Nimechelewa ahadi ya kukutana na shemeji / wifi yenu mtarajiwa kwa dakika 10 tu nimekuta kaondoka na sms zinamiminika nyingi zikimalizia na asante / thanks. nakosa usingizi leo.
si unajua kibongo bongo dakika kumi mbona ni chache ukizingatia na mafoleni ( sometimes hata kama hamna tunachomekea), kazi nnayo leo
Kwakweli nilibanwa na shughuli nyengine mdogo wangu Nemo. Ila dakika kumi tu basi ndo akasirike na kuondoka? Yeye alishaniweka sana kama masaa mawili, kwavile bia zilikuwa zinanikampani basi haikuwa shida, sijataka kumkumbusha, ntakwambia siku nikikutana nae atachelewa tu kama kawaida ya wadada, kakosa uvumilivu wa dakika kumi kweli? ten minutes???Mabagala
With this type of thinking you will always end up where you at now! If keeping time is of essence kwa mwenzio then act accordingly na achana na hizi siasa za kizamani ie. kibongo bongo! Besides what is the point of having an appointment when one never shows up on time???
Amyner huwa nawahi masaa mawili kabla yake, ni leo tu nilibanwa si unajua pia ni siku ya kazi leo ( mwenzako yeye si mwajirtiwa)
Kwa leo hataki kuelewa kabisa, nimejaribu hadi nimechoka sasa, usingizi hauji