga wewe ndio una vipimo vya dhambi za watu? au wewe ndio mtoa hukumu?
 
Hiyo dhambi ya Lissu alitubu? Mtu Ali paralyse unadhani aliwezaje kufanya toba? Tuachage unafiki kwamba sijui tusihukumu!! Lazima ukweli usemwe kwamba tujiandae muda wote maana hatujui lini tunaondoka Duniani.
 
Dah!...hiyo stroke ilikuwa sababu ya kile kifaa kushindwa kufanya kazi ?
 
Labda aliungama dakika za mwisho, usiseme hawezi kuiona mbingu.
Aliungama kwa Lissu au kwa Padre??? Kama hakukaa na Lissu kumwomba msamaha hata kama aliungama kwa Padre ni bure maana hata leo Lissu yupo nje ya nchi yake bila kupenda.
 
Back
Top Bottom