Nimeboreka mpaka basi

sipendi au sijazoea kuazima.

Niko comfortable na kitu changu.

same here....mimi hata baiskeli yangu mtu haendeshi........
tabia ya kuazimana vitu (sio gari pekee) ni tabia mbaya sana.....lazima mgombane......hasa pesa.....
 
Hata kama una gari, unaazima la mtu la nini? Afu kuna watu mjini wanaazimana hadi viatu na nguo! Tabia mbaya kweli! Afu ukute gari yako unapelekaga kwa wachina, akaitengeneze gongo la mboto ikirudi iko kama mgongo wa kobe!

Uswahili mzigo, kha!

Ila King'asti huwa unanifurahishaga sana yani, sasa hapo kwa red umefikiriaje hivyo?
 
Kuna rafiki yangu huwa ananiazima gari kwenda kwenye shughuli zake.

Lakini kama mwezi umepita gari ilikuwa haifungi boneti, nikamwambia hawezi kutembeza kwani boneti haifungi. Akaniambia haina tatizo atatengeza tu kwani tatizo dogo. Sasa jana karudi bneti imefunguka akiwa anaendesha ikagonga kioo cha mbele na show yake ya mbele kwenye boneti imetoka na haijulikani ipo wapi. Nilimuuliza kama alitengeneza akasema alikuwa bado hajatengeneza. Hapo nilikasirika sana gari ipo nyang'a nyang'a. Alichoniambia ni kuwa yaani unajali gari kuliko uzima wangu? Na hapo hana hela ya kutengeneza., sijamjibu kitu na mpaka sasa sitaki hata kumwona.

Kweli cha mtu mavi, loh!
 
nazidi kuogopa, mbona tunataka fanana kuwaza??

Mie kuazima na kuzimishwa marfuku.
Hata kama ninalo siku bovu napanda daladala tu.

Hata kama una gari, unaazima la mtu la nini? Afu kuna watu mjini wanaazimana hadi viatu na nguo! Tabia mbaya kweli! Afu ukute gari yako unapelekaga kwa wachina, akaitengeneze gongo la mboto ikirudi iko kama mgongo wa kobe!

Uswahili mzigo, kha!
 
Hata kama una gari, unaazima la mtu la nini? Afu kuna watu mjini wanaazimana hadi viatu na nguo! Tabia mbaya kweli! Afu ukute gari yako unapelekaga kwa wachina, akaitengeneze gongo la mboto ikirudi iko kama mgongo wa kobe!

Uswahili mzigo, kha!
\
mmh! King'asti naona tunawaza sawa. yaani nashangaa eti mtu unaazima gari? labda kama ni shida ama tatizo kubwa kama kwenda hosp ila kwa safari tu za kawaida jamani nashukuru Mungu TZ 11 yangu iko poa aisee. sasa hao wanaokuja na kuazima pamba lol! mjini shule aisee.

kimsingi mimi bora niazime kazini yaani gari la ofisi lkn si la mtu.
 
Last edited by a moderator:
nazidi kuogopa, mbona tunataka fanana kuwaza??

Mie kuazima na kuzimishwa marfuku.
Hata kama ninalo siku bovu napanda daladala tu.
Kuna mdada I was introduced kwake anifanyie kazi flani. Ananiona for the second time ananiambia njoo nikupe shoes to match ur bag. Nikatamani kumuuliza huna fungus? Nikamezea, nikasema nikaona vizuri hivyo viatu namuambia sirudishi. Bahati nzuri vikawa vikubwa. Nikienda tena navaa sura ya kazi, staki mie!
Afu wewe Kama ni 'tall Tina' ntakunyofoa koromeo, weeh Endelea kufanana na mimi
 
\
mmh! King'asti naona tunawaza sawa. yaani nashangaa eti mtu unaazima gari? labda kama ni shida ama tatizo kubwa kama kwenda hosp ila kwa safari tu za kawaida jamani nashukuru Mungu TZ 11 yangu iko poa aisee. sasa hao wanaokuja na kuazima pamba lol! mjini shule aisee.

kimsingi mimi bora niazime kazini yaani gari la ofisi lkn si la mtu.
Mie nna roho nzuri mwayego, Kama ni hospitali nitakupeleka! Na mafuta staki kuwekewa usije ukasema tupitie mbagala Kabla sijakurudisha tegeta. Sizoei cha mtu na mie staki changu kizoelewe!
 
Kwi kwi kwi umenichekesha sana ila na wewe una majungu khaa

hapana siyo majungu, mleta mada hakusema kama anaomba ushauri au msaada. Alichosema ni kwamba yeye alimuazima rafiki yake gari bovu, akaliaribu kabisaa, rudia kusoma uzi wake. Utamuelewa tu.
 
Mie nna roho nzuri mwayego, Kama ni hospitali nitakupeleka! Na mafuta staki kuwekewa usije ukasema tupitie mbagala Kabla sijakurudisha tegeta. Sizoei cha mtu na mie staki changu kizoelewe!

mimi niseme tu nina roho mbaya.manake mtu haniombi kitu bali mimi ndo nasukumwa kusaidia, na nikisaidia basi mm ndo mwenye mamlaka ya mwisho. kwako siombi kitu na kwangu vivyo hivyo. msibani nakuja natimiza yaniasayo kwenye ugonjwa ama sherehe naja natimiza yanipasayo lkn kamwe sitaki kuombwa na ukiniomba sikupi.
 
Ndo maana na sema Kama ni hospital nitakupeleka kiroho safi. Kama huna viatu nitakupa, sio kuazimana. Mwisho ukachukue CL yangu uendee kariakoo wakati mwenzio hata harusi za uchafuni siendi nayo! Tutaharibu urafiki. Mie hata khanga ya mtu sivai!
 
Mambo ya kuazimana mnayawezaje jamani?

Kwanza hana uchungu na mali yako, pia unajua uendeshaji wake?

Naomba ukishalitengeneza uniazime na mie nina trip ya tandahimba loh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom