Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
- Thread starter
- #21
Samahani SoP siko kwenye group la kuleta vitu vya uzushi kama wewe umezoea vitu kama hivyo si wote tunaofanya hivyo havinisaidii kitu.Si KWELI KIVUYO HAWEZI SEMA HIVYO ANANJAA KALI NAMJUA,HUU NI UZUSHI
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=12633
HabariLeo
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amedai kipigo alichokipata kutoka kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa, wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mombeji, ni matokeo aliyotarajia kutoka kwa Jeshi hilo siku nyingi, lakini hatarudi
nyuma kudai haki za msingi na yuko tayari kufa.
................................................................................
Kwa upande wake, Kivuyo akizungumza kwa simu, alisema Chadema wamepagawa na hawajui wanaloongea kwani kwenda kwake katika ukumbi na CCM kumchagua, sio kwamba amesaliti chama hicho.
Kivuyo alisema kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kufuata taratibu za kisheria na sio kuleta vurugu na kutuhumiana kwani huo sio wakati muafaka kwa sasa.
Alisema kanuni ziko wazi na hata kipofu anajua hilo na kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kwenda katika vyombo vya sheria na sio kuleta vurugu na kupayuka ovyo barabarani.
''Meya amechaguliwa kinyume na kanuni na hata mimi nimechaguliwa kinyume na kanuni sasa Chadema wanalia nini? Sheria si ziko wazi, mahakama zipo kwa ajili ya watu wafuate taratibu kudai haki zao za msingi na sio kulaumu watu eti nimenunuliwa?" alisema Diwani huyo wa Sokoni One.